Naungana na mtoa mada...wanaume wengi ndo tunaowalemaza akili wanawake kwanzia wakiwa watoto(mtoto wa kike anahitaji kua karibu zaidi na baba) mpaka wakiwa wakubwa kuwafanya wategemee akili za wanaume moja kwa moja utadhani Mungu alitupendelea akili wakati alitupa wote sawa.
Hiyo imepelekea wanawake wengi mno(japo sio wote)kua vilema wakutumia akili zao ipasavyo,akili na fikra zao zimeshajengeka kupewa,kutegemea fikra za wanaume,wao ni kuwaza kuvaa,kula,vitu vizuri tu!
Katika kutumia fikra zetu huhitaji kua na uume na pum** bali ni akili akili ambayo kila mwanadamu amepewa bila upendeleo wowote ule.
Siku mumeo akifa,akifukuzwa kazi,akifilisika,akiumwa hoi kitandani au chanzo unachokitegemea utafanyaje kama sio kutoa mwili wako kwa wanaume wengine ili ujikimu kimaisha!?
Nyie wanaume wenzangu mnaosema wanawake eti ni maua,mnawalemaza mno aisee.mwanaume ni jukumu lake kuitunza familia yake kwa kila kitu asilimia 100 ila usimuache mkeo alemae akili zake bila kua na kitu chakufanya kumuingizia kipato kabisa.siku ukikwama je?ukiumwa hoi kitandani?ushafikiria siku ukifa je watoto wenu watakula nini?watasoma?watakua na maisha gani?
Au mnategemea watatunzwa na ndugu zenu au kanisa na misikiti!?
Huu hapa chini ni mfano uliopo kwenye biblia juu ya mwanamke mjane mmoja ambae mumewe alikua mchungaji amekufa amemuacha mkewe na hali mbaya ya kiuchumi,madeni mengi ambayo aliingia mkataba watoto wakawe watumwa endapo atashindwa kuyalipa.so akamfwata nabii Elisha amsaidie juu ya hali yake kisa tu mumewe alikua mtumishi wake.
Ambapo alipewa ushauri wakujikomboa kwenye hali ngumu kwa vitu ambavyo alikua navyo nyumbani kwake ila hakuviona thamani yake au kuviangalia kwa jicho jingine sababu ya kulemaa fikra zake kutegemea kila kitu toka kwa marehemu mumewe.
Kwa dunia ya sasa nawaambieni wake zenu wataliwa mno ili kuwalea wanao!
2 Wafalme 4:1-7
Basi, mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wana wa manabii alimlilia Elisha, akasema, Mtumishi wako mume wangu amekufa; nawe unajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa mcha BWANA; na aliyemdai amekuja ili ajitwalie wana wangu wawili kuwa watumwa. Elisha akamwambia, Nikufanyie nini? Niambie; una kitu gani nyumbani? Akasema, Mimi mjakazi wako sina kitu nyumbani, ila chupa ya mafuta. Akasema, Nenda, ukaazime vyombo huko nje kwa jirani zako wote, vyombo vitupu; wala usiazime vichache.
Kisha uingie ndani, ukajifungie mlango wewe na wanao, ukavimiminie mafuta vyombo vile vyote; navyo vilivyojaa ukavitenge. Basi akamwacha, akajifungia mlango yeye na wanawe; hao wakamletea vile vyombo, na yeye akamimina. Ikawa, vilipokwisha kujaa vile vyombo, akamwambia mwanawe, Niletee tena chombo. Akamwambia, Hakuna tena chombo. Mafuta yakakoma. Ndipo akaja akamwambia yule mtu wa Mungu. Naye akasema, Nenda ukayauze mafuta haya, uilipe deni yako; nayo yaliyosalia uyatumie wewe na watoto wako.
Sent using
Jamii Forums mobile app