hawana shida hawa majamaa, ila tu wanapenda kuona mtu yupo active kwenye eneo lake, hata kama kazi kwa muda huo imeisha ila atleast uwepo wako unaonekana. Changamoto nyingine hawa majamaa wengi wao ni wagumu kutoa bonus.
By uwepo wako kuonekana wanamaanisha;
1) Hakuna kuumwa.
2) Malipo ya overtime ni kulazimishana na kutafutana.
3) Muda wote uonekane kuna kitu unafanya.
4) Huna kitu cha kufanya? Njoo unifanyie masaji au jifiche.
5) Unatarajiwa ufanye kila kazi atakayoitaka.
6) Hamna likizo ili uwepo wako uonekane vizuri.
7) Kesho off yako ila inabidi uingie kazini kama hutaki kazi basi. Hawasemi nakufukuza wanasema kazi basi
8) Umerundika off nyingi? Kwahiyo unahitajika kulipwa over time? Ngoja nijadiliane na meneja wako.
9) Muda wa kuingia ni saa moja asubuhi. Kutoka ni majaliwa.
Niliwahi fanya kazi resta moja hivi wale jamaa walikua ni kwikwi resta ikawa inawashinda wakauza kwa mhindi mwenzao. Huyu wa sasa alikua poa zaidi, ukifika muda wa kuondoka anahimiza watu muondoke.
Ukibaki over time yako on time.
One day akakuta nimesinzia (jana yake kulikua na party so waiters tulikesha) sehemu akaniuliza kama niko sawa kwa kuhofia kuonekana mzembe nikasema naumwa. Akaniambia nirudi nyumbani, nikahisi ndiyo nimefukuzwa nikawa naranda randa mule mule.
Akaniona tena akaniuliza kwanini sijaondoka wakati naumwa? Nikamjibu nahisi kizunguzungu jamaa akanikodia taxi hadi home. Na kesho yake napigiwa simu na meneja wa waswahili ananiuliza naendeleaje (kwa maelekezo ya bosi)
Yaani ghafla nikawa nimeexperience wahindi wawili kwa mara moja turns out mhindi mpya na mkewe hawakukulia na kuishi India, wamekulia Uk huko. Ila wale wa kwanza ni wakazi wabobevu wa Bombay.