What about R&D?..The Case of Foreign Aid Influx & 'A Japanese Expert' Invite

What about R&D?..The Case of Foreign Aid Influx & 'A Japanese Expert' Invite

Dar Es Salaam,
Mkuu unaposema:- nakumbuka Mahathir Muhammad alifanya hivyo hivyo na leo tunaiona Malaysia kwa viwanda...
Hivyo hivyo una maana gani kabla sijaweka hoja yangu.

Unajua mkuu unapozungumzia vitu haswa kule tulikotoka na kuchukulia mfano kwa kuitumia Japan nadhani utakuwa unatupotosha kabisa. Wachina walikuja funga mitambo na kuifanyia Ukarabati ndani ya contract ya kiserikali jambo ambalo ni la kawaida kabisa. Kuzorota kwa uchumi wetu hadi viwanda vikafa imetokana na mrengo wa kisiasa wa Mwalimu ambaye alitaka kwanza kuhakikisha tunaweza kuzalisha ndani bila kushindana na masoko toka nje ama kujali quality na technologia mpya maadam vitu hivyo vinapatikana kwa mahitaji ya wananchi ndani. Pili inajuulikana vizuri kuwa baadhi ya mazao yetu yalikosa soko baada ya kuanguka kwa bei za mazao hayo ktk soko la dunia, mfano sukari iliweza tengenezwa kirahisi na cheap kutoka mimea mingine nje ya sukari. Katani vile vile ilipata mrithi wa nyuzi za plastic zinazotokana na recycle ya plastic materials ambazo nchi hizo za Ulaya ilikuwa ikizitupa. Ukitazama mazao mengine ya chakula hawa jamaa waliweza vumbua mbegu zinazoweza kua na kuzalisha ktk mazingira yao na within muda mfupi sana wa jua bila kutegemea tena mazao yanayotoka Afrika mwaka hadi mwaka.
Sasa kama wao wameweza tafuta ufumbuzi wa mahitaji yao leo hii kweli tunabaki kulalamika kuwa sisi tulichemsha hali sisi hatukuangalia nini kinafanyika nje, hali hawa jamaa maabara zao - R&D siku zote ni ktk kutafuta ufumbuzi wa mahitaji yaani soko.
Hivyo maendeleo ya nchi za Ulaya yaliweza tazama mahitaji yao kwanza na kutafuta solution (invention) within their own necessity... Hiyo ilikuwa miaka hiyo ya Ujamaa wakati wa cold war na Uchumi unaotegemea siasa za mfungamano.

Sasa tulitazame swala hili kwa wakati huu maanake tusipokuwa tunatazama wakati, mkuu tutakuwa tunazidi kujisindika ktk ujuha zaidi. Viwanda vyetu vilikufa kutokana na kutoweza kushindana hasa baada ya mali toka nje ziliporuhusiwa kuingia nchini. Ni kweli wasomi wetu wengi walikuwa bado wakitumia technologia ya miaka ya 70 na pia monopoly power ambayo mashirika hayo yalikuwa yamejijengea kutokana na kuwa ya serikali hayana mshindani wala ubishi ktk uendeshaji wake. Palikuwa hakuna viatu isipokuwa vya Bora, hata dawa ya mswaki nakumbuka ilikuwa Tara mbaya kishenzi, na vingine vingi ambavyo vilikuwa bado ktk utaalam wa soko ambapo quality ilikuwa muhimu zaidi ya just demand. Na viwanda vyote vilivyokuwa ktk hali nzuri ama ya kati kiushindani ndivyo vimeweza kuendelea kufanya vizuri hadi leo na nakuhakikishia kuwa sii kweli viwanda kama General Tyre, Tanzania Breweries, Sigara, Africafe na kadhalika havikuwa vimechoka. Na pili hatuwezi kusema waliosababisha kuchoka kwa baadhi ya viwanda vyetu ni Wachina ama huduma zilizokuwa zikitolewa na Wachina isipokuwa ni sisi wenyewe pamoja na siasa yetu ya Kijamaa ambayo haikutazama wakati mbele yetu kiuchumi.

Kwa hiyo Mkuu hata kama huyo Mjapan akija na kutuongoza sijui viwanda gani vinahitajika sidhani kama ataweza pia kutuongoza jinsi ya kuviendesha maanake tulikopotea mwanzoni viwanda hivyo vilikuwa chini ya mikono yetu sio Mchina, Tazara hiyo hapo inadunda hadi leo..Je, huoni kama swala hapa sio utaalam wa kubuni viwanda na jinsi ya kuviendesha isipokuwa ni uwezo wa kutambua soko la nje na ndani wakati huo huo ukitumia gharama ndogo zaidi. Japna was a an economic Giant miaka ya 60 ya 70 (second largest economy in the world) lakini leo hii wao wenyewe wanakiri kuwa China na India zitawapita wala sii Muda mrefu. Hata Russia ambao walikuwa Wajamaa kuliko sisi leo hii wanashika nafasi ya 9 duniani. Hivyo tuwe wakweli kuangalia wakati na kitu gani kinaendelea ktk dunia hii ya Utandawazi...
If China na Russia waliokuwa wajamaa tena Ma komunist wameweza kuja juu kuliko hata nchi zilizokuwa za Kibepari imekuwaje sisi tuwe kila mwaka tunapiga hatua kurudi nyuma?...Wapi tunafanya makosa na haya makosa yanaweza rekebishwa vipi.

Now, kama huyu mtaalam anakuja tuambia ni wapi tunafanya makosa labda naweza ungana na wazo hili lakini bado tutabaki na mfujo wa pakacha kuwa tatizo la Mdanganyika sio kuanzisha miradi inayoweza kuzalisha bali ni uendeshaji wake kutokana na siasa kuingilia uzalishaji, mazingira na pengine hata tamaa za viongozi nje ya necessity.

