Wewe ni mkubwa kuliko shilingi milioni Kumi

unavyoviongea vinawezekana kwenye jamii za KISTAARABU.Ila huku MAVUMBINI huu upako wako unaouhubiri hauna mashiko.

Jamii ya sasa inasifu wezi,mafisadi na waovu wote ndo wanaonekana wajanja katika jamii ya namna hiyo wewe kuwa wa tofauti ni kujitafutia shida.

Tupo zama za UBEPARI ULIOKOMAA,haya maubiri ya kufikirika ni kwa walioshiba tu,ila kama bado unajitafuta huwenda hiyo hela ndo njia yako ya kutokea.

MATAJIRI WOTE KUNA RAFU WAMECHEZA AU WANACHEZA MPAKA KUWA HAPO WALIPO.Sasa kama wewe unapenda umaskini endeleza mawazo ya akina PLATO na wanafunzi wake!!!!

Cha msingi ,kama hutaki kuwa disapointed hapa duniani VIBE NA BEAT linalochezwa wakati husika!!!
 
Binafsi narudisha
Kuna mtu aliwahi kudondosha pesa mbele ya duka langu na namba nadhani alikua anaenda kuiweka mpesa . Nilichukua Ile pesa ni zile namba nikasema nitampigia nimuulize kama Kuna mtu alikua na mihadi nae ya kutumiana pesa if yes aje hapo dukani nimpe hyo pesa nikashughulishwa kile kikaratasi sijui kilipotea vipi ila Ile pesa nilienda kumtolea sadaqa kwenye ujenzi wa msikiti hope atakutana na pesa yake siku ya kiyama in shaa allah
 
MATAJIRI WOTE KUNA RAFU WAMECHEZA AU WANACHEZA MPAKA KUWA HAPO WALIPO
Matajiri wengi siyo watu wazuri.
Ndiyo maana wapo tayari kuuza bidhaa zilizopita muda wake ili mradi waongeze utajiri wao.
Baadhi ya matajiri wanalipa stahiki ambazo hazikidhi haja za waajiliwa wao.
Katika jamii kama hiyo uaminifu wa watu unakuwa chini.
 
Mimi kama mimi kurudisha hela nimeokota siwezi,. Leo saa3 asubuhi kuna mtu kakosea kutuma Laki2 kwenye namba yangu ya Voda nimeihamishia Kwenye Halopesa nimetulia na mpango wa kuirudisha sina

Ubinadamu nilishafanyaga sana na haukunilipa wala kunifikisha popote. Wacha nijilipe tu maana nishalizwa sana
 
Siku haki ya huyo mtu ikirudi kwake naomba uyakumbuke haya unayosema ,tena kwako ingekuwa rahisi sana kurudisha kwakuwa unamjua mhusika

Hivi kpnz ulishawaza huenda hiyo hela kuna mgonjwa anahitaji kufanyiwa matibabu? Au kuna mjamzito ambaye anahitaji hiyo hela au labda kuna mpangaji ambaye huenda leo ndio deadline yake?
 
Ndio maana imeandikwa ni rahisi sana ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajir kuuona ufalme wa mungu,hakika kuna mambo mengi sana nje ya utajiri
 
Siku haki ya huyo mtu ikirudi kwake naomba uyakumbuke haya unayosema ,tena kwako ingekuwa rahisi sana kurudisha kwakuwa unamjua mhusika

Hivi kpnz ulishawaza huenda hiyo hela kuna mgonjwa anahitaji kufanyiwa matibabu? Au kuna mjamzito ambaye anahitaji hiyo hela au labda kuna mpangaji ambaye huenda leo ndio deadline yake?
Umesema vema, mimi naona hakuna kitu kigumu kama kila siku unatubia makosa yako lkn una dhambi moja ambayo unayo ipo constant kama hii ya kudhulumu haki ya mtu

Afu kingine watu wajue hakuna ukomo wa mema ila ufanye mara nyingi kdru nafasi zipotokea mpka uwe mtindo wa maisha
 
Mkuu mimi nimelizwa pesa nyingi sana sana sana, kuna nyingine mpaka saizi nadhani mzee wangu bado hajamaliza kulipa deni maana nilipigwa pesa nyingi halafu zilikua za kampuni ( naogopa tu kumention maana kuna watu hua wananifatilia sana ).

Hizo senario za kukosea kutuma hela na zilikua zinahitajika kwenye issue serious ndio kabisa sijawahi kurudishiwa

Hivi hapa kuna watu wawili niliwakopesha mmoja laki7 mwingine laki8 toka mwaka jana mpaka leo hawana mpango wa kunilipa hadi nawaza sijui niwaroge,.

So mimi saizi kwenye masuala ya kuwa na ubinadam kwenye hela nimejipa tu likizo, wacha nijilipe hivihivi mdogomdogo
 
NIlikua hivyo zamani, tena nadhani nilikua nina roho nzuri kukuzidi lakini wanadam wamenifundisha ukatili wacha tu nikachomwe moto kama ninachokifanya ni dhambi🙌
 
Umesema vema, mimi naona hakuna kitu kigumu kama kila siku unatubia makosa yako lkn una dhambi moja ambayo unayo ipo constant kama hii ya kudhulumu haki ya mtu

Afu kingine watu wajue hakuna ukomo wa mema ila ufanye mara nyingi kdru nafasi zipotokea mpka uwe mtindo wa maisha
Ni sahihi kabisa,na hakika ogopa dua ya mtu ambaye amedhulumiwa,hiyo inasemwa haina kinga kwa maana inakubaliwa moja kwa moja
 
Mkuu mimi nimelizwa pesa nyingi sana sana sana, kuna nyingine mpaka saizi nadhani mzee wangu bado hajamaliza kulipa deni maana nilipigwa pesa nyingi halafu zilikua za kampuni ( naogopa tu kumention maana kuna watu hua wananifatilia sana ).

Hizo senario za kukosea kutuma hela na zilikua zinahitajika kwenye issue serious ndio kabisa sijawahi kurudishiwa

Hivi hapa kuna watu wawili niliwakopesha mmoja laki7 mwingine laki8 toka mwaka jana mpaka leo hawana mpango wa kunilipa hadi nawaza sijui niwaroge,.

So mimi saizi kwenye masuala ya kuwa na ubinadam kwenye hela nimejipa tu likizo, wacha nijilipe hivihivi mdogomdogo
Kwanza pole sana kwa mitihani ambayo imekupata,ndio binadamu tulivyo tukiwa na shida tunakuja mikono nyuma ila tukikidhi haja zetu huwa imeisha hiyo

Nikwambie kitu Leejay49, najua umeumizwa na sasa hivi moyo wako umeingia ganzi lakini usiwahukumu wengine kwa makosa ya wengine

Usichoke kuomba walio kudhulumu warudishe haki yako,lkn liwe somo kwako uwe makini kuwakopesha watu ambao hawastahili
 
Mimi kama mimi kurudisha hela nimeokota siwezi,. Leo saa3 asubuhi kuna mtu kakosea kutuma Laki2 kwenye namba yangu ya Voda nimeihamishia Kwenye Halopesa nimetulia na mpango wa kuirudisha sina

Ubinadamu nilishafanyaga sana na haukunilipa wala kunifikisha popote. Wacha nijilipe tu maana nishalizwa sana
Yeah maisha yanafunza sana
 
Kwanza pole sana kwa mitihani ambayo imekupata,ndio binadamu tulivyo tukiwa na shida tunakuja mikono nyuma ila tukikidhi haja zetu huwa imeisha hiyo

Nikwambie kitu Leejay49, najua umeumizwa na sasa hivi moyo wako umeingia ganzi lakini usiwahuku wengine kwa makosa ya wengine

Usichoke kuomba walio kudhulumu warudishe haki yako,lkn liwe somo kwako uwe makini kuwakopesha watu ambao hawastahili
Uko sahihi sana mkuu, lakini nadhani huu ushauri kuna mtu atasoma na utamfaa ila mimi sio mlengwa hapa nimeshajikataa.

Kwenye hili kama ni dhambi nimekubali kwenda kuitumikia huko akhera, nimelizwa mnooo wacha tu niendelee kuwa hivihivi nachoomba Mungu ni kwamba waendelee kukosea na wengine na wengine
 
Sawa bwana mimi ni nani nipinge maamuzi yako😂😂
 
Back
Top Bottom