Wewe ndio chanzo cha umasikini katika familia yenu

Rapper Young thug aliwai kusema hivi,

Anatamani Mungu awa ondolee uwezo watu Maskini kupata watoto. Maana wana endeleza Umaskini kwa vizazi vyao.
FB_IMG_1689617390941.jpg

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
….Sio kila tajiri hapendi kuzaa,wengine mashart ya waganga wao…wengine jogoo hawiki + Presha kisukari n.k
 
Nitajie matajiri watano kutoka kwenye 'top list' ya dunia (1-100) wenye watoto wengi
Hahahaha mkuu unajitoa ufahamu kama ambavyo wizara ya afya inafanyaga hitimisho la kijinga kabisa la kushawishi masikini kuzaa watoto wachache kwa mpangilio bila kujua hili ni suala la kisaikologia na kijamii zaidi, kuliko linavyoonekana kwa nje.

Je, unafahamu kwanini watu ama wanayama wanatengeneza familia?
1. Tunatengeneza familia kama kiashiria cha kukua na kumiliki. Ndio maana hata mtu awe na mali kiasi gani kama hana familia anaonekana muhuni aliyefanikiwa.
2. Familia ni nguvu kazi hasa kwa watu masikini. Vitu vingi ambavyo ungeajiri watu wakusaidie ama wakufanyie basi utasaidiwa na wanafamilia.
3. Familia ni back up yako pale utakapokuwa umezeeka ama lolote kukutokea ambalo litasababisha usiwe na uwezo wa kutafuta.

Kwanini matajiri wanazaa watoto wachche
1. Matajiri wanaona mali zao ni kielelezo tosha cha kuonyesha mafanikio na umiliki wao. Wakati kwa masikini familia nzuri na bora ni kielelezo cha mafanikio na umiliki.

2. Kwa matajiri watoto siyo nguvu kazi bali pesa zao. Kwa masikini watoto ni nguvu kazi ya familia.

3. Kwao watoto siyo back up bali investments zao. Kwa masikini watoto ndio back up. Na wanajitahidi kuzaa wengi maana haujui yupi atafanikiwa na yupi hatofanikiwa.

Hivyo kisaikolojia sababu za tajiri kuwa na watoto hazina nguvu kama sababu alizonazo masikini. Hivyo matajiri wengi wanakuwa na watoto sababu ya kutafuta loyalty na successor wao wa kuendeleza legacy zao. Na si vinginevyo

N.B ndio maana hata vijijini siku hz watu wamepunguza kuzaa kwasababu sababu na uhitaji wa kuzaa watoto wengi umepungua. Wasomi wanahisi ni sababu ya Elimu la hasha ni sababu sana na uhitaji kupungua

Bila shaka nimekufafanulia kwa lugha rahisi sana
 
Kumbuka ukiwa na watoto saba tu, debe la mahindi linaisha mchana mmoja
 
Tatizo kubwa la Mtoa mada ni kutumia hisia kuliko facts.
Kama mtu anaweza kupiga hesabu ya matumizi kwa kila kichwa 10k, basi huyo siyo masikini.

Umasikini hausababishwi na wingi ama uchache wa watu bali fikra na mipango duni.

Narudia tena kwa masikini watoto wanawapa hamasa kubwa sana ya kutafuta. Na masikini akipoteza watoto hata Hamasa ya kutafuta inapungua vile vile.

N.B ukimsaidia masikini Kulea familia yake usitegemee kuwa atageuka kuwa tajiri kwa kuwa matumizi yamepungua
 
Mimi ningekuelewa ikiwa mtoto ndo mwenye maamuzi ya kuzaliwa na sio mzazi mwenye maamuzi ya kuzaa au kuzalisha.... Ila kwa kuwa ni maamuzi ya wazazi kukuleta duniani basi jukumu lipo kwao kuhakikisha maisha yako yakaa stable kwa nguvu zozote zile
 
Swali, ulaji wa watoto kumi ni sawa na ulaji wa watoto wawili?
 
Mimi ningekuelewa ikiwa mtoto ndo mwenye maamuzi ya kuzaliwa na sio mzazi mwenye maamuzi ya kuzaa au kuzalisha.... Ila kwa kuwa ni maamuzi ya wazazi kukuleta duniani basi jukumu lipo kwao kuhakikisha maisha yako yakaa stable kwa nguvu zozote zile
Kwa hiyo, unamaanisha lawama zote ziende kwa wazazi?
 
Katika familia, gharama hazipo kwenye kuzaa tu; bali gharama zipo kwenye malezi.

Na kwa mazingira ya sasa, unaweza kuta kijana ana miaka zaidi ya 30, lakini bado anaishi kwao, huku akiendelea kuwapa mzigo mzito wazazi wake.

Kwa nini nasema wewe ndio chanzo cha umasikini wa kwenu; ni kwa sababu gharama zilizotumia kukuza au kukulea wewe, ni gharama kubwa ambazo wazazi wako wangewekeza kwenye ujenzi wa viwanda, tungekuwa na bidhaa nyingi huko nje ya nchi na tungepata fedha za kigeni.

Mfano:-

Chukulia kwa siku unatumia 10,000/=

Mwaka una siku 365

Kukaa kwa wazazi mpaka kujitegemea, chukulia miaka 30

Fedha/nguvu zilizotumika kwa wazazi = 10,000 x siku 365 x miaka 30

=109, 500,000/=

Hii ina maana, mtu mmoja mpaka aje aondoke kwa wazazi wake, atakuwa ametumia kiasi kisichopungua Tsh. 109,500, 000/=

Kama mmezaliwa saba (7), ina maana wazazi wenu mmewabebesha mzigo wenye thamani ya Tsh. 766,500,000/=; kwa hiyo kama wanaishi kwenye mazingira mabovu, kaa ukijua, chanzo chao cha umasikini ni wewe.

Ndio maana matajiri hawazai watoto wengi, sio kwamba wana akili sana, bali wanaepuka gharama hizo nilizoziainisha hapo juu.

Kwa hiyo, usiwalaumu wazazi wako, kwa sababu chanzo chao cha umasikini ni wewe.

Karibuni kwa hoja.​
Wazazi wanawajibuwa kutunza watoto waliowazaa kwa starehe zao, watoto wasilaumiwe maana hamna mtoto anayejizaa.
 
Back
Top Bottom