Japan pamoja na mafanikio yao yote waliyopata, leo hii wamekwama inapofikia gharama za utengenezaji. Sasa isije huyu Mtaalam akaifananisha Japan na Tanzania ama kujaribu kuleta mabadiliko ya Kiuchumi Japan akayajaribu Tanzania kwani hatufanani hata kwa chembe. Japan ni matajiri na wenye techonologia ya hali ya juu kabla hata ya vita kuu ya dunia. As a fact sidhani kama huyu mama anaweza kutuambia mafanikio ya Japan ktk viwanda ambayo yanaweza kuigwa Tanzania maanake hatuna uwezo huo kabisa..

Labda kwa kuwapeni picha halisi nadhani bora tutazame wenyewe Wajapan wanasema nini ktk uchumi wao kisha tuyapime mahitaji yetu na jinsi ya sisi wenyewe kujaribu kutafuta mbinu mpya za kibiashara kulingana na soko huria. Nje ya hapo tutakuwa tunajidanganya kama kawaida yetu...
Someni report hii toka ministry of Economic, Trade and Industry of Japan (METI) labda tunaweza omba ama ku- join program zao za - ONE VILLAGE ONE PRODUCT!

http://www.meti.go.jp/english/report/downloadfiles/NewEconomicGrowthStrategy(outline).pdf

Watusaidie kuzalisha kile kinachotakiwa kwao (Japan) ama nchi za Asia toka Africa.
 
Mkandara hapa tunaongelea ushauri, ushauri, ushauri.

Kuna ubaya gani wa kutaka ushauri? hebu jamani tufunguwe mawazo kidogo na tusibishane tu kwa ajili ya kubishana.
 
habari Leo

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Masoko, Mary Nagu, amesema Tanzania itamtumia mtaalamu kutoka Japan kuhakikisha inaondokana na kutegemea jembe la mkono badala yake inakuwa nchi ya maendeleo ya viwanda.

Nagu aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuwa mtaalamu huyo kazi yake kubwa ni kuishauri serikali namna ya kuweza kuondokana na jembe la mkono badala yake nchi kuwa ya viwanda kama ilivyo kwa Japan.

Mtaalamu huyo, Yoshiyasu Mizuno ametokana na ziara aliyofanya Rais Jakaya Kikwete mwaka jana nchini Japan ambako pamoja na mambo mengine, aliiomba nchi hiyo iisaidie Tanzania ili nayo iweze kupiga hatua kubwa katika maendeleo ya viwanda.

Japan imetoa mtaalamu wa mambo ya viwanda ambaye atafanya kazi na Serikali ya Tanzania asaidie katika kutoa ushauri wa namna ambavyo taifa hili masikini linaweza kupiga hatua ya maendeleo kwenye sekta ya viwanda. Nagu alisema kwa kuanzia, mtaalamu huyo atajikita zaidi katika kushughulika na viwanda vya kusindika mazao ya kilimo kuinua sekta hiyo.

HAPO MIMI NAONA MNA KITU, KWANI KIPAUMBELE KILICHOWEKWA NI VIWANDA, NA MTALAAM HUYO NI WA VIWANDA, SIYO KILIMO. SASA IWEJE WAZIRI ASEME KWAMBA TUTAONDOKANA NA JEMBE LA MKONO? KWANI JEMBE LA MKONO WANALOTUMIA WAKULIMA KULE VIJIJINI LITAONDOLEWA KWA VINDA KWELI?

NI KWELI TUNAHITAJI MAENDELEO YA VIWANDA, LAKINI JE? NDIYO KIPAUMBELE CHETU? HAKUNA HATA HAJA YA KUSEMA SUA HAKUNA AGRO-MECHANICS IPO! ILA WANANCHI BADO HAWAJAWEZESHWA KUTUMIA HIZO NYENZO ZA NGO'MBE, TRACTORS, COMBINE HARVESTERS NK. SASA LEO TUAMBIWE HUYU MTALAAM WA VIWANDA ATASHAURI MPAKA TUONDOKANE NA JEMBE LA MKONO? THIS IS REDICOLOUS.

MTALAAM HUYO ANASEMA, USHAURI WAKE UNAJIKITA KWENYE VIWANDA VYA KUSINDIKA. LENGO LAKE NI KUISHAURI SERIKALI IALIKE WAWEKEZEJI!! DAMN IT? HII NDIYO KAZI YA MSHAURI WA KIMATAIFA ILI KUTUONDOA NA JEMBE LA MKONO?

TUKUMBUKE ILE METHALI YA MTEGEMEA CHA NDUGUYE HUFA MASIKINI, MASUALA YA MAENDELEO SI MAMBO YA KISIASA. HILO NAONA LINAHARUFU YA KISIASA.
 
Sioni ubaya wa huyu mtaalamu kuja kwake Tanzania, ujio wake ulitokana na na maombi ya RAISI alipokwenda kutembea kule Japan, nafikiri hapa tatizo lilikuwa ni kipaumbele cha raisi katika kupitisha lile bakuli.

Mtaalamu ameshakuja, what next? Ni vizuri kutumia nafasi hiyo ili watu wetu wajifunze kutoka kwake.

Wajapan wenyewe walijifunza kutoka USA na kufikia hapo walipo.

Naamimi huyu kaka/dada ataboreka na sisi, kwa sababu sisi si wachapa kazi kama walivyo wao (committed), ni wavivu wa kufikiri na huwa tunapenda ready made solutions. Hawa jamaa ukifanya nao kazi unaweza kulia, kukiwa na 'mission to be accomplished'- masaa ya kazi kwao ni 24hrs. Je sisi tutaweza hiyo kasi?

Jamani mliopo katika nafasi ya kuwa na huyo jamaa hakikisheni mnajifunza kutoka kwake,wanapronciples nzuri sana hasa kwa upande wa quality improvement.
 
