Wenzangu mnaombaje mpaka maombi yenu yanajibiwa?

Wenzangu mnaombaje mpaka maombi yenu yanajibiwa?

Habari ndugu zangu

Naomba kuelekezwa namna ya kuomba maombi yangu yakajibiwa,kama kusali nasali sana,kufunga nafunga sana,kutoa sadaka natoa ila maisha yangu yameandamwa na magonjwa ya ajabu,kutofanikiwa na kukosa kazi

Sasa wapi ninakosea au mimi sijui kuomba ndugu zangu,kwani ninyi mnafanyaje?

Asanteni
Ulishaenda kwa Mwamposa?
 
Uwe na imani uwe mvumilivu.
Kuna mkuu wangu wa kituo cha kazi alikuwa abanibania saba semina na vikao. Ikafika kipindi semina za kwenda mimi anamtuma mwingine jamaa anakula per diem ya siku hadi 20 ilifika kipindi nikatafuta mtu wa kunishauri nifanye nn. Priest moja akaniambia kwenye mahakama za duniani utadhulumika ila sio mahakana za mbinguni, nenda kanshitaki kwa MUNGU. Aisee sifurahii yanayompata ila jamaa anateseka. Na mm semina za vikao kila mwezi. MUNGU anajibu maombi
 
Mungu hujibu maombi kwa wakati wake hachelewi wala hawahu

Soma hii itakusaidia sana

Thread 'Miaka ya neema, miaka ya uharibifu' Miaka ya neema, miaka ya uharibifu
Katika ulimwengu wa Roho maombi huwa yanajibiwa kwa wakati huku kwenye mwili sio kwamba mambo yanachelewa ila vile Mungu huwa anaandaa njia mpya ya mtu kupata mafanikio tofauti na matarajio ya wengi
 
Kuomba ni kujifariji tu, kwanza unamuomba nani?

Mungu? Mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote?

Kama yupo, kwa nini umuombe? Ina maana hajui matatizo yako?

Huoni kwamba kitendo cha kumuomba huyo Mungu ni uthibitisho kwamba huyo Mungu hayupo, na angekuwepo usingehitaji kumuomba, angekupa unachotaka kabla hujajua unakihitaji, na kile ambacho si kizuri kwako hata usingekitaka?

Huoni kwamba kumuomba Mungu ni uthibitisho kwamba Mungu hayupo?
Kawachote wajinga wewe
 
Kwa huu mwandiko huu utasuburi sana kujibiwa, naona uchungu, majuto na kukata tamaa
 
Self Fulfilling Prophecy..., Ukifanikiwa ni maombi yamefanya kazi usipofanikiwa haujui kuomba....

Moja the notion kwamba Mungu (ambaye hapendelei na ni Supreme Being) kusema kwamba anawapa wengine na wewe hakupi au anapenda kubembelezwa goes against being a supreme....

Mbili Chochote kile ukikifanya kwa usahihi (kanuni zake) iwe wizi, cut corners, playing rough n.k. (utafanikiwa no matter umeomba au haujaomba)

Mwisho kabisa confidence inasaidia kama utaamini kuna supreme power inakusaidia utapata confidence na utakuwa kwenye better position ya kufanikiwa kuliko asiye na Imani (Confidence)
 
Habari ndugu zangu

Naomba kuelekezwa namna ya kuomba maombi yangu yakajibiwa,kama kusali nasali sana,kufunga nafunga sana,kutoa sadaka natoa ila maisha yangu yameandamwa na magonjwa ya ajabu,kutofanikiwa na kukosa kazi

Sasa wapi ninakosea au mimi sijui kuomba ndugu zangu,kwani ninyi mnafanyaje?

Asanteni
Kila jambo na wakati wake ndugu, zamu Yako ipo karibu....ukiona Giza linazid kuwa nene ujue kunakaribia kupambazuka.....usikate tamaa.
 
Eti Mungu anatenda kwa kusikiliza maombi yetu sasa hapo Mungu ni mimi ninaemumulisha atende hiki dhidi yangu au Mungu ni yeye
 
Habari ndugu zangu

Naomba kuelekezwa namna ya kuomba maombi yangu yakajibiwa,kama kusali nasali sana,kufunga nafunga sana,kutoa sadaka natoa ila maisha yangu yameandamwa na magonjwa ya ajabu,kutofanikiwa na kukosa kazi

Sasa wapi ninakosea au mimi sijui kuomba ndugu zangu,kwani ninyi mnafanyaje?

Asanteni
Achana na kuomba, fanya action.
 
Usitake ushauri kwa Wanadamu Ndugu yangu wote ni wanafiki... Watakuektia mara oohoo omba hivi, Mara oohoo acha DHAMBI wakati wao ni waovu zaidi yako. Na pia wakipata shida ni wa kwanza kulalamika lakini kwenye KEYBOARD wanajifanya wema
Cha msingi endelea kujifunza zaidi kuhusu ulimwengu na ujaribu kuongea na Babu zako au Bibi zako waliotangulia huenda ukapata nafuu, Kuliko kumwamini Mungu ambaye ameshindwa kuwasaidia watoto wasiokuwa na hatia GAZA, Vilema pale KIMARA, Hata wale waliokufa maji MV BUKOBA. EPUKA USHAURI KUTOKA KWA WANAFIKI WANADAMU
 
Iko hivi mtu wa Mungu,wewe ni mmoja ya wale wanaofikiria kuwa watu wenye pesa na mali,majumba na kazi nzuri,pamoja na uzima wa afya ni watu waliobarikiwa na Mungu,ukiona unapitia magumu na unamuomba Mungu huku unaishi maisha ya haki na kweli,juwa kuwa Mungu amekukubali,anachokifanya ni kutaka kuhakikisha kuwa uko serious au ukikutana na majaribu utamuacha,usiwazie sana haya maisha ya hapa duniani,wazia kule mbinguni unakotakiwa kwenda,simama imara na huo msimamo wako,hivyo unavowazia sana na kuumiza kichwa ni vya hapa duniani na kila mtu ataviacha,huo ugonjwa pia utapita,wakati wa Mungu ndio wakati sahihi,usikate tamaa,inawezekana kabisa uko karibu kabisa na kuifikia baraka yako lkn shetani anataka kukukatisha tamaa...
Huyu jamaa Yuko sahihi, Mungu anakuwazia mema, kuwa mvumilivu, ukitoka relini kwisha habari yako
 
Habari ndugu zangu

Naomba kuelekezwa namna ya kuomba maombi yangu yakajibiwa,kama kusali nasali sana,kufunga nafunga sana,kutoa sadaka natoa ila maisha yangu yameandamwa na magonjwa ya ajabu,kutofanikiwa na kukosa kazi

Sasa wapi ninakosea au mimi sijui kuomba ndugu zangu,kwani ninyi mnafanyaje?

Asanteni
zawadi ya uhai, ulinzi na afya anayokujalia ni sehemu tu kidogo ya majibu ya maombi na ibada zako kwa Mungu.
Mshukuru Mungu kwa kila Jambo 🐒
 
Back
Top Bottom