GE2025 Wenyeji wa Mikoa ya Kaskazini Wana Haki ya Kuongoza Majimbo Yao

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Akili fupi kama za Babu Talee!
Akili yako ndogo kama kisoda!!
Zama hizi bado unawaza kikabila kabila!!
Tafuta wachawi wenzako wa kabila lako mkatambike ila kwenye masuala ya UBUNGE kaa pembeni kabisa kwani maarifa yako na upeo wako ni mdogo sana na hauna nafasi!!
Mtu anakuwa au anagombea UBUNGE popote anapoona ana ushawishi na wenzake katika Jimbo hilo wanaweza kumpa nafasi ya kuwawakilisha.
Hapa Tanzania hakuna Jimbo lolote wanakoishi watu wa kabila moja tu! Nasema HAKUNA!
Wewe mkabila tafuta Nchi yako na Chama chako cha Ukabila.
Kaa mbali kabisa na mambo ya CCM na Uongozi wa Tanzania kwani wewe ni kirusi kinachotakiwa kutokomezwa haraka sana!
 
Toa mfano acha porojo. In short Arusha wamebakwa mwaka huu
Kumbe hata historia ya kisiasa huijui unaropoka tu na ukabila wako
Fuatilia majimbo ya Dar na Mwanza
Fuatilia Mrema aliwahi kuongoza Jimbo Gani nje ya kaskazini

Tukirudi Arusha usiwaingizie ukabila wako kwa kukosa hoja
Watu wa Arusha wanajitamnua ni Jimbo lenye historia ya kipekee
Liliwahi kuongozwa Hadi MTU wa Mara huko

Ukabila Unaotaka Arusha kwa mgongo wa ukaskazini achana nao kabisa ni upuuzi

Lema ni mwenyeji wa Hai Kilimanjaro mmchame lakini Alipewa ubunge Arusha lenye asili ya waamasai na wameru
 
Hizi ni ishara za jamii zenye superiority complex kujiona wao Bora kuliko jamii nyingine.

Ninyi mnaongoza majimbo ambayo siyo ya kwenu kiasili ila watu hawana shida, Ili ninyi kuongozwa na wengine imekuwa nongwa?

Kuliwa kuliwe kwa mwali tu, ila kungwi aaah
 
Naunga mkono hoja. Hizi mafasi za ubunge zinahitaji hasa mtu ambaye kama sio mzawa, basi awe mzawa kanda ama walau ameisha sehemu husika kwa miaka walau 20 hivi mfululizo.
 
Bila shaka wewe ni akili kubwa na kamanda wetu CHADEMA huko Arusha..
 
Nakuunga mkono, ila imenisoma hapa?Mkuu wa Mkoa wa Arusha (Batilda Buriani) na ukabila; Ukemewe na kila mmoja wetu! humo nimetoa na mfano Sasa kama wenyeji hawana uwezo,lazima wasaidiwe!。

P
 
Wacha tuone
 
NATAKA NIMKATIE KAENEO KANGU DR.SAMIA,HAPA MARANGU KAMA EKARI 2,HIVI AJE AJENGE NYUMBA YAKE HAPA,AKICHOSHWA NA JOTO,AWE ANAKUJA KUPUMZIKA HAPA MARANGU.
 
Naunga mkono hoja. Hizi mafasi za ubunge zinahitaji hasa mtu ambaye kama sio mzawa, basi awe mzawa kanda ama walau ameisha sehemu husika kwa miaka walau 20 hivi mfululizo.
Nyumbu katika ubora wake!
 
We ni mpumbavu wa kiwango cha uprof, watanzania yote wangekuwa wanawaza kama ulivyo wewe mwenyewe hapo pamoja na ukoo wako wangepata taabu sana. Uone aibu
 
Kama Makongoro Nyerere alikuwa Mbunge Arusha Mjini mwaka 1995 ni ajabu miaka 30 baadae waibuke watu wajinga kuwazidi wale wa 1995.
 
Watu wakieleza ukweli mnasema ukabila!

ukabila unatokea wapi wakati ni ukweli.

Awamu ya 5 ya Msukuma mwenzio ambao ulikuwa nanukabila kwa kubagua mokoa ya Kaskazini mbona ukukemea?????
Nani alibaguliwa? Nyinyi ni Wabaguzi miaka yote.
Mwacheni Makonda na Usukuma wake awe Mbunge.
 
Basi na Dar-es-Salaam wagombee wenyeji kama wazaramo
 
Watu wa mikoani tuamke, haiwezekani wauza uchi wa Dar inapofika kipindi cha uchaguzi wanakimbilia mikoani kuchukua fomu za uongozi kisha wabarudi Dar kuishi,tuwakatae asubuhi na mapema.
Wachukue fomu hukohuko Dar kwao.
 
Soma tena sifa za kuwa Mbunge kisha ujenge hoja yako vizuri.
 
Unahubiri ukabila na ukanda ndugu mleta mada. Kila mtanzania ana haki ya kuishi na kugombea ubunge mahala popote kwenye Jimbo lolote.
Kajaribu huko Biharamulo au Newala kama utapita kisa mtanzania! Utoke huko kwenu uje ugombee kwetu upewe eti kuonyesha hatuna ukabila au ukanda. Jimbo letu ufanye ndio ganzi ya kupandia matamanio yako. Kama unawiwa kuwasaidia wananchi kanzie kwenu ambako wanashida kama sehemu nyingine. Ilala kwenyewe katika ya jiji hupewi kama sio mdau. Arusha wanajifanya wajanja lakini wanamatatizo ya akili.
 
Acha ndoto zako cha mchana kuna mtanzania hawazi ukabila. Kama ukabila haupo kwanini wasukuma, waha, wajita, wasambaa, wangunya... bado wanatajwa Tanzania. Nyerere mwenyewe alishindwa kufuta ukabila utakuwa wewe. Kukaa mjini hakuna maana kwamba umejifuta kwenye kabila lako. wazaramo dar pamoja na kwamba walianza kujichanganya na watu wengine zaidi ya miaka mia iliyopita lakini bado wanajimbua kama wazaramo na wako proud
na kabila lao. Wananchi wa Tanzania wanajitambua kwa makabila yao, hizo stori zenu za kwamba Tanzania hakuna ukabila pigeni kwenye vijiwe vya kahawa au baa mkiwa mnalewa lakini mpaka sasa ukabila upo na watu wako proud na makabila yao.
 
Mbona Dar karibu majimbo yote yana wabunge siyo Wazaramo?
Achana na Dar kwa akili yako Kuna Mzaramo mwenye akili timamu ya kuwa mbunge nani acheze ngoma. Kuna jamii hapa bongo by default niwakutawliwa tu hasa huku pwani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…