Wewe unaweza kurudisha kwa muhusika

Wewe unaweza kurudisha kwa muhusika

elf 70 mkuu inakuondolea utu namna hiyo, haya tufanye umeichukua umefanyia nini cha maana? usikute kuna mgonjwa alikuwa anatakiwa apone kwa ajili ya hiyo hela, kuna mwanafunzi alitakiwa afanye mtihani wa chuo maana hiyo ndio ada ya kujazia
Nimeirudisha mkuu mda san nikuwa nawachora tu
 
Kuna mmoja alikosea 210000, kuna mwenzangu nikamuonyesha akasema tukatoe nikakataa, nikamsubiria apige maana alitumia kwa NMB, kapiga kesho yake..nikaanza kucheka ikabidi naye acheke alinambia " bro utaweza nirudishia kweli 😂" nikamjibu ndio, aliniambia toa 30000 chukua, mpaka leo marafiki 🤣🤣
 
Mfano tu mtu kakosea katuma pesa kwako kimakosa 70k elfu anaomba uirudishe na wewe ulipo iona ukaamua kuitoa hapo hapo maana ulikuwa karibu na wakala af anapiga simu sana una amua kublock namba kuna shida yoyote?
inategemeana na namna muhusika atakavyo nijia. kama kaja kwa ukali sirudishi vinginevy saw
 
Kuna mmoja alikosea 210000, kuna mwenzangu nikamuonyesha akasema tukatoe nikakataa, nikamsubiria apige maana alitumia kwa NMB, kapiga kesho yake..nikaanza kucheka ikabidi naye acheke alinambia " bro utaweza nirudishia kweli 😂" nikamjibu ndio, aliniambia toa 30000 chukua, mpaka leo marafiki 🤣🤣
Mimi nimerudisha kabla sijaleta uzi hapa ila nilitaka kuona gubu la waja wa jf na nimeliona kuna wengine wananipa laana ila wangekuwa wao wasingerudisga na wangezima simu
 
Ndo inavyokuwa mara zote...jamaa yangu alilaumu sanaa.
Unajua mtu akikosea anamwogopa sana aliyepokea asiye na matusi maana anajua huu mzigo haurudiii ...kuliko mmwaga matusi 🤣🤣
 
Kuna mwaka maisha yalinipiga mno aisee chanzo nilinunua mbaazi kwa shiling 1200 kwa kilo halafu wanunuzi ambao ni wahindi wakasigana na serikali kwahiyo hawakununua na ukizingatia nilinunua mzigo kwa pesa yangu yote...hapo ndipo maisha yakaànza kuwa magumu sana ....kuna siku nilikuwa kijiji fulani ghafla ikaingia pesa laki 7 kwenye airtelmoney kabla sijawaza vizuri nani katuma nikapigiwa Simu na mama mmoja kuwa amekosea ,,nikamwambia mama subiri nakurudishia nikakodi bodaboda mpaka kijiji cha jirani kuliko na wakala nikainyofoa ile pesa
 
Wejama katili
 
Mfano tu mtu kakosea katuma pesa kwako kimakosa 70k elfu anaomba uirudishe na wewe ulipo iona ukaamua kuitoa hapo hapo maana ulikuwa karibu na wakala af anapiga simu sana una amua kublock namba kuna shida yoyote?
Me nishawai pata 500k dakika1 nikachoa 200k kwa wakala chap, hapo ndo nikanza tafakari hii amount imetoka wapi?? Dakika ya tatu nikaona acc yangu tigopesa imefungiwa, nikajua kishaumana huko.
Kama dakika 5 naona namba ngeni inanipigia, nikapokea jamaa akasema "nimekosea muamala afu umepunguza naomba urudishe hela".
Coz nlikua na wana hapo wananimaind kwann sikutoa yote 500k, nikawaambia ngoja nikamrudishie sio poa. Wakati naenda kurudisha Kama dakika 5 mbele nikapokea picha zangu kwenye whatsapp na biti la kufa mtu kwamba kama najipenda nikatume hiyo amount upesi sana, otherwise kesho sifiki. Biti likawa jingi kwamba ameriport kwa watu cybercrime na anajua nilipo.

Nikabadilisha uamuzi, nikamwambia kama mnajua nilipo sawa njoo na hao watu cyber. Maana kelele zilikua mingi mixer sms kama mkeka...
Tukaenda zetu kula rite, tokea 2021 hadi leo hawajaja.😆

Hela ukikosea omba kistaarabu, muungwana anakurudiahia tuh.
 
Mimi nilituma laki saba na hamsini juzi kupitia Airtel money. Wakala akakosea namba zikaenda kwa mwenyekiti wa mtaa wa CCM huko Tabora. Ilikuwa saa sita na nusu. Saa kumi nampigia niliyemtumia pesa anasema hajaipata! Kwenda kwa wakala akacheki na mtu wa Tabora akakuta ameshaitoa hela yote. Na baada ya hapo akablock simu!!!
Mimi hapa niko njia panda sijui Airtel watanisaidiaje!
 
Mfano tu mtu kakosea katuma pesa kwako kimakosa 70k elfu anaomba uirudishe na wewe ulipo iona ukaamua kuitoa hapo hapo maana ulikuwa karibu na wakala af anapiga simu sana una amua kublock namba kuna shida yoyote?
Kuna jamaa juzi alikuwa anatuhafithia et alipokea milioni moja mara simu ikaita kapigiwa na aliekosea anadai hiyo hela ili kuwa inatumwa kwa ajili ya matibabu jamaa moyo ukalainika akairudisha walivyoipata wakampoza laki tat, ila nahisi niliongo ilikuwa ni chai maana jamaa anasifa ya uongo
 
Mimi nilituma laki saba na hamsini juzi kupitia Airtel money. Wakala akakosea namba zikaenda kwa mwenyekiti wa mtaa wa CCM huko Tabora. Ilikuwa saa sita na nusu. Saa kumi nampigia niliyemtumia pesa anasema hajaipata! Kwenda kwa wakala akacheki na mtu wa Tabora akakuta ameshaitoa hela yote. Na baada ya hapo akablock simu!!!
Mimi hapa niko njia panda sijui Airtel watanisaidiaje!
Duuuh
 
Mfano tu mtu kakosea katuma pesa kwako kimakosa 70k elfu anaomba uirudishe na wewe ulipo iona ukaamua kuitoa hapo hapo maana ulikuwa karibu na wakala af anapiga simu sana una amua kublock namba kuna shida yoyote?
Hiyo hela ndogo rudisha, kwanza mimi hata sitashughulika nayo nitasubiri mwenyewe apige.
Kuna mzee aliwahi kunirudishia,. Baadae nilimsaidia sana kwa muda mrefu maana nilimfanya kama baba yangu.
 
Kubwa isirudishwe?
 
Mwambie ali verse mwenyewe,wewe usitume au awasiliane na mtandao husika wafanye hio process.

Ila wengi humu wanasema rudisha,siwaamini sana kama wao wangefanya hivo.
Shida laini haitakua na amani hata vocha utashindwa kuweka
 
Kwa mtu mwenye mtaji wa elfu tano anatembeza mboga mboga hiyo ni hela kubwa, ila kwa zuchu ni ndogo.
Sasa hela kubwa ipi sijui.
Kubwa zaidi ya elfu 70? Kama mada inavyosema na wewe ulivyojibu.
 
Back
Top Bottom