Wewe ndio chanzo cha umasikini katika familia yenu

Wewe ndio chanzo cha umasikini katika familia yenu

Kama wewe umeweza kutoka kwenu mapema na kwenda kujitegemea ni jambo la kumshukuru mungu lakini kamwe usitumia hiyo fursa uliyoipata kama fimbo ya kuwatandikia ambao bado wapo makwao .

Watu kubaki kwao siyo kama wanapenda ila ni changamoto tu za kimaisha ndyo zimepekekea wawe hapo walipo , mfano katika umri huo wapo waliomaliza vyuo lakini mungu hajawafungulia milango ya wao kupata kazi , wapo waliojaribu kuanzisha biashara lkn kutokana na mazingira kutokuwa rafiki biashara zimeanguka hivyo sababu ni nyingi ..

Mwisho unapofanya kitu na kikafanikiwa siyo kwamba wewe ndyo umefanya vizuri kuliko wengine hapana bali ni baraka za mungu zimekuwa upande wako hivyo jitahidi kuombea na wengine waipite hyo changamoto na siyo kuwasengenya ...
Basi tuongeze iwe miaka 45
 
Katika familia, gharama hazipo kwenye kuzaa tu; bali gharama zipo kwenye malezi.

Na kwa mazingira ya sasa, unaweza kuta kijana ana miaka zaidi ya 30, lakini bado anaishi kwao, huku akiendelea kuwapa mzigo mzito wazazi wake.

Kwa nini nasema wewe ndio chanzo cha umasikini wa kwenu; ni kwa sababu gharama zilizotumia kukuza au kukulea wewe, ni gharama kubwa ambazo wazazi wako wangewekeza kwenye ujenzi wa viwanda, tungekuwa na bidhaa nyingi huko nje ya nchi na tungepata fedha za kigeni.

Mfano:-

Chukulia kwa siku unatumia 10,000/=

Mwaka una siku 365

Kukaa kwa wazazi mpaka kujitegemea, chukulia miaka 30

Fedha/nguvu zilizotumika kwa wazazi = 10,000 x siku 365 x miaka 30

=109, 500,000/=

Hii ina maana, mtu mmoja mpaka aje aondoke kwa wazazi wake, atakuwa ametumia kiasi kisichopungua Tsh. 109,500, 000/=

Kama mmezaliwa saba (7), ina maana wazazi wenu mmewabebesha mzigo wenye thamani ya Tsh. 766,500,000/=; kwa hiyo kama wanaishi kwenye mazingira mabovu, kaa ukijua, chanzo chao cha umasikini ni wewe.

Ndio maana matajiri hawazai watoto wengi, sio kwamba wana akili sana, bali wanaepuka gharama hizo nilizoziainisha hapo juu.

Kwa hiyo, usiwalaumu wazazi wako, kwa sababu chanzo chao cha umasikini ni wewe.

Karibuni kwa hoja.​
Swali: [emoji117] mtoto anacha kuwa tegemezi kwa wazazi kwa asilimia kubwa akiwa ana miaka mingapi iwe wakike ama kiume .....hasa wakiume
 
Watu wanawez kukaa mpka zaidi ya miaka 30 hata pengne kuzeekea nyumbna Kwa juu 2 ambazo nazifaham

1. Pengne huyo ndo chanzo wazazi wake kula na kupta baadi ya matumiz japokuwa yuko home
2. Tunatofautiana maisha Kuna mwingne ametoka maisha flan ya hadhi ya juu kidogo amejengewa nyumba yake ndani ya uzio mmoja lakin chakula wanakula pamoja
Ko unaposema hvyo jalibu kuangalia na utofauti WA maisha Kwa Kila mmoja usiseme chanzo ni ww katika kufeli maisha
Mada inalenga idadi ya watu ndio chanzo cha umasikini katika familia, kwa kufanya tathmini, iwapo mtu mmoja anaweza kutumia kiasi fulani, je ukiwa nao idadi fulani, gharama itakuwaje?
 
