Wewe ndio chanzo cha umasikini katika familia yenu

Wewe ndio chanzo cha umasikini katika familia yenu

Katika familia, gharama hazipo kwenye kuzaa tu; bali gharama zipo kwenye malezi.

Na kwa mazingira ya sasa, unaweza kuta kijana ana miaka zaidi ya 30, lakini bado anaishi kwao, huku akiendelea kuwapa mzigo mzito wazazi wake.

Kwa nini nasema wewe ndio chanzo cha umasikini wa kwenu; ni kwa sababu gharama zilizotumia kukuza au kukulea wewe, ni gharama kubwa ambazo wazazi wako wangewekeza kwenye ujenzi wa viwanda, tungekuwa na bidhaa nyingi huko nje ya nchi na tungepata fedha za kigeni.

Mfano:-

Chukulia kwa siku unatumia 10,000/=

Mwaka una siku 365

Kukaa kwa wazazi mpaka kujitegemea, chukulia miaka 30

Fedha/nguvu zilizotumika kwa wazazi = 10,000 x siku 365 x miaka 30

=109, 500,000/=

Hii ina maana, mtu mmoja mpaka aje aondoke kwa wazazi wake, atakuwa ametumia kiasi kisichopungua Tsh. 109,500, 000/=

Kama mmezaliwa saba (7), ina maana wazazi wenu mmewabebesha mzigo wenye thamani ya Tsh. 766,500,000/=; kwa hiyo kama wanaishi kwenye mazingira mabovu, kaa ukijua, chanzo chao cha umasikini ni wewe.

Ndio maana matajiri hawazai watoto wengi, sio kwamba wana akili sana, bali wanaepuka gharama hizo nilizoziainisha hapo juu.

Kwa hiyo, usiwalaumu wazazi wako, kwa sababu chanzo chao cha umasikini ni wewe.

Karibuni kwa hoja.​
Nmecheka ila sijui nimecheka nini😅😅
 
Kama wewe umeweza kutoka kwenu mapema na kwenda kujitegemea ni jambo la kumshukuru mungu lakini kamwe usitumia hiyo fursa uliyoipata kama fimbo ya kuwatandikia ambao bado wapo makwao .

Watu kubaki kwao siyo kama wanapenda ila ni changamoto tu za kimaisha ndyo zimepekekea wawe hapo walipo , mfano katika umri huo wapo waliomaliza vyuo lakini mungu hajawafungulia milango ya wao kupata kazi , wapo waliojaribu kuanzisha biashara lkn kutokana na mazingira kutokuwa rafiki biashara zimeanguka hivyo sababu ni nyingi ..

Mwisho unapofanya kitu na kikafanikiwa siyo kwamba wewe ndyo umefanya vizuri kuliko wengine hapana bali ni baraka za mungu zimekuwa upande wako hivyo jitahidi kuombea na wengine waipite hyo changamoto na siyo kuwasengenya ...
Hichi ulichoandika mkuu siku zote kitazidi kuturudisha nyuma ama kutudumaza. Acha ukweli usemwe. Tukianza kubembelezana na kutafutiana lugha laini, kamwe hatutasonga na kuuaga umasikini. Siku zote ukweli mchungu na unauma vibaya mno, lakini hatuna namna lazima tuunywe. Unapowaona Israel wameendelea kiuchumi, kijeshi na kijamii ujue hawakuchekeana. Waliambiana ukweli, jasho liliwatoka na hatimae leo wamekuwa miongoni mwa mataifa super power. Vijana tuache kudeka. Ajira Kama hazipo kafyatue hata tofari uuze, nenda shambani kalime, kachime mkaa wa kupikia uuze, jifunze ufugaji ama nenda migodini kachimbe madini. Tanzania ni nchi iliyobarikiwa fursa lukuki. Tuache kutumia mda mwingi kwenye mambo yasiyo na tija, hakika ipo siku Tanzania tutakuwa wazalishaji wakubwa duniani wa mazao ya mifugo na shambani. Vijana watoke magetoni!!
 
Ninachojua watoto ama familia ni moja ya motivation ya kutafuta zaidi. Maana unajua usipotafuta familia itateseka na utaadhirika. Kama watoto ndio wanaotia umaskini mbona kuna watu wengi tu hawana watoto na siyo matajiri ama wanamtoto mmoja na hawajatoboa. Kwa familia za chini watoto ni sehemu ya ngivu kazi ya familia na ni uwekezaji pia. Japo siyo kila uwekezaji utakulipa
Nitajie matajiri watano kutoka kwenye 'top list' ya dunia (1-100) wenye watoto wengi
 
Hivi unajua elfu 10 miaka thelathini iliyopita ulikuwa unanunua kiwanja kabisa, hesabu zako hazijakaa vzur
Tafuta maana ya time value of money na maana ya inflation. 30,000 ya sasa ni sawa na 500 ya mwaka fulani. Ukiwa unapiga hesabu kwa sasa unataja thamani ya sasa hivi na ukipiga hesabu ya zamani unataja kiasi kile kisha subject ya thamani ya sasa.
 
Hichi ulichoandika mkuu siku zote kitazidi kuturudisha nyuma ama kutudumaza. Acha ukweli usemwe. Tukianza kubembelezana na kutafutiana lugha laini, kamwe hatutasonga na kuuaga umasikini. Siku zote ukweli mchungu na unauma vibaya mno, lakini hatuna namna lazima tuunywe. Unapowaona Israel wameendelea kiuchumi, kijeshi na kijamii ujue hawakuchekeana. Waliambiana ukweli, jasho liliwatoka na hatimae leo wamekuwa miongoni mwa mataifa super power. Vijana tuache kudeka. Ajira Kama hazipo kafyatue hata tofari uuze, nenda shambani kalime, kachime mkaa wa kupikia uuze, jifunze ufugaji ama nenda migodini kachimbe madini. Tanzania ni nchi iliyobarikiwa fursa lukuki. Tuache kutumia mda mwingi kwenye mambo yasiyo na tija, hakika ipo siku Tanzania tutakuwa wazalishaji wakubwa duniani wa mazao ya mifugo na shambani. Vijana watoke magetoni!!
Muhimu ni kukubali ukweli, na kuchukua hatua.
 
Back
Top Bottom