Dar Es Salaam,
Naelewa fika mkuu kuwa tunachoongelea hapa ni Ushauri!..
Ni ushauri huo huo umetuletea habari za viwanda vyetu vilivyokufa!..sikuona connection mkuu.
Sasa kama ingelikuwa ni jinsi ya kuvifufua labda ningeweza kuelewa mfano wako ulilenga kitu gani lakini tunapozungumzia kuondokana na jembe la mkono ktk swala la viwanda mkuu wangu sioni solution ya ushauri kutoka nje!. Ni ushauri huo huo toka nje uliotuingiza ktk madeal yote mabaya iwe IPTL, ama mikataba ya madini kina Sinclair wanazivuta hadi kesho.
Tatizo lipo ktk viongozi wetu kutotambua umuhimu wa mahitaji yetu sisi wenyewe. I mean hivi kweli utumiaji wa trector unahitaji mtaalam kutoka Japan kutuambia!, ama viwanda hivyo vitakuwa vinafanya nini kiasi kwamba yule mkulima wa jembe la mkono hawezi kuhitajika tena na hakuna mtaalam nchini aliyefikiria hivyo.
Trust me mkuu wangu mimi naona kama ni vyandarua vingine vinakuja badala ya sisi kuomba dawa za kuua mbu ama kufukia mashimo ya maji yaliyosimama, which is way cheap and the ONLY solution ya kuondokana na maleria.
Ama kweli awamu hii tumepata viongozi vilaza mkuu wangu, hizi safari zao kila siku huzua maajabu mara tutaahidiwa mvua za sayansi, huku nyuma wamechukua Richmond na tungekwisha maanake mvua zisinge kuwepo na Richmond deal lingeendelea kwa miaka 10.
 
Nimefikia conclusion kuwa Tanzania na watanzania wote labda tunahitaji kuchapwa viboko ili tufikirie mambo ya maana kwanza na kuacha mengine.

Huyu mtaalam wa Japan ni bogus na to me ni usanii tu wa serikali.

Kuna ile report imetoka leo ambayo kina Tindu Lissu wameitoa kuhusu madini (Gold). Mbona wataalam wameshatoa opinion na ni common sense lakini serikali na sisi humu ndani discussion zetu wala hazijali ukweli uliopo kwenye losses za over 1 billion USD ambazo zingeweza kabisa kusaidia kilimo.

Also huyo Mary Nagu anaongea vitu ambavyo hata hajui, kilimo cha mkono solution ni serikali kuprovide makasio na matractor ili yakopeshwe kwa wakulima. oh sorry kipaumbele ni maVX kwa viongozi.
 
kule ilikotakiwa kuanzia..

Maendeleo ya watanzania na Africa kwa ujumla yatatoka kwa watanzania wenyewe.

Unajua bado Tanzania tunakasumba ya kutokuwa na imani na wataalamu wetu, Tunataasisi nyingi sana hapa Tanzania, vyuo vikuu na taasisi za Utafiti kibao ila kwa kasumba yetu tuliyo nayo ya kuamini kitu kizuri kinatoka nnje ndio haya sasa. Mkataba wake ukiisha akiondoka anaondoka na utaalamu wake.

Huku ni kuwadhalilisha wataalamu wetu wa nchini. Unajua Japan ndio wanatoa Technical Asistance na Financial Asistance. Haimaanishi kuwa wataalamu kutoka Japan ndio compitent na watawaletea maendeleo Japan. Ukitaka kujua Japan iliendelea je soma historia yake. Huyo bwana mimi simjui ila mimi nimekaa Jpn muda mrefu sana nafanya nao kazi na nimekuwa na uhusiano mzuri sana na wataalamu wa JICA na JOVC na wengi wanapeekwa huko sio wataalamu kama wengi tunavyoamini. Mikataba yao ikiisha ili warudi Japan huwa wanalia na huwa ni ngumu sana kupata kazi Japan. Ukitaka kujua zaidi nitakujulisha zaidi.

Ila natumaini gharama zote zitakuwa zinagharamiwa na Japan na si serikali ya Tanzania.

Huu mradi wa huyu bwana mimi binafsi naujua. Malawi wamejaribu kuanzisha mradi kama huo unaitwa ONE VILLAGE ONE PRODUCT unaweza ku google. Kati ya Miradi yote 60% iliweza kuwa implemented na kati ya hiyo 2% ya miradi yote ndiyo imefanikiwa.

Tatizo ni kuwa You can adopt Good policy but if you have wron institutions you will not achieve your goals. But u can have wrong policy but good institutions na ukaachive good results. Hii ndio inayotukumba hata kwenye sera zinazotolewa na IMF na WB.

Swala la msingi hapa ni kuboreshe mazingira ya ndani, kuboresha miundo mbinu, taasisi za fedha, sheria kama za property right, invest in human capital etc.
 
1. Tunazungumzia mwaka 1961 sio mwaka 1661! Nchi zilizoendelea zilikuwa tayari zina vyuo na institutions zilizokomaa wakati walipotuacha sisi na wahandisi wanne.

2. Hawa walikaa miaka 41 bila kufanya lolote bado unaamini kuwa wangekaa zaidi ndiyo wangetujengea vyuo?

3. Hao hao waliomuona mwalimu mpuuzi kusisitizia kuwekeza kwenye elimu na social issues leo wamegeuka na kukubali kuwa bila kuwekeza katika sehemu hizo hakuna maendeleo. makosa yalifanyika ndiyo, lakini si katika kufanya asilimia karibu 80 ya watanzania wajue kusoma na kuandika.

4. Mashamba hayakuendeshwa na wazawa walio na digrii. Hao walikuwa wachache sana wakati wa Azimio la Arusha. Pamoja na hayo sipingi kuwa tulifanya makosa kutaifisha mashamba lakini hii haina maana kuwa tumelaaniwa. Mashamba hayakufa katika muda huo unaoutaja. mashamba haya yalikufa kama yalivyokufa mashamba mengi yaliyoendeshwa kijamaa hata huko kwa wazungu. Mfano mzuri ni USSR na Uchina.

5. Uzembe mwingi ulifanyika katika sekta ya elimu. Si hiyo tuu ya kutokuchapisha vitabu vinavyohitajika. wakati mimi nasoma ilikuwa hauwezi kwenda A-level kama haujafaulu masomo ya siasa na kiswahili. Ilikuwa ni lazima mjumbe wa nyumba kumi akupitishe ili uweze kwenda ng'ambo kwenye masomo ya ziada. Lakini haya ni matatizo ya sera na si ya ethnicity.

6. Mradi wa makao makuu umefanyika kisiasa ni makosa. Kama vile warusi walivyokausha ziwa lao kubwa kwa ajili ya mradi wa kilimo . Au wachina na zoezi la vita za utamaduni za Chairman Mao. Wote walifanya makosa ya kiitikadi na si rangi.

7. utakuwa unajidanganya kama utakana kuwa idadi ya wasomi na uwezo wa kujiendesha tulioachiwa na watawala wetu haukuwa na impact katika hali yetu ya sasa. hiyo performance unayoizungumzia wakati wa wakoloni ni ipi? Hali ya Native ilikuwaje. Ni kama kusema afrika kusini ilikuwa na hali nzuri wakati wa Apartheid kuliko sasa. kwa watawala labda lakini si kwa jamii yote.

8. Siwezi kukubishia kuhusu ethiopia. lakini hawa nao si waafrika kama sisi? au wahabeshi si nyani?

9. Tutaweza kujikosoa pale tu tutakapokubali hali yetu halisi, historia yetu na bila kutafuta hivi visingizio vyenu kuwa ndivyo tulivyoumbwa. Tutakapokataa kujiona tumelaaniwa na kudai kuwa tupimwe kama binadamu mwingine ndipo safari itakapoanza. Na safari hii ni ndefu na ina suluba nyingi lakini tukipania tutafika.

Fundi Mwenzangu:

Tukiacha siasa. Tulikuwa na bado tupo Naive na mambo ya pesa. Suala la kuwa mkoloni alituacha na mainjinia wanne halina mpango sana kama tungekuwa SAVY katika matumizi ya kipesa.

China na Urusi walifanya majaribio kibao katika siasa zao za ujamaa lakini walikataa kuchukua pesa kutoka WB na IMF.

Komredi Mkandara anasema kuwa Nyerere alichukua grant kujenga UDSM na Urafiki. Huo sio ukweli Nyerere alikopa lakini alikuwa Naive katika mambo ya mikopo na ikamtokea puani. Kasomesha watu, watu wanamaliza shule nchi mdabwada, nchi haina pesa.

Jamii za kiAfrika hazijazoea mambo ya mikopo. Na mfano mkubwa ni tuliokuja Marekani (Land of Opportunity) na kuanza kununua nyumba kwa kutumia mikopo tusiyojua hesabu za na sasa inatutokea puani na nchi ndicho kilichokuta nchi kama Tanzania.

Tukirudi kwenye mada. Unasema kuwa tuna priorities zingine na R & D hatuwezi. Watu wakisema NDIO TULIVYO, unaleta Uzalendo. Hii mada ina makundi mawili tu (kama binary function). Kundi la kwanza ni kukubali kuwa tunaweza na vitu gani vifanyike. Kundi la pili NDIVYO TULIVYO, ukiwa mjanja wewe ni Exceptional.
 
Hili ni jambo zuri sana tena sana. JK hongera kwa kuona mbali, waJapan wanajulikana dunia nzima kwa viwanda vyao ambavyo viko mbele sana kiteknologia, nakumbuka Mahathir Muhammad alifanya hivyo hivyo na leo tunaiona Malaysia kwa viwanda.

Ilimradi tuwasikilize maoni ya hao wataalam na tuyafatishe tusijidai kujuwa zaidi yao.

Anaetaka ushauri, akapewa na akaufatisha = Mtu kamili
Anaetaka ushauri, akapewa na asiufatishe = Mtu nusu
Asiyetaka ushauri, = hakuna mtu kabisaaaa.

Japan imejengwa na wajapan waliojifunza Ujerumani.

Korea imejengwa na wakorea waliojifunza USA.

China inajengwa na wachina waliojifunza USA, Ulaya na Japan.

Lakini Tanzania inajengwa kwa kuwaleta Wajapan Tanzania

Kumbe SISIEMU imeishiwa nyimbo kiasi hiki?

Tatizo linajulikana kwamba SISIEMU imebuma kwenye kila kitu. Sasa Mjapan huyu ni njama za kuongeza muda juu ya miaka 47 madarakani ili ionekane kazi inafanyika kumbe wapi .
 
Maendeleo ya watanzania na Africa kwa ujumla yatatoka kwa watanzania wenyewe.

Unajua bado Tanzania tunakasumba ya kutokuwa na imani na wataalamu wetu, Tunataasisi nyingi sana hapa Tanzania, vyuo vikuu na taasisi za Utafiti kibao ila kwa kasumba yetu tuliyo nayo ya kuamini kitu kizuri kinatoka nnje ndio haya sasa. Mkataba wake ukiisha akiondoka anaondoka na utaalamu wake.

Huku ni kuwadhalilisha wataalamu wetu wa nchini. Unajua Japan ndio wanatoa Technical Asistance na Financial Asistance. Haimaanishi kuwa wataalamu kutoka Japan ndio compitent na watawaletea maendeleo Japan. Ukitaka kujua Japan iliendelea je soma historia yake. Huyo bwana mimi simjui ila mimi nimekaa Jpn muda mrefu sana nafanya nao kazi na nimekuwa na uhusiano mzuri sana na wataalamu wa JICA na JOVC na wengi wanapeekwa huko sio wataalamu kama wengi tunavyoamini. Mikataba yao ikiisha ili warudi Japan huwa wanalia na huwa ni ngumu sana kupata kazi Japan. Ukitaka kujua zaidi nitakujulisha zaidi.

