Wenye Hotels na Lodges hasa mikoa hii. Mablanket yenu huwa mnafua kweli?

Wenye Hotels na Lodges hasa mikoa hii. Mablanket yenu huwa mnafua kweli?

Arusha, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Njombe na Rukwa.

Haya mablanket yenu huwa mnafua kila mara kweli? Kuwa kila anapoondoka mteja mnabadilisha mnaweka jingine? Au tunaendelea kulalia na sisi wengine tukija?

Mimi sioni dalili ya kuwa haya yanabadilishwa. Nikiangalia hivi sioni kabisa hizo dalili. Naona tu kama kuna kuyatumia haya mpaka ukamilifu wa dahali. Sijui dahari. Mtajua huko huko.

Watu tunapata mpaka mafua. Siyo fair na mnatucharge pesa kama yote kwenye Hotels zenu.
Ukilala Mafinga ndiyo utajuta kuzaliwa. Yaani mablanketi ni machafu mpaka basi.

Niliwahi kuanzisha mpaka uzi hapa wa kuzilalamikia Lodge za Mafinga zilizopo Wilayani Mafinga, Mkoani Iringa. Nhingi hazifui kabisa mablanketi! Mbaya zaidi kuna baridi mwaka mzima.
 
Mimi huwa naamini Hotels za kuanzia Tsh 25000 Ni Safi na kweli sijawahi kukuta chafu
 
Hotel ni zile kama melia, point of sheraton,mount meru ila zingine ni lodges, na guest house, au hostel so watu kwa ushamba wao hawawezi kutofautisha na ndio maana wakitendwa wanadhani walikutana hotelini
Sawa, kwa kiasi Fulani Ni kweli,lakini believe me, Hotel sio lazima inafanane na hizo mnazodhani, Hotel sio lazima iwe three star+ au three stories building

Kwa mujibu wa Cambridge dictionary, Hotel is a building where you pay to have a room to sleep in, and where you can sometimes eat meals, hii Ina maanisha kwamba,Mimi hapa nikijenga Jengo langu la kawaida kabisa sio ghorofa,nikaweka ka restaurant humo na reception alafu vyumba nifanye elfu 25 kwa siku hii tayari Ni Hotel kwa sababu by definition sio lazima zile services zote za kwenye Hotel ziwepo isipokuwa Kama Kuna restaurant basi ni Hotel tayari

Wikipedia wanasema hivi kuhusu definition ya Hotel,A hotel is an establishment that provides paid lodging on a short-term basis. Facilities provided inside a hotel room may range from a modest-quality mattress in a small room to large suites with bigger, higher-quality beds, a dresser, a refrigerator and other kitchen facilities, chairs, a flat-screen television, and en-suite bathrooms. Small, lower-priced hotels may offer only the most basic guest services and facilities

Note
Small, lower-priced hotels may offer only the most basic guest services and facilities.

Hivo basi, sifa ya Jengo kuwa Hotel Ni kwamba watoe huduma za kulala pamoja na chakula, hii ndio sifa kubwa
 
Nilienda na maza flani Njombe kikazi. Anabeba mashuka yake, blanketi, taulo, neti. Yaani very complicated.

Wakati mi natumia mataulo ayo ayo na nipo nadunda.
The more sensitive the more vulnerable , vichaa na machizi huwa wanakula jalalani na hawadhuriki!!!
Hata mie huwa sijali sana mambo ya mashuka na utilities ninazozikuta kwenye lodge ila huwa na kuwa makini ninapochagua pa kulala
 
Back
Top Bottom