Wenye mazoea ya kutopokea simu mnakera, si uungwana, mbadilike!

Daaah mimi nahisi nina ugonjwa wa kutopokea sim yaaani kuna kipindi nikivurgwa huwa staki kabisa kuona simu yoyote mpaka ya mke wangu... saa hizi ndoa inapumulia mshine kisa simu... hebu tuambie dawa gani ya kuzuia hii kitu
 
Yaani huyu ni mdogo wangu kabisa, yeye kupokea simu huwa ni nadra sana. Yaani yeye hata simu kuwa hewani tu ni issue, unaweza kumtafuta hata week nzima usimpate labda umpigie mkewe kama yuko naye ndiyo ampe simu muongee. Ila kwa upande wangu, simu kwangu ndiyo hela so huwa siachi pokea simu ya mtu hata iweje, kuzima simu ndiyo huwa sifikirii kabisa
 
Labda wako busy, hawataki ongea nawe, simu iko mbali, iko silent au ina vibrate na hawamsikii!
Kwani hata hivyo lazima wapokee?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…