Ila natumaini gharama zote zitakuwa zinagharamiwa na Japan na si serikali ya Tanzania.

Huu mradi wa huyu bwana mimi binafsi naujua. Malawi wamejaribu kuanzisha mradi kama huo unaitwa ONE VILLAGE ONE PRODUCT unaweza ku google. Kati ya Miradi yote 60% iliweza kuwa implemented na kati ya hiyo 2% ya miradi yote ndiyo imefanikiwa.

Tatizo ni kuwa You can adopt Good policy but if you have wron institutions you will not achieve your goals. But u can have wrong policy but good institutions na ukaachive good results. Hii ndio inayotukumba hata kwenye sera zinazotolewa na IMF na WB.

Swala la msingi hapa ni kuboreshe mazingira ya ndani, kuboresha miundo mbinu, taasisi za fedha, sheria kama za property right, invest in human capital etc.

Mtoto wa mkulima,
..........ndg yangu hapo umemaliza yote....kula tano! Mkuu

Kama serikali yake (Japan) inalipa gharama za yeye kuja huku, hatukatai, sisi hapa tunawa-challenge viongozi wetu ya kwamba....tukiwa na nia....nilitumia neno UTASHI...sidhani kama kuna kitachoshindikana

........Ndg yangu Dar Es Salaam
kuja kwa huyo Mtaalamu toka Japan sio kitu cha ajabu cha kumfanya Waziri Waziri wetu kutamka aliyoyatamka.........kama ulivyosema mwenyewe kuna wataalamu wengi wako nchini tunashirikiana nao na vivyo hivyo wataalamu wetu wengi wako nje wanshirikiana na watu wa huko waliko...............NO BIG DEAL

BIG DEAL ni kupiga vita ufisadi ili kutoa nafasi kwa rasilimali zetu kutumika kwa faida yetu kwa kuwatumia wataalamu wetu kuonyesha.................miradi mingi sana imebuniwa na wataalamu wetu lakini haina support..........simply because haina 10% kwa mafisadi
 
Jamani Eeeeeh!

Mwambieni Mheshimiwa Kikwete anao wataalamu wengi kabisa wanaotosheleza sasa kutoa ushauri na kusimamia maendeleo ya Tanzania katika kila nyanja mhimu pale nchini.

Serikali yake inatakiwa iweke mikakati ya kuwatumia vizuri wataalamu hawa na kuwapa motisha kama hao wageni wanaoletwa kufanya mambo ambayo sisi wazawa tunayajua vizuri kabisa.

La Mhimu: Uongozi, Uongozi, na Uongozi; ukishirikiana na 'vision' iliyo sawa.

Mwambieni Kikwete aunde "TASK FORCE" ya wataalamu wachache wapitie na kuchambua ni viwanda vipi vinahitajika. Wachanganue pia sababu mhimu zilizosababisha juhudi zetu za kuendeleza viwanda vilivyokufa zishindwe, watoe mapendekezo ni yapi yafanyike ili safari hii mafanikio yapatikane.

Kama huyo mtaalamu wa Japan ni lazima awepo, basi ashirikiane na Task force hiyo.

Kwa ufupi - Kama Dr. Mwakyembe na kamati yake ya Bunge waliweza kufanya kazi ambayo wengi wetu humu JF tunakubali kuwa ilikuwa ni kazi nzuri; ni sababu zipi tunazoweza kuzitoa zinazotuzuia kusema kuwa wataalamu wa kufanya hii kazi ya viwanda hawapo?

Kikwete, we just need leadership with a vision, that's all. We are ready to take control of our own development. Tuachane na mambo ya omba omba ya kila kitu - mnatutia aibu!
 
Wazee huu utumwa wa mawazo bado tuao tuu kuwa mgeni ndie anaweza. Nakumbuka zamani tulikuwa na ma TX kibao kwani nchi ilikuwa wapi? Kila nchi itajengwa na wenye nchi. Kama ni kutupa utaalamu basi watupe elimu, tupeleke wataalamuwentu Japan wakajifunzi na sio kwenda kutalii na kila mtaalamu akirudi awajibike na awe anatakiwa kuonyesha output ya alichojifunza.

Utumwa huu sasa umeingia hata kwenye timu zetu za nyumbani kuanzia timu ya Taifa hadi club zote sasa zinataka mgen as long as ni mgeni basi watu wanakuwa na imani. Mimi najua kunamtaalamu mmoja wa Canada aliwahi kufanya kazi kwenye wizara moja nyeti jamaa alikuwa bogus kichizi na mshahara ulikuwa zidi ya Ddola 20,000 kwa mwezi na maslahi mengine na excemption kibao.

Naamini tunawataalamu wengi sana wa viwanda kama kina Dr. Semboja ni watu wanaoheshimika kila mahali tatizo ni kuwa hatuwatumii.

Niwape mfano wa mradi wa kilimo cha Mpunga Moshi chini. Huu ni mradi wa Japan na nimradi mzee sana lakini wataalamu wa JICA wenyewe wanasema mradi huo umeshindwa kunufaisha wananchi na wananchi wameshindwa kujifunza na kutransiform kilimo chao kuwa cha kisasa kama wanachofanya wajapan pale. Sababu ziko nyingi ni kwanini.

Tuwape nafasi wataalamu wetu watumie taaluma yao, tuweke mazingira mazuri ya uwekezaji kwa wenyeji na sio wageni kama sasa tunavyong'ang'ana, tuweke miundo mbinu, mashirika kama SIDO kwani yanafanya nini? tutumie taasisi zetu ipasavyo.

Kunahaja ya kutoa elimu kwa wananchi ilikuwa na maendeleo endelevu kwa kutumia rasilimali zao zilizopo. Serikali yenyewe ifacilitate kwa kutafuta masoko na kupunguza gharama za uzalishaji kama bara bara, umeme na maji. Wape elimu kuhusu umuhimu wa packaging na quality control etc. Naamini kuna watanzania wanavipaji ni vyakuendeleza tuu. Tuangalie ni maeneo ghani tuna comperative and competitive advantage. Naweza kuwapa mifano michache.

