February 2022, nilikuwa na Safari toka Dar to Arusha. Niliunga magari, nilipofika Handeni somewhere "Kabuku" nilipita kwa wakala kuweka 150,000 kwa tigopesa ili nilifanye malipo flani kisha niendelee na safari.
Nilitoka pale dukani na kuelekea stendi ili niendelee na safari, kabla ya kuendelea nikalipia bili yangu, ajabu nikaona Salio jipya Tsh 1,350,000/=
Kuangalia vizuri nikaona kumbe wakala aliweka 1,500,000 badala ya 150,000
Nikarudi ofisini kwake kumbe alikuwa bado hajashtukia hilo. Nikatoa pesa yake yote iliyozidi kisha akanipa Tsh 50,000 kama ahsante. Alinishukuru sana, akachukua na namba yangu tunawasiliana hadi leo
Siku mbili baada ya kufika Arusha, nikiwa nimepanda boda boda mitaa ya Njiro jirani na (Njiro SDA Church) nilikua naelekea 'France Corner' nilidondosha wallet iliyokuwa na Zaidi ya Tsh 600,000/= bila kujua nimedondosha
Tulipofika nane nane, kuna boda ilikua ikitufuata, akatupigia honi kuashiria tusimame. Alikuwa ni boda anaishi mtaa ninaoishi na tulifahamiana katika zile siku mbili. Aliniletea wallet yangu ikiwa na pesa na kila kilichokuwemo. Nilimpatia posho kiasi tukaendelea na safari
Hili tukio lilinistaajabisha sana na nilipata somo kubwa, kumbuka ni siku mbili tangu nimetoka kumrudishia muamala jamaa