Wenzangu mnaombaje mpaka maombi yenu yanajibiwa?

tumia vifungu vya.baible na maombi ya uchonganish
 
Ulishaenda kwa Mwamposa?
 
Uwe na imani uwe mvumilivu.
Kuna mkuu wangu wa kituo cha kazi alikuwa abanibania saba semina na vikao. Ikafika kipindi semina za kwenda mimi anamtuma mwingine jamaa anakula per diem ya siku hadi 20 ilifika kipindi nikatafuta mtu wa kunishauri nifanye nn. Priest moja akaniambia kwenye mahakama za duniani utadhulumika ila sio mahakana za mbinguni, nenda kanshitaki kwa MUNGU. Aisee sifurahii yanayompata ila jamaa anateseka. Na mm semina za vikao kila mwezi. MUNGU anajibu maombi
 
Mungu hujibu maombi kwa wakati wake hachelewi wala hawahu

Soma hii itakusaidia sana

Thread 'Miaka ya neema, miaka ya uharibifu' Miaka ya neema, miaka ya uharibifu
Katika ulimwengu wa Roho maombi huwa yanajibiwa kwa wakati huku kwenye mwili sio kwamba mambo yanachelewa ila vile Mungu huwa anaandaa njia mpya ya mtu kupata mafanikio tofauti na matarajio ya wengi
 
Kawachote wajinga wewe
 
Kwa huu mwandiko huu utasuburi sana kujibiwa, naona uchungu, majuto na kukata tamaa
 
Self Fulfilling Prophecy..., Ukifanikiwa ni maombi yamefanya kazi usipofanikiwa haujui kuomba....

Moja the notion kwamba Mungu (ambaye hapendelei na ni Supreme Being) kusema kwamba anawapa wengine na wewe hakupi au anapenda kubembelezwa goes against being a supreme....

Mbili Chochote kile ukikifanya kwa usahihi (kanuni zake) iwe wizi, cut corners, playing rough n.k. (utafanikiwa no matter umeomba au haujaomba)

Mwisho kabisa confidence inasaidia kama utaamini kuna supreme power inakusaidia utapata confidence na utakuwa kwenye better position ya kufanikiwa kuliko asiye na Imani (Confidence)
 
Kila jambo na wakati wake ndugu, zamu Yako ipo karibu....ukiona Giza linazid kuwa nene ujue kunakaribia kupambazuka.....usikate tamaa.
 
Eti Mungu anatenda kwa kusikiliza maombi yetu sasa hapo Mungu ni mimi ninaemumulisha atende hiki dhidi yangu au Mungu ni yeye
 
Achana na kuomba, fanya action.
 
Usitake ushauri kwa Wanadamu Ndugu yangu wote ni wanafiki... Watakuektia mara oohoo omba hivi, Mara oohoo acha DHAMBI wakati wao ni waovu zaidi yako. Na pia wakipata shida ni wa kwanza kulalamika lakini kwenye KEYBOARD wanajifanya wema
Cha msingi endelea kujifunza zaidi kuhusu ulimwengu na ujaribu kuongea na Babu zako au Bibi zako waliotangulia huenda ukapata nafuu, Kuliko kumwamini Mungu ambaye ameshindwa kuwasaidia watoto wasiokuwa na hatia GAZA, Vilema pale KIMARA, Hata wale waliokufa maji MV BUKOBA. EPUKA USHAURI KUTOKA KWA WANAFIKI WANADAMU
 
Huyu jamaa Yuko sahihi, Mungu anakuwazia mema, kuwa mvumilivu, ukitoka relini kwisha habari yako
 
zawadi ya uhai, ulinzi na afya anayokujalia ni sehemu tu kidogo ya majibu ya maombi na ibada zako kwa Mungu.
Mshukuru Mungu kwa kila Jambo 🐒
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…