Swali: [emoji117] mtoto anacha kuwa tegemezi kwa wazazi kwa asilimia kubwa akiwa ana miaka mingapi iwe wakike ama kiume .....hasa wakiume
Kutokana na changamoto mbali mbali, wapo wanaoanza kujitegemea mapema, na pia wapo wanaochelewa kabisa kujitegemea
 
Mada inalenga idadi ya watu ndio chanzo cha umasikini katika familia, kwa kufanya tathmini, iwapo mtu mmoja anaweza kutumia kiasi fulani, je ukiwa nao idadi fulani, gharama itakuwaje?
Ndy ndo maana nakwambia ebu jalbu kuangalia baadhi ya familia pia,, lakin katika watu walio na kipato Cha chini haipendezi kabisa lakin Hilo swala sababu mtu anaingiz 10000 Bado na ww unasogea Tena Bado inakuwa haiko swa
 
Mtu mmoja ndani ya familia awe ana anatumia 10,000 kwa siku?

Familia yenye uwezo huo mbona sio hata ya kuionea huruma kabisa.

Kama wenzangu wote hali ipo hivi basi mi nimetokea kwenye familia ya kimasikini sana.

Na kama hii hali ipo kweli kwa watu wengi basi zile kelele za kulia lia tozo ambazo kimsingi ni mia mia za juu zilizoongezwa ni unafiki wa kiwango chake.
Ata kule kijijini wangeamua kuthaminisha idadi ya watoto walionao, wangeona kuna sehemu wametumia nguvu kubwa kuliko angekuwa na watoto wachache.
 
Ninachojua watoto ama familia ni moja ya motivation ya kutafuta zaidi. Maana unajua usipotafuta familia itateseka na utaadhirika. Kama watoto ndio wanaotia umaskini mbona kuna watu wengi tu hawana watoto na siyo matajiri ama wanamtoto mmoja na hawajatoboa. Kwa familia za chini watoto ni sehemu ya ngivu kazi ya familia na ni uwekezaji pia. Japo siyo kila uwekezaji utakulipa
 
Katika familia, gharama hazipo kwenye kuzaa tu; bali gharama zipo kwenye malezi.

Na kwa mazingira ya sasa, unaweza kuta kijana ana miaka zaidi ya 30, lakini bado anaishi kwao, huku akiendelea kuwapa mzigo mzito wazazi wake.

Kwa nini nasema wewe ndio chanzo cha umasikini wa kwenu; ni kwa sababu gharama zilizotumia kukuza au kukulea wewe, ni gharama kubwa ambazo wazazi wako wangewekeza kwenye ujenzi wa viwanda, tungekuwa na bidhaa nyingi huko nje ya nchi na tungepata fedha za kigeni.

Mfano:-

Chukulia kwa siku unatumia 10,000/=

Mwaka una siku 365

Kukaa kwa wazazi mpaka kujitegemea, chukulia miaka 30

Fedha/nguvu zilizotumika kwa wazazi = 10,000 x siku 365 x miaka 30

=109, 500,000/=

Hii ina maana, mtu mmoja mpaka aje aondoke kwa wazazi wake, atakuwa ametumia kiasi kisichopungua Tsh. 109,500, 000/=

Kama mmezaliwa saba (7), ina maana wazazi wenu mmewabebesha mzigo wenye thamani ya Tsh. 766,500,000/=; kwa hiyo kama wanaishi kwenye mazingira mabovu, kaa ukijua, chanzo chao cha umasikini ni wewe.

Ndio maana matajiri hawazai watoto wengi, sio kwamba wana akili sana, bali wanaepuka gharama hizo nilizoziainisha hapo juu.

Kwa hiyo, usiwalaumu wazazi wako, kwa sababu chanzo chao cha umasikini ni wewe.

Karibuni kwa hoja.​

Si tulishakubaliana sisi hatulishi watu wazima!?

Hebu leta projects tugawane majukumu na pesa kaka
 
Ninachojua watoto ama familia ni moja ya motivation ya kutafuta zaidi. Maana unajua usipotafuta familia itateseka na utaadhirika. Kama watoto ndio wanaotia umaskini mbona kuna watu wengi tu hawana watoto na siyo matajiri ama wanamtoto mmoja na hawajatoboa. Kwa familia za chini watoto ni sehemu ya ngivu kazi ya familia na ni uwekezaji pia. Japo siyo kila uwekezaji utakulipa
Ebu mueleze aelewe kabisa usiongee sana inatosha kaishaelew
 
Mtu unatakiwa uondoke kwa wazazi ukiwa na umri gani wakuu? Mimi huu mwaka wa 42 Ila bado nipo kwa mama na baba nadunda afu kula kulala bure( KKB)
Wewe ndio unawadidimiza zaidi, bila wewe si ajabu wangekuwa wanamiliki visima vya mafuta
 
Back
Top Bottom