1. Viwanda vya kusindika samaki na dagaa.
2. Matunda na juice.
3. Sabuni kwa kutumia mawese na mimea mingine kama mwa40.
4. Ngogo za asili kama vitenge na khanga
5. Vinyago vya wamakonde badala ya kuuzwe na Kenya waendeleze na endeleza clusters kama vinyago vya mwenge na funiture za Keko pale watu wanazalisha.

Hiyo ni mifano michache tuu ila kuna vitu vingi vidogo vidogo tunatakiwa kufanya, hatuhitaji kutengeneza kiwanda cha kutengeneza magari au ndege kwa sasa.

Tumieni VETA na Vyuo vya ufundi na maenginer wetu. Serikali iandae maonyesho na mashindano ya wafanya biashara na wazalishaji wa ndani kila iwezekanapo.

Serikali ioneshe mfano wa kuwa wazelendo hasa kwa kuwapatia wazalishaji wa ndani masoko. MFANO sioni sababu ya serikali kuagiza funiture za kutoka China na kwingineko na si kununua kutoka ndani.
 
HAPO MIMI NAONA MNA KITU, KWANI KIPAUMBELE KILICHOWEKWA NI VIWANDA, NA MTALAAM HUYO NI WA VIWANDA, SIYO KILIMO. SASA IWEJE WAZIRI ASEME KWAMBA TUTAONDOKANA NA JEMBE LA MKONO? KWANI JEMBE LA MKONO WANALOTUMIA WAKULIMA KULE VIJIJINI LITAONDOLEWA KWA VINDA KWELI?

NI KWELI TUNAHITAJI MAENDELEO YA VIWANDA, LAKINI JE? NDIYO KIPAUMBELE CHETU? HAKUNA HATA HAJA YA KUSEMA SUA HAKUNA AGRO-MECHANICS IPO! ILA WANANCHI BADO HAWAJAWEZESHWA KUTUMIA HIZO NYENZO ZA NGO'MBE, TRACTORS, COMBINE HARVESTERS NK. SASA LEO TUAMBIWE HUYU MTALAAM WA VIWANDA ATASHAURI MPAKA TUONDOKANE NA JEMBE LA MKONO? THIS IS REDICOLOUS.

MTALAAM HUYO ANASEMA, USHAURI WAKE UNAJIKITA KWENYE VIWANDA VYA KUSINDIKA. LENGO LAKE NI KUISHAURI SERIKALI IALIKE WAWEKEZEJI!! DAMN IT? HII NDIYO KAZI YA MSHAURI WA KIMATAIFA ILI KUTUONDOA NA JEMBE LA MKONO?

TUKUMBUKE ILE METHALI YA MTEGEMEA CHA NDUGUYE HUFA MASIKINI, MASUALA YA MAENDELEO SI MAMBO YA KISIASA. HILO NAONA LINAHARUFU YA KISIASA.

Ni viwanda vingapi tulivyovi-taifisha na vikatushinda? hatuwezi, bado.

lakini hivyo hivyo vilivyotushinda sisi tukiwapa wawekezaji vianaendelea.

Elimu si kuta nne tu za darasani.

Juzi tu tumeona siku inafunguliwa kiwanja kipya cha mpira, tulipocheza na Mozambique, tulifanya nini pale kiwanjani?
 
Japan imejengwa na wajapan waliojifunza Ujerumani.

Korea imejengwa na wakorea waliojifunza USA.

China inajengwa na wachina waliojifunza USA, Ulaya na Japan.

Lakini Tanzania inajengwa kwa kuwaleta Wajapan Tanzania

Kumbe SISIEMU imeishiwa nyimbo kiasi hiki?

Tatizo linajulikana kwamba SISIEMU imebuma kwenye kila kitu. Sasa Mjapan huyu ni njama za kuongeza muda juu ya miaka 47 madarakani ili ionekane kazi inafanyika kumbe wapi .

Tatizo ni kwamba unasema na kujijibu mwenyewe, sasa kuna ubaya gani Tanzania ikileta mshauri wa Kijapan?
 
Dar Es Salaam,
Naelewa fika mkuu kuwa tunachoongelea hapa ni Ushauri!..
Ni ushauri huo huo umetuletea habari za viwanda vyetu vilivyokufa!..sikuona connection mkuu.
Sasa kama ingelikuwa ni jinsi ya kuvifufua labda ningeweza kuelewa mfano wako ulilenga kitu gani lakini tunapozungumzia kuondokana na jembe la mkono ktk swala la viwanda mkuu wangu sioni solution ya ushauri kutoka nje!. Ni ushauri huo huo toka nje uliotuingiza ktk madeal yote mabaya iwe IPTL, ama mikataba ya madini kina Sinclair wanazivuta hadi kesho.
Tatizo lipo ktk viongozi wetu kutotambua umuhimu wa mahitaji yetu sisi wenyewe. I mean hivi kweli utumiaji wa trector unahitaji mtaalam kutoka Japan kutuambia!, ama viwanda hivyo vitakuwa vinafanya nini kiasi kwamba yule mkulima wa jembe la mkono hawezi kuhitajika tena na hakuna mtaalam nchini aliyefikiria hivyo.
Trust me mkuu wangu mimi naona kama ni vyandarua vingine vinakuja badala ya sisi kuomba dawa za kuua mbu ama kufukia mashimo ya maji yaliyosimama, which is way cheap and the ONLY solution ya kuondokana na maleria.
Ama kweli awamu hii tumepata viongozi vilaza mkuu wangu, hizi safari zao kila siku huzua maajabu mara tutaahidiwa mvua za sayansi, huku nyuma wamechukua Richmond na tungekwisha maanake mvua zisinge kuwepo na Richmond deal lingeendelea kwa miaka 10.

