Wenye magari namba (A) tuwe waungwana tuyatoe barabarani ili TRA warudi kusajili (A) tena itakapo jaa namba D

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]mkuu umenichekesha sana, tuna mengi ya kufanyia kazi, sio namba A za magari.
 
Hizi namba ipo siku zitajaa. TRA wangekua wanasajili kwa mkoa.
 
Mkuu usajili wa magari si kama kula ndizi na kutupa maganda.
 
Point
 
Kuna gari mpya zina namba A, wanasema ni za wale jamaa.......kwa hiyo namba A isikutie wenge sana maana hata majuu zipo gari za kizamani na zina bei ya juu sana kuliko hizo mpya.
 
Na nyumba pia zibomolewe na kujengwa nyingine
 
Iyo ist yako namba D utaweka juu ya mawe mimi napeta na chuma changu.
 
Kuna gari mpya zina namba A, wanasema ni za wale jamaa.......kwa hiyo namba A isikutie wenge sana maana hata majuu zipo gari za kizamani na zina bei ya juu sana kuliko hizo mpya.
Hizo chache nimesema zitapewa plate number nyekundu kutofautisha usajili wa A njano
 
Mimi sidhani kama itakuwa sawa sababu tayari namba ilishatumika kwa mtu mwingine na huwezi jua matumizi ya gari yake yalikuwa ni yapi au kuna nini aliwahi fanya hapo awali. Ndiyo maana TRA wanautaratibu wa namba ambazo hazitumiki tena kuziondoa kabisa katika mfumo.Haiwezekani namba moja ikatumika katika magari mawili hata ukisema uweke pkate number nyekundu bado ni usumbufu na ukizingatia ndugu zetu wenye mavazi meupe barabarani unaweza jikuta umalipa fine kila siku kumbe kosa la mtu mwingine.
mfano mzuri sasa hivi parking wanascan plate number na kutuma taarida saver zao kisha mwenye gari unatakiwa tafuta wakala au simu kwenda lipia 500 TSH sasa fikiria hapo scan kama itakuwa na uwezo wa kujua rangi ya plate number zaidi inavuta namba tu.Utaratibu uliopo ni sawa kabisa na mpaka ikifika Z inawezekana kabisa hata number zikawa hamna ikawa kama bima kwa sasa unascan tu stika (bacode).
 
Na wewe ungekuwa gari si ungekuwa ulianzia TZA!? Kwa hiyo uuwawe kisa ni wa zamani!?
 
Yawezekana walishaanza kulifanyia kazi, maana nimekutana na V8 kilimo kwanza tatu kwa siku tofauti zinawaka kweli kweli zikiwa na namba ALK, AAF na AAR
 
Ha ha et kigari koko [emoji1][emoji1][emoji1]
 
Huu mji unashangaza kuna magari no C na D yamechoka sana na kuna Land cruiser no A na B bado zinawaka sana hasa V8
 
Katika hili hoja yako ni dhaifu sana haipaswi hata kujibiwa ila kwa kuwa tunakuheshimu acha watu wakujibu.

Herufi za magari zimeanzia AAA kwenye usajili wa sasa, inatazamiwa kwenda mpaka herufi ZZZ ndipo waangalie njia mbadala, ndio kwanza tupo D tunakaribia E. Wewe hofu yako nini?

Uchakavu wa gari haupimwi kwa usajili wa A au D bali efficiency na performace ya chombo husika. Hata kama utanunua gari ukasajili DX now kama hutolitunza basi mwenye A atabaki kuwa na gari zuri zaidi kuliko wewe.
 
Bongo hata ununue Prado la 2021 kwa 150M cash money lifike mjini na 10Km kwenye Dashboard ukimtafuta mteja wa million 100 tu hutakaa umuone na gari ni mpya kabisa haina hata week ndani ya Ardhi ya Tanganyika[emoji28]

Bongo tuna laana
Ujuaji mwingi ushamba mbele mkuu ndio laana inapoanzia[emoji16][emoji16]
 
Mimi nilinunua gari ya 2000 ilikuwa imetembea kilomita elf 17 tu, lakini kuna mtu ananunua gari ya 2015 iliyokwisha tembea kilomita laki tatu.....sasa kwenye maswala ya uchakavu ni gari ipi itakuwa imechakaa zaidi kati ya hizo gari mbili....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…