Dunia inachange sana, style ya maisha hubadilika kila uchwao,kwa hali na maisha ya kitanzania kusave pesa ya kutosha kukidhi mahitaji ya kuja kuhonga uzeeni ni kazi, kumbuka ukiwa mzee huna mvuto tena, hata ukifanya biashara hawanunui, nani atanunua bidhaa za mzee wakati kutakuwa na vijana wa wakati huo wenye mvuto na mawazo mapya na mbinu za wakati huo?
Ramani unazozipata leo ukiwa na age mate wako ukiwa mzee hutaweza ku compete na vijana,
Unachotakiwa kufanya mda huu ni kutengeneza familia na uwe na bond na kizazi chako, ujue wameamkaje , wanakula nini, mtoto akianguka umwinue mpe pole jenga uhusiano ili uweke akiba ya fadhila kwenye moyo wake. Usiseme kuwa hatakujali na ukanipa mifano uchwara, Zimwi lokujualo halikuli likakwisha
Ukizeeka hata akili zako hazitafanya kazi vizuri, utaanza kujinyea na utahitaji pampas, utapata stroke , sijui binti wa wap ndogo atakutunza kwa hali hiyo na sijui utampa shilingi ngapi, ila kati ya utakaowazaa yupo mmoja tu Mungu atampa roho ya kukuhudumia.
Labda kama utakataa ndoa basi omba Mungu ufe mapema, hapo ntakuunga mkono.