Wenye nyumba wamekuwa na hii tabia Kwa wapangaji wao

Lipa kodi wacha ulalamishi, mtu mwingine alijinyima akajenga na sasa hana ajira anategemea pesa za kodi halafu wewe unamletea nyenyenye.
 
Hapo mdau lazima kuwe kuna tatizo.

Kuja kuoneshana chumba wakati ukiwa bado mpangaji kuna mambo yafuatayo:
Mpangaji unazungusha kulipa kodi kwa wakati jinsi mlivyokubaliana kwenye mkataba.

Mwenye nyumba ashachoka na uongo uongo wako, hakutaki tena uendendelee kupanga hapo.

Mwenye nyumba hawezi kuleta kuonesha mtu mwingine wakati mkataba wa kuishi hapo haujaisha.
 
Yani suala linakuja pale ambapo umemwambia huongezi mkataba hapo ndo anapoanza kuleta watu kuangalia chumba
 
Lipa kodi wacha ulalamishi, mtu mwingine alijinyima akajenga na sasa hana ajira anategemea pesa za kodi halafu wewe unamletea nyenyenye.
Kodi inalipwa Tena Kwa wakati ukimwambia tu unahama hayo mambo ndo yanaanza kutokea
 
"No pain,no gain bro!!!".......hauwezi kujenga nyumba yako bila kupitia misukosuko na manyanyaso,,,,,nakumbuka zamani sana nikiwa mdogo,ata vidudud sijaanza tulikuwa tukiishi pa UBUNGO NHS,,,ila baba yetu aliweza kujenga sinza na tukahama,,issue ikabaki kwa wapangaji wenzake...kutokana serikali ilikwa haiwasumbui kuhusu malipo ya kodi,basi walibweteka mpaka wakistaafu wakiwa hapohapo,,,,yaani ilibidi watoto wakibalehe stoo na jiko zinageuzwa vyumba vya watoto,na mapishi yanahamishiwa nje!!!
 
Sawa broo
 
MKUUU ILE N UTASHI WENU ILA KUNA WENGINE WANAWEKA KWENYE MKATABA

MF

UNATOKA 30AUG
UJE KUOMBA UNA SHIDA NIKUPE SIKU 7[HIZI NAZO MJUE N UPENDO TU]
NDIO MAANA KAMA MM UNAHAMA UNANIAMBIA 3MNTHS KABLA

NA MWEZI WA MWISHO NARUHUSIWA KULETA MTEJA. A UNAKUWA UMESAINI KABISA
 
Labda lakini haipendezi
Kwa kweli haipendezi. Lakini una haki ya kumkatalia kuingia ndani ya nyumba yako. Labda kama kuna sehemu katika mkataba wenu wa upangishaji inayompa haki hiyo. Hata kama kipo ni vizuri ukisisitiza kuwa akutaarifu siku kadhaa kabla ya kuja na huyo mpangaji mtarajiwa.

Amandla...
 
Jenga ya kwako mkuu.Kupanga nyumba ni kama upo guest house.Kaza roho.
 
Sawa mkuu lakini anakuja kuomba sasa
Tatizo letu watanzania ni nidhamu ya uoga. Maana kama hupendi hiyo tabia ni simple tu akija kukuomba unamweleza tu kistaarabu kuwa “ kwa nia njema tu, kuwa unalinda faragha zako na hutopenda kila mtu akujue chumbani kwako”.
 
Umeongea ukweli kabisaa.
 
Kwani watu wanafanana vitu vya umiliki ktk chumba husikaa?
Afu sasa kwani lazima? Si hiyari ya mpangaji kuruhusu au laah.
 
N
Kwani watu wanafanana vitu vya umiliki ktk chumba husikaa?
Afu sasa kwani lazima? Si hiyari ya mpangaji kuruhusu au laah.
Ni busara kukaa vizuri na mwenye nyumba yako kama bado una mpango wa kuendelea kukaa. Na ni busara pia kwa mwenye nyumba kuto mkwaza mpangaji wake. Bahati mbaya siku hizi busara imekuwa adimu sana.

Amandla...
 
Ulifanya kosa kumwambia unahama, hapo madalali lazima wakusumbue.
 
Ulifanya kosa kumwambia unahama, hapo madalali lazima wakusumbue.
Mkataba unaonesha unaisha lini, kistaarabu lazima mmoja aseme iwapo hataongeza mkataba. Mpangaji wangu aliniambia hataongeza mkataba na mimi nikatangaza nyumba inapangishwa kuanzia tarehe atakayoondoka. Yaani akitoka yeye tu mtu anaingia, akapatikana mtu nae huko atokako kamaliza mkataba same day. Mpangaji mpya akaniambia anaomba kuona nyumba apate picha halisi nikamwambia siwezi labda umuombe huyo anaekaa akikukubalia kaangalie ila mimi siwezi kumuomba akuruhusu uingie. Wakaongea wenyewe wakakubaliana jamaa akaoneshwa nyumba alipotoka na yeye akaingia.
Kifupi ni maelewano tu. Mpangaji ana haki ya kukataa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…