WHO: Corona Virus inaweza isiondoke
WHO yakubali msimamo wa Tanzania kuhusu ‘lockdown’





Na Mwandishi Wetu
GENEVA, Mjumbe Maalum wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na Mkurugenzi Mkuu wa Convid-19, Dkt.David Nabarro amependekeza kuwe na jamii ambayo watu watakuwa tayari kuuzoea na kuishi na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) badala ya kuendelea kuwekewa zuio la kukaa ndani (lockdown) au kutoka kwa mashariti, kwani hatua za awali zinaonyesha hakuna chanjo au tiba ya virusi hivyo.
Wachambuzi wa masuala ya afya wameueleza mtandao wa TimesMajira Online kuwa, hatua hiyo ni ushindi mkubwa kwa misimamo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo tangu awali ilikataa kuweka zuio la watu kukaa ndani, ikiwa ni agizo la Rais Dkt. John Magufuli huku akiwasisitiza wananchi kuzingatia miongozo yote inayotolewa na Serikali ikiwemo kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, kuvaa barakoa, matumizi ya vitakasa mikono na kuepuka mikusanyiko isiyokuwa ya lazima.
Dkt.Nabarro ametoa taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya Twitter akisema kwamba kuendelea kuwawekea watu zuio, kunaweza kuwaumiza zaidi kutokana na athari zake kwa watu na uchumi wa mataifa kwa jumla.
“Virusi hivi vitakuwa na sisi kwa siku za usoni inayoonekana na hakuna mtu anayetaka kuwa katika zuio,kama tulivyo na wakati huu,”amesema.

Fuata link ifuatayo for more information.

WHO yakubali msimamo wa Tanzania kuhusu 'lockdown' - TimesMajira
Ushindi huo maana yake ni nini hasa? Kwamba Rais Magufuli amefanikiwa kudhiti korona au kudhibi athari ya mlipuko kiuchumi?
 
Tatizo Baba alianza kutenga watoto kwa nguo wanazovaa wakati wote ni watoto wake wa kuzaa.

Baadae Baba akaanza kuwafanyia kila aina ya ukatili watoto asiowapenda.

Sasa watoto hawampendi tena Baba na wanatamani afe. Kuskia hivyo watoto pendwa wanadai wenzao wana laana...

Mwambie Baba asitenge watoto, Mwambie Baba kuwa akiingia jambazi nyumbani asikimbie kujificha chumbani na kuacha vita iendeshwe na watoto huku yeye akitoa maagizo tu...

Ukiwapenda watoto wako...watajua,
Ukiwachukia watoto wako...watajua,

Za kuambiwa changanya na zako

In Vino Veritas (In Wine Lies the Truth)
 
Nkuruzinza has expelled WHO out Bujumbura for good
 
Back
Top Bottom