100 others Inaonekana hujasoma replies zangu zote, maana comment kama hii nimeishaijibu. Anyway, ngoja nikusaidie:
Yesu hakuwapa watu sumu. Nashukuru ume-bold hiyo sentensi yenye maneno "
divai nzuri"
Kinywaji chenye sumu kinaweza kuitwa kizuri? Yesu alitengeneza divai njema/nzuri, siyo ile iliyochacha
Neno ‘divai’ katika Biblia linatumika kwa maana pana: Wakati mwingine linamaanisha juisi safi ya zabibu (Isaya 65:8). Na wakati mwingine ni divai yenye kilevi iliyochacha (fermented). Hivyo ukisoma maandiko yenye neno divai, inabidi usome kwa muktadha.
Yesu alikuja kuleta uzima, iweje tena awanyweshe watu kinywaji chenye sumu ya kuharibu ini na ubongo?
Kumbuka pia wakati wa arusi watu wanakunywa sana. Sasa kama divai ile ingekuwa na kilevi, ni wazi wangelewa. Hivyo Yesu asingetengeneza kinywaji cha kuwafanya watu walewe halafu aseme walevi hawataingia mbinguni.
1 Kor 6:9-10
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi.