Wewe ni mkubwa kuliko shilingi milioni Kumi

Wewe ni mkubwa kuliko shilingi milioni Kumi

Matajiri wengi siyo watu wazuri.
Ndiyo maana wapo tayari kuuza bidhaa zilizopita muda wake ili mradi waongeze utajiri wao.
Baadhi ya matajiri wanalipa stahiki ambazo hazikidhi haja za waajiliwa wao.
Katika jamii kama hiyo uaminifu wa watu unakuwa chini.
Mkuu endelea kubaki kuwa fukara hili ukutane na pepo
 
Yaani niokote pesa nikawapeleke polisi, POLISI hawa hawa ninaowajua mimi, ndugu yangu huwajui polisi wetu vizuri.
Ikiwa imetangazwa basi ninaweza rejesha.

Lakini pia inahitaji imani kubwa haswaa, una dhiki zako, mwanao anahitaji laki 7 hapo muhimbili, nyumba yako inahitaji milioni 2 kupaua upya, mabati ya sasa yanavuja.
Inahitaji imani ya level ya juu sana.
10M imetangazwa kaidondosha nani? Mo Dewji?

Mungu anajua anazo nyingine
 
Yaani niokote pesa nikawapeleke polisi, POLISI hawa hawa ninaowajua mimi, ndugu yangu huwajui polisi wetu vizuri.
Ikiwa imetangazwa basi ninaweza rejesha.

Lakini pia inahitaji imani kubwa haswaa, una dhiki zako, mwanao anahitaji laki 7 hapo muhimbili, nyumba yako inahitaji milioni 2 kupaua upya, mabati ya sasa yanavuja.
Inahitaji imani ya level ya juu sana.

Kwa shida hizo haihitaji imani tena, Ni lazima uwe nabii au mtume ndo utashinda hapo!
 
Mimi kama mimi kurudisha hela nimeokota siwezi,. Leo saa3 asubuhi kuna mtu kakosea kutuma Laki2 kwenye namba yangu ya Voda nimeihamishia Kwenye Halopesa nimetulia na mpango wa kuirudisha sina

Ubinadamu nilishafanyaga sana na haukunilipa wala kunifikisha popote. Wacha nijilipe tu maana nishalizwa sana
Umekuwa mkweli
 
Nikiokota pesa ya kuokota namtafuta mwenye nayo nampatia. Pesa ya kuokota sio yako wala haiwezi kukuongezea chochote kwenye akili yako.
Nitafanya kila jitihada mpaka nimpate mwenye nayo mimi mwenyewe.
Unasema hivyo Kwa sababu wewe ni Meneja Wa Makampuni, ngoja ufukuzwe kwenye hiyo nafasi uone kama utarudisha hele uliyookota hata kama ni Tsh 200.

Monetary doctor mwenyewe huwa harudishi wewe ni nani?
 
View attachment 3186821

Hivi leo hii ukisikia mtu kaokota shilingi milioni kumi [10,000,000] halafu kaipeleka polisi au karudisha kwa mwenyewe,je utamwonaje? Bilashaka wengi wetu tutamwona ni mpumbavu

Ukweli ni kwamba mtu huyu ni mkubwa kuliko hiyo hela ambayo wengi wetu tunababaika nayo,yupo imara kiroho,kihisia na ana uwezo mkubwa wa kudhibiti tamaa yake,akisema hapana ni hapana na akisema ndio ni ndio,hakuna tena migongano au mvutano wa fikra zake

Hata sisi ni wakubwa pia ni vile tu bado hatuja tumia uwezo wetu wa ndani kabisa,sisi ni wakubwa kuliko dharau tunazo fanyiwa na watu mbali mbali katika maisha yetu ya kila siku,ukiwa mkubwa kuliko dharau unazofanyiwa,utazipuuza na hazita kuumiza kichwa na kushindwa kufanya mambo yako binafsi

Ukiwa mkubwa hautashindwa kusamehe makosa uliyofanyiwa na binadamu wenzako,kwakuwa unajua wewe ni mkubwa kuliko hayo makosa uliyofanyiwa hivyo unaweza kuwasamehe wale wote walio kukosea,lau ukiamini wewe ni mdogo kuliko hayo makosa hakika hautaweza kuwasamehe watu na utaishi kwa vinyongo kila siku

Tambua kwamba wewe ni mkubwa kuliko hayo mapenzi ambayo kila siku yanakuumiza kichwa na hisia zako pia,unaweza kuyaweka pembeni na kusonga mbele,kwakuwa unajua wewe ni mkubwa kuweza kupata mwenza mzuri zaidi atakayeendana na vigezo vyako

Kwa jambo lolote na hali yoyote utakayo kutana nayo maishani tambua wewe ni mkubwa kiroho,kihisia,kimtazamo na una uwezo wa kuhimili hali hiyo kwakuwa uwezo huo unao

Ni hayo tu!
Mtu kama bakil/resa, mo dewji wadondoshe alafu niwarudishie wakati nabeba viroba asubuhi mpaka jioni kwa buku nne
 
Nitarudisha pesa ya kuokota kama tu;

  1. nimemuona alieidondosha.
  2. kumetangazwa kupotea hiyo pesa na muhusika.
Sitokuja kufanya kosa la kuokota pesa na kuipeleka Polisi. Polisi ni wezi na majambazi. Kupitia hiyo pesa wanaweza hata kunidhuru ili wajimilikishe.
Yaani uko sahihi mno. Asante.
 
Back
Top Bottom