Wewe unaweza kurudisha kwa muhusika

Wewe unaweza kurudisha kwa muhusika

Uwizi + dhulmaaa hiyooo
Sema hiyo ndiyo jadi yetu
Wabongo

Ova
 
Mfano tu mtu kakosea katuma pesa kwako kimakosa 70k elfu anaomba uirudishe na wewe ulipo iona ukaamua kuitoa hapo hapo maana ulikuwa karibu na wakala af anapiga simu sana una amua kublock namba kuna shida yoyote?
Mimi ukifanya huo ujinga, utanitajirisha nakuambia. Labda ukimbie nchi.
 
Hivi nikiweka picha yake humu nitakuwa nimefanya kosa? 750,000 sio hela ndogo jamani! Maana tayari tumefanikiwa kupata namba yake ya NIDA
 
Niliwahi fanyiwa wema,nilidondosha wallet ikiwa na pesa nyingi tu(kwenye daldala) na id's na dada mmoja alieiokota akafanya namna mpaka akanipata, aisee sikuamini
Nikamkatia kidogo katika ile pesa nikaondoka zangu
Rudisha tu hiyo pesa
 
Nimeipenda hii ikiwa sio kauli za nyuma ya keyboard basi jf imejaa watu wema.

Karibia wote mnamwambia mleta uzi airudishe hapo akifanya kinyume ni juu yake sasa.
 
Inategemea imeingia kwenye simu yako ukiwa katika hali gani 😅
 
February 2022, nilikuwa na Safari toka Dar to Arusha. Niliunga magari, nilipofika Handeni somewhere "Kabuku" nilipita kwa wakala kuweka 150,000 kwa tigopesa ili nilifanye malipo flani kisha niendelee na safari.

Nilitoka pale dukani na kuelekea stendi ili niendelee na safari, kabla ya kuendelea nikalipia bili yangu, ajabu nikaona Salio jipya Tsh 1,350,000/=

Kuangalia vizuri nikaona kumbe wakala aliweka 1,500,000 badala ya 150,000

Nikarudi ofisini kwake kumbe alikuwa bado hajashtukia hilo. Nikatoa pesa yake yote iliyozidi kisha akanipa Tsh 50,000 kama ahsante. Alinishukuru sana, akachukua na namba yangu tunawasiliana hadi leo

Siku mbili baada ya kufika Arusha, nikiwa nimepanda boda boda mitaa ya Njiro jirani na (Njiro SDA Church) nilikua naelekea 'France Corner' nilidondosha wallet iliyokuwa na Zaidi ya Tsh 600,000/= bila kujua nimedondosha

Tulipofika nane nane, kuna boda ilikua ikitufuata, akatupigia honi kuashiria tusimame. Alikuwa ni boda anaishi mtaa ninaoishi na tulifahamiana katika zile siku mbili. Aliniletea wallet yangu ikiwa na pesa na kila kilichokuwemo. Nilimpatia posho kiasi tukaendelea na safari

Hili tukio lilinistaajabisha sana na nilipata somo kubwa, kumbuka ni siku mbili tangu nimetoka kumrudishia muamala jamaa
 
Back
Top Bottom