Wewe kijana Acha Upuuzi wa Kupoteza Muda, Amka Upige Pesa!

Wewe kijana Acha Upuuzi wa Kupoteza Muda, Amka Upige Pesa!

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
533
Reaction score
1,499
wanangu, hebu tusidanganyane hapa mtaani. Maisha ya sasa hayana pause wala rewatch, yanakwenda mbio kuliko sana. Unajikuta kijana unakomaa kutwa nzima kwenye vijiwe vya kahawa unajadili mipango ya mpira au unapoteza data kusubiri miujiza kwenye mitandao ya kijamii wakati mfuko wako unasoma zero balance. Kaa ukijua, hakuna mtu atakayekuja kukushika mkono kama wewe mwenyewe hujasimama kwenye nafasi yako na kuamua kubadilisha mchezo.

Mimi mwenyewe nina Master’s yangu ya Project Management hapa, nimepita kupitia mikikimikiki mingi sana kuanzia kusoma Diploma in Marketing Management mwaka 2018, kutembea mbugani na kumaliza Degree in Wildlife Tourism mwaka 2021, kupiga kazi ngumu za Mountain Tour Guide course ya Septemba 2022, mpaka kutulia na vyeti vya nguvu vya Digital Marketing kutoka Harvard Business School Online. Na bado nina miaka 6 ya uzoefu kwenye digital marketing na web design, lakini bado nakaza kila siku kwa sababu najua ukizingua hakuna cha maana kitakachotokea. Sasa inakuwaje wewe unayepoteza masaa kumi kwa siku unapiga soga zisizo na mwelekeo?

Acha kabisa upuuzi huo, ikae kichwani kuwa dunia ya sasa inamheshimu mtu mwenye mindset ya kibabe, anayetafuta solutions badala ya kulalamika kuwa maisha magumu. Amka sasa hivi, achana na mambo ya kijinga yanayokula muda wako wa thamani, ingia kwenye grind halisi upige pesa maana muda ni mali na hakuna wa kukusaidia zaidi ya jasho lako mwenyewe!
 
Amka upige nimekimbia chap kuja sijaona hiyo sehemu ya pesa
 
Back
Top Bottom