Wenye miaka 30+ ni maswali gani hupendi kuulizwa ukikutana na mtu ambae hamjaonana kwa muda mrefu sana

Wenye miaka 30+ ni maswali gani hupendi kuulizwa ukikutana na mtu ambae hamjaonana kwa muda mrefu sana

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
  • class mates wa shule ya msingi / secondary
  • marafiki wa utotoni / secondary
  • Majirani
  • n.k

Mimi huwa nikikutana na mtu wa muda mrefu huwa nadeal na haya mambo

Nimefurahi kukuona baada ya miaka mingi, ni majaliwa kufika hadi tulipo

Ntakumbushia memories hasa tuliposaidiaana au aliponisaidia.

Tutapeana namba ya simu kwa msisitizo wa kuwasiliana kwa ishu muhimu

Imeisha hio
 
Unafanya kazi wapi?
Unakaa wapi siku hizi?
Una watoto wangapi ndugu?
Nimefurahi kukuona

Unakumbuka siku flani ulinisaidia kitu flani sijawahi kusahau

Naomba namba tuwe tunachekiana ishu muhimu

Vitu hivyo vinatosha kuwa sehemu ya mazungumzo, mambo ya kufatiliana unaweza kuambiwa "ninawahi sehemu flani"
 
1 .Umeoa
2.Umejenga
3.Unafanya kazi Gani..
Mi nilipokua Shure nilikua Nawaongoza ila kutokana na Hali ya kipato Home nikaacha shule Darasa la B.
Sasa wao walizani nimeenda soma shule ingine.
Tukikutana maswali kibao huwa inakera sana.
Tusalimiane tu uwe imeisha hiyo.
Salamu iwe Hi
Mambo------ Poa
Za masiku ----- Freshi
Imeisha hiyo Kila mtu atambae na mipango yake.
 
Back
Top Bottom