Connection ni kuwa, kwa kuwa wenzetu wameanza zamani na wanaviwanda vikubwa vikubwa na vidogo vodogo vingi zaidi ye nchi nyingi tu duniani, kuna uwezekano mkubwa pia kuwa walishapita katika hali kama yetu, ya kuwa na viwanda vikafa kifo cha mende.
Na kuwataka ushauri wenzetu ambao wameshafnanikiwa katika hilo ambalo sisi limetushinda, tukapata ushauri ukawa ndio remedy kuna ubaya gani?

Hayo mengine uliyoongea hayana kichwa wala miguu wa kuungana na hili la mshauri.
 
Ni viwanda vingapi tulivyovi-taifisha na vikatushinda? hatuwezi, bado.

lakini hivyo hivyo vilivyotushinda sisi tukiwapa wawekezaji vianaendelea.

Elimu si kuta nne tu za darasani.

Juzi tu tumeona siku inafunguliwa kiwanja kipya cha mpira, tulipocheza na Mozambique, tulifanya nini pale kiwanjani?

Mkuu naomba tusiseme kuwa viwanda vilitushinda bali tatizo zilikuwa ni ubovu wa sera yenyewe mkuu. Sisi tulipo adopt sera ya viwanda Import substitution industry au tuiite Inward looking industrial strategy tulioverlook mambo mengi sana na hii sera ilishindwa kote ilikokuwa ikitumika zikiwemo nchi nyingine za Africa na Latin america. Sera hii ilikwamisha iliuwa viwanda vingine na sector kama kilimo kwa gharama ya viwanda tulivyokuwa tunavilinda. Kwa ufupi sera hii ilikuhusisa:-

i) kuongeza thamani ya shilingi yetu ili kufanya imports ziwe ghali. Kwa hiyo hata malighafi na capitak goods kama mashine zikawa ghali.

ii) Kuongeza kodi kwa imports ambazo.
iii) Kutoa ruzuku kwa baadhi ya viwanda na kutoza kodi kwa baadhi ya sector.

Zote hizi zilifanya wazalishaji wa ndani wasiwe competitive na na creative (kutafuta masoko, kupunguza gharama za uzalishaji na kuwekeza kwenye technolojia mpya) pia kuuwa sector nyingine. Wenzetu wa Far east waliadopt Export promotion na matokeo yao tunayaona.

Kitu kingine ni kuwa siasa ni uchumi kwa Tanzania. Unakuta mkuu wa kuwanda kachaguliwa na raisi au mkuu wa mkoa kwa sababu ni Kada wa chama na si kwa utaalamu, ujuzi na ufanisi wake.

Kilichokuwa kinazalishwa kama faida kulikuwa kinachukuliwa na serikali au wajanja wachache na sio kuwa reinvested.

Pia tatizo kubwa ni kuwa hatukuwa na ambacho Schumpeter anakiita incentive kwa enterprenure "CARROT & WIP" kwa sababu hivi viwanda vilikuwa vimeshikiliwa na serikali kwa hiyo waendeshaji hawana incentive ya kuongeza faida au hawana maumizu ya hasara. Hii ni kokote hata kama kuna wataalamu mkuu.

Ndio hatukuwa na wataalamu sana lakini sababu kubwa ni sera na namna ilivyokuwa implimented.
 
Nimefikia conclusion kuwa Tanzania na watanzania wote labda tunahitaji kuchapwa viboko ili tufikirie mambo ya maana kwanza na kuacha mengine.

Huyu mtaalam wa Japan ni bogus na to me ni usanii tu wa serikali.

Kuna ile report imetoka leo ambayo kina Tindu Lissu wameitoa kuhusu madini (Gold). Mbona wataalam wameshatoa opinion na ni common sense lakini serikali na sisi humu ndani discussion zetu wala hazijali ukweli uliopo kwenye losses za over 1 billion USD ambazo zingeweza kabisa kusaidia kilimo.

Also huyo Mary Nagu anaongea vitu ambavyo hata hajui, kilimo cha mkono solution ni serikali kuprovide makasio na matractor ili yakopeshwe kwa wakulima. oh sorry kipaumbele ni maVX kwa viongozi.

Hiyo ya kuhitaji kuchapwa viboko na kuunga mkono, ndio maana mpaka leo tu-masikini na mitaji ya asili tunayo. Inabidi tutafute washauri na huyu mmoja hatutoshi, kila sehemu tunahitaji washauri na mpaka watendaji hatuna, tunahitaji watendaji vile vile.

Leo kuna mifano hai kibao, wawekezaji wote, wameleta wataalam kutoka nje, hata makarani simpo tu. Kwa nini? jibu tunalo lakini hatutaki kuukubali ukweli, bado ni kidogo sana wawezao hapa kwetu na wengi (majority) ni opportunists tu. Utakaloambiwa fanya utasema unaliweza kumbe wapiiii? Hao wataalamu wetu mnaoongelea wako wapi? wanafanya nini? nani aliowazuia kuonyesha utaalam wao? mnaandikia mate wakati wino upo?
 
Mkuu naomba tusiseme kuwa viwanda vilitushinda bali tatizo zilikuwa ni ubovu wa sera yenyewe mkuu. Sisi tulipo adopt sera ya viwanda Import substitution industry au tuiite Inward looking industrial strategy tulioverlook mambo mengi sana na hii sera ilishindwa kote ilikokuwa ikitumika zikiwemo nchi nyingine za Africa na Latin america. Sera hii ilikwamisha iliuwa viwanda vingine na sector kama kilimo kwa gharama ya viwanda tulivyokuwa tunavilinda. Kwa ufupi sera hii ilikuhusisa:-

i) kuongeza thamani ya shilingi yetu ili kufanya imports ziwe ghali. Kwa hiyo hata malighafi na capitak goods kama mashine zikawa ghali.

ii) Kuongeza kodi kwa imports ambazo.
iii) Kutoa ruzuku kwa baadhi ya viwanda na kutoza kodi kwa baadhi ya sector.

