Heart Wood.
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 982
- 1,179
Ni kweli kuwa simu ni yako, ila unapokuwa kazini na umeandikisha namba yako kuwa ndio itumike kwa mawasilaino si busara kutopokea simu na huna sababu ya msingi ya kutopokea.
Hata mimi huwa sipokei kila wakati, inategemea na majukumu niliyonayo. Ila inapokwa muda wa kazi huwa nayapa kipaumbele mawasiliano yanayohusu kazi. Hivyo mtu yeyote anaponipigia muda wa kazi na nikajua ni mtu ninayehusiana nae kwa ajili ya kazi huwa nampa kipaumbele. Vilevile napokuwa nje ya kazi, huwa nayapa kipaumbele mawasilaino yanayohusu masuala ya kifamilia.
Sasa unakuta mtu anafahamu kabisa yeye anahitajika kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali ya kila siku juu ya majukumu ya kikazi. Ila akipigiwa simu kila siku haipokelewi. Hii si nzuri na watu wa namna hii mbadilike. Si ustaarabu na uungwana kabisa.
Au mnataka na sisi tuanze utamaduni wa kupeana appointment kwenye kupigiana simu? Kama tumefikia levels hizi kama ilivyo nchi za wenzetu basi weka wazi tuwe tunapeana appointment. Ila siyo kupigiwa kisha unaiangalia tu simu na kupuuza.
Nimemaliza uzi tayari.