Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Katika familia, gharama hazipo kwenye kuzaa tu; bali gharama zipo kwenye malezi.
Na kwa mazingira ya sasa, unaweza kuta kijana ana miaka zaidi ya 30, lakini bado anaishi kwao, huku akiendelea kuwapa mzigo mzito wazazi wake.
Kwa nini nasema wewe ndio chanzo cha umasikini wa kwenu; ni kwa sababu gharama zilizotumia kukuza au kukulea wewe, ni gharama kubwa ambazo wazazi wako wangewekeza kwenye ujenzi wa viwanda, tungekuwa na bidhaa nyingi huko nje ya nchi na tungepata fedha za kigeni.
Mfano:-
Chukulia kwa siku unatumia 10,000/=
Mwaka una siku 365
Kukaa kwa wazazi mpaka kujitegemea, chukulia miaka 30
Fedha/nguvu zilizotumika kwa wazazi = 10,000 x siku 365 x miaka 30
=109, 500,000/=
Hii ina maana, mtu mmoja mpaka aje aondoke kwa wazazi wake, atakuwa ametumia kiasi kisichopungua Tsh. 109,500, 000/=
Kama mmezaliwa saba (7), ina maana wazazi wenu mmewabebesha mzigo wenye thamani ya Tsh. 766,500,000/=; kwa hiyo kama wanaishi kwenye mazingira mabovu, kaa ukijua, chanzo chao cha umasikini ni wewe.
Ndio maana matajiri hawazai watoto wengi, sio kwamba wana akili sana, bali wanaepuka gharama hizo nilizoziainisha hapo juu.
Kwa hiyo, usiwalaumu wazazi wako, kwa sababu chanzo chao cha umasikini ni wewe.
Karibuni kwa hoja.