Zote hizi zilifanya wazalishaji wa ndani wasiwe competitive na na creative (kutafuta masoko, kupunguza gharama za uzalishaji na kuwekeza kwenye technolojia mpya) pia kuuwa sector nyingine. Wenzetu wa Far east waliadopt Export promotion na matokeo yao tunayaona.

Kitu kingine ni kuwa siasa ni uchumi kwa Tanzania. Unakuta mkuu wa kuwanda kachaguliwa na raisi au mkuu wa mkoa kwa sababu ni Kada wa chama na si kwa utaalamu, ujuzi na ufanisi wake.

Kilichokuwa kinazalishwa kama faida kulikuwa kinachukuliwa na serikali au wajanja wachache na sio kuwa reinvested.

Pia tatizo kubwa ni kuwa hatukuwa na ambacho Schumpeter anakiita incentive kwa enterprenure "CARROT & WIP" kwa sababu hivi viwanda vilikuwa vimeshikiliwa na serikali kwa hiyo waendeshaji hawana incentive ya kuongeza faida au hawana maumizu ya hasara. Hii ni kokote hata kama kuna wataalamu mkuu.

Ndio hatukuwa na wataalamu sana lakini sababu kubwa ni sera na namna ilivyokuwa implimented.

Na hizo sera tulizibadilisha lini na viwanda tumevigawa lini?

Kwa sababu tu tutatooa lukuki, lakini at the end of the day
tumeshindwa kama tunavyoshindwa kote.

Hizo sera si zetu wenyewe? tutalaumu mtu katupangia, hebu tuwacheni huyu mshauri aje afanye mambo yake.

Hivi leo ni uwezo gani tulionao wa kujenga kiwanda hapa Tanzania bila kutegemea nje? nani ataejenga kiwanda hapa Tanzania? hata sindano ya kushonea tunahitaji kutoka nje, kwa nini? HATUNA WATAALAM HAPA? Ngoja tuwe na uwezo wa kutenda hayo ambayo tunahitaji kutoka nje, iwe kwa kununuwa wenyewe au kuwekezewa.

Tusijidai tunaweza kila kitu kumbe bado.

Au tu kwa sababu JK ndie aliesemwa kuwa hayo ni matunda ya ziara yake ya Japan, ndio kuna watu roho zinawauma?
 
Kwa wale wanaopinga kuja kwa washauri kutoka nje, nataka kuwakumbusha kuwa hilo halijaanza leo, halitaisha leo, hata nchi zilizoendelea zinahitaji ushauri kutoka kila kona ya dunia na isiwe ni kiroja kwa kuwa JK kaleta mshauri wa ki Japan. Tazama hii link, inaonyesha makubaliano wakati wa Nyerere:

[media]http://untreaty.un.org/unts/60001_120000/4/30/00007493.pdf[/media]

hivi sasa nisemavyo tuna washauri wengi tu kutoka nje na tunao washauri wetu wengi tu nje.
 
Na hizo sera tulizibadilisha lini na viwanda tumevigawa lini?

Kwa sababu tu tutatooa lukuki, lakini at the end of the day
tumeshindwa kama tunavyoshindwa kote.

Hizo sera si zetu wenyewe? tutalaumu mtu katupangia, hebu tuwacheni huyu mshauri aje afanye mambo yake.

Hivi leo ni uwezo gani tulionao wa kujenga kiwanda hapa Tanzania bila kutegemea nje? nani ataejenga kiwanda hapa Tanzania? hata sindano ya kushonea tunahitaji kutoka nje, kwa nini? HATUNA WATAALAM HAPA? Ngoja tuwe na uwezo wa kutenda hayo ambayo tunahitaji kutoka nje, iwe kwa kununuwa wenyewe au kuwekezewa.

Tusijidai tunaweza kila kitu kumbe bado.

Au tu kwa sababu JK ndie aliesemwa kuwa hayo ni matunda ya ziara yake ya Japan, ndio kuna watu roho zinawauma?

Mkuu Dsm Mtaalamu aletwe sijapinga kuletwa mtaalamu, Kila nchi hata Japan yenyewe na US ina wataalamu kutoka nnje. Mimi ninachosema ni kuwa, sisi tunawataalamu wa ndani. hawa wataalamu wa ndani tunatakiwa tuwatumie. Tutawatumia je?

Kama tunaleta mtaalamu wa nnje kwa mkataba lets say wa 5 year awe yuko attached na wataalamu wetu wa nndani ili aweze kutransfer knowedge na akiondoka ujuzi ubakie na si akiondoka na mradi unakufa.

Japan wakati inaendelea ilikuwana na sera kama hizi na qute.
"3 Education Policies of Meiji Gvt to Build the Economy"
- Send talented student abroad in the field of Gvt administration, finance, engeneering and industry.
-- Invite foreign professors and technicians to Japan
-- Write text books in japanese by Japanese.
Source: www.nifty.com (Tamagawa University 2006)"

Kutumia au kushirikisha wataalamu wa ndani ni muhimu sana mkuu.
Hii ni muhimu sana mkuu. Mazingira ya Japan na tanzania ni tofauti sana. Akija na utaalamu wake ukawa adoped na mazingira yetu ya ndani hiyo ni nzuri. Ni muhimu na ni vizuri sana wanavyofanya JICA/Japan kwani wanatupa utaalamu napendelea sana watufundishe kuvua samaki na si kutupa samaki mkuu.

Tatizo langu mkuu sio kuwa tusilete wataalamu lakini hii tabia ya kuamini kuwa kila kizuri kinatoka nnje ni soo ipo siku tutaleta raisi mtaalamu kutoka nnje ili aje atuongozee nchi yetu.
 
Back
Top Bottom