Who is Fatma Karume? | Fatma Karume ni nani?

Who is Fatma Karume? | Fatma Karume ni nani?

Mtoto bora kabisa wa marais kuwahi tokea Tanzania ,huwezi mlinganisha na hao wengine kina Rizone wanaobebwa bebwa kichwani hakuna kitu, au Makongoro sijui.

Anaye mfahamu mtoto yoyote wa marais waliowahi shika bara na visiwani anayemshinda kiupeo huyu Fatma Karume ,na amtaje hapa
 
Ni kweli nakubali hapo ningekula Zero unajua ilikaa kama Tundu Lisu ana undugu na huyo dada sema na huyu Ngosha anatupagawisha mpaka tunakuwa out of topic nakubali kwa mikono miwili hii 'Zero ' yangu, no hard feeling
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
FATMA KARUME!

Pamoja na kutofautiana itkadi na huyu mama lakini bado inabidi nikubali kwamba ni kiongozi 'potential' wa nchi hii!

Kutokana na harakati chache ninazoona akishiriki imebidi nikubali kwamba 'KWELI ANALITENDEA HAKI JINA LA BIBI YAKE, FATMA KARUME, MJANE WA HAYATI, SHAHID, RAIS WA KWANZA WA ZANZIBAR ABEID AMAN KARUME!'

Mwnye kujua japo historia yake fupi na achangie tunogeshe baraza!






KARIBUNI WADAU!
 
Ni Mwanaharakati Mpya Mzuri
Msomi, Anayejitambua, Jasiri.
Kwa Kweli Nimevutiwa Na Huyu
Wakili Msomi Fatuma Karume
Kwa Udhubutu Ukizingatia Ni
Mwanamke.
 
Nimewatazama wanawake wote walio katika ulingo wa siasa sijawahi kuona wala kumuamini hata mmoja katika nafasi ya urais..

Lakini kwa huyu Fatma Karume, nimekuwa mwepesi sana kushawishika kwamba anatosha kabisa kuwa mkuu wa nchi!

Kwangu mimi Fatma namuona kama mwanamama wa tofauti sana!
 
Kajitahid kumake headlines wiki 2 mfululizo

Wewe umeanza kumtilia maanani baada ya kumuona akijishughulisha na kesi za Lissu tuu! Angalia hizo video mbili utuambie kama ni za hii habari nyepesinyepesi ya msemahovyo Lissu pia!
Yaani sasa naona anaanza kulitia Tembo maji kwa kujimiksi na watu wasio na maana!
 
hivi kuna wakili sio msomi??
Binafsi, Mimi Sio Mwanasheria
Ila Kwa Uelewa Wangu Mdogo
Nafahamu Kila Mtu Anaweza
Kuwa Au Kuitwa "Wakili" Kwa
Namna Moja Ama Nyingine.
Kibiblia Yesu Anaitwa Wakili
Kutokana Na Kutetea Makosa
Yetu. Turudi Kwenye Neno "wakili
Msomi" Ni Asili Ya Neno "Learned Brother Or Sister" Kutoka Ulaya.
Dhumuni Ni Kuweka Utofauti ( Distinction) Ya
Wakili Ambaye Amesomea Sheria
Na Yule Ambaye Hana Ujuzi Wa
Taaluma Ya Sheria.
 
Binafsi, Mimi Sio Mwanasheria
Ila Kwa Uelewa Wangu Mdogo
Nafahamu Kila Mtu Anaweza
Kuwa Au Kuitwa "Wakili" Kwa
Namna Moja Ama Nyingine.
Kibiblia Yesu Anaitwa Wakili
Kutokana Na Kutetea Makosa
Yetu. Turudi Kwenye Neno "wakili
Msomi" Ni Asili Ya Neno "Learned Brother Or Sister" Kutoka Ulaya.
Dhumuni Ni Kuweka Utofauti ( Distinction) Ya
Wakili Ambaye Amesomea Sheria
Na Yule Ambaye Hana Ujuzi Wa
Taaluma Ya Sheria.
Duuh.... ! Wakili Yesu ! Hii sijawahi ona mabuku yotee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimewatazama wanawake wote walio katika ulingo wa siasa sijawahi kuona wala kumuamini hata mmoja katika nafasi ya urais..

Lakini kwa huyu Fatma Karume, nimekuwa mwepesi sana kushawishika kwamba anatosha kabisa kuwa mkuu wa nchi!

Kwangu mimi Fatma namuona kama mwanamama wa tofauti sana!
Akili za ki ukawa hizo, hata Lowassa mliona anafaa after years of hatred

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom