Wewe Mbosso haya mambo yako ndiyo yalisababisha bwana Marioo alifuta verse zako kwenye nyimbo zake mbili

Konde kabadilika saana....huwa anazi
Muziki ni kama Gari the more you drive the better you become. Hata Mario anaimprove siku hadi siku.

Sisemi hawajui muziki kabisa wanajitahidi kwa uwezo wao. Kuna wasanii wape beat yoyote kitachopikwa studio kinasikilizika sasa hawa jamaa zako wafikirie tu uwape beat mbaya mbaya....nakuhakikishia husikilizi hiyo ngoma.
 
kweli mkuu
Marioo aliyeimba "Dar Kugumu", "Aya" na "Inatosha" aliingia chimbo na kuanza kuachia amapiano, aligeukia muziki wa vibes na si kufanya watu wapende uandishi wake.

Ukisikiliza "Beer Tamu", "Mama Amina", "Sumu", "Adiwele" , "Lonely" na nyimbo zake nyingi za amapiano utaelewa kwamba alichagua [Marioo] njia mpya. Kiutunzi bado yupo vizuri.

Mbosso alianza kubadilika kwenye wimbo wa "Moyo", kisha "Shetani" hatukukaa sawa akashusha "Sitaki" na "Sele", tofauti yake na Marioo ni moja tu. Marioo tangu alipoangukia upande wa amapiano ni kama hataki kuandika tena kama zamani. Ila upande wa Mbosso yeye hata aliporejea kuimba mziki wa Bongofleva/Afrobeats aliendelea kuandika kwa utaalamu wake ule ule.

Usimdogoshe Marioo!
 
Mkuu hata wewe upewe biti mbaya kuna uwezekano ukayakanyaga tu!, msanii yoyote lazima achague biti anayoiweza ndio maana wana style za kuimba huyu rap, mapiano, R&B n.k
msanii hapimwi kwa beat anapimwa kwenye kuimba live kufuata sheria zote zakimuziki.. mi kuna baadhi ya nyimbo zimepikwa studio sijazielewa lkn msanii huyohuyo akiipiga live unakuta naikubali hiyo ya live.. nafikiri kila mtu na sikio lake kwenye muziki lkn nikuibie siri ndogo pia aina ya muziki mtu anaopenda kusikiliza na wanamuziki fulani fulani anaopenda kuwasikiliza, huelezea kwa kiasi fulani uwezo wa akili wa mtu huyo!.
na hichi kitu ni automatic huwezi ku fake..😅
 
Anatamani apime uwezo wa Adele, Usher, na Chris Brown kwenye midondoko ya singeli.
 
Anatamani apime uwezo wa Adele, Usher, Chris Brown kwenye midondoko ya singeli.
wataangukia pua tu!.. wasanii wana style zao na ndo wanapobase sasahivi wamebakiza mziki wakuimba soft sio kama wa akina Celine Dion watu wanapanda mpk key za juu huko!.. hizo enzi zilikuwa na mambo yake najua huwa zinarudi uzuri mziki unafundishika na sauti inafunguliwa vizuri tu.
 
Wewe unajua Muzik huyo dogo hajua kuimba technology inamboreshea saut
Upo sahihi kuandika unachofikiri, Marioo ni kijana aliyetambua kwamba kinyume na jamii itavyomchukulia ana nafasi yake katika mto huu wa muziki.

Kuimba ni sanaa, sanaa inafundishika. Ukitoa teknolojia uliyoitaja kumsaidia Marioo muziki una tabia ya kuwatenga wasio na vipaji, kwa miaka hii kadhaa ambayo Marioo amekaa kwenye hii tasnia mpatie heshima yake.
 
Ila tukubali Mario kajisahau ameanza kutoa maronya
 
Mkuu mbona marioo anaimba fresh tuu na anapini kibao, ingawa amapiano zinampenda Ila Kwa sisi ambao tulianza kumsikiliza marioo tangu anaimba nyimbo za kulia lia tunamwelewa
 
Mkuu mbona marioo anaimba fresh tuu na anapini kibao, ingawa amapiano zinampenda Ila Kwa sisi ambao tulianza kumsikiliza marioo tangu anaimba nyimbo za kulia lia tunamwelewa
Marioo wala si msanii mbaya ila mbosso khan kilungi na marioo tz nani ni bora ?
 
Kuna Huu wimbo kaimba na Yammy nimetamani watoe EP aiseee Kuna vocal na Nashauri mazuri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…