WHO wathibitisha pombe ni sumu. Sasa nina ujasiri wa kusema: "kunywa pombe bila kulewa ni dhambi."

WHO wathibitisha pombe ni sumu. Sasa nina ujasiri wa kusema: "kunywa pombe bila kulewa ni dhambi."

Unywe pombe usinywe miaka yetu imehesabiwa kwenye biblia. Miaka ya kuishi kiumbe kilichozaliwa na mwanamke 70...ikizidi saana 79/80 usijihangaishe
Issue ni utaishi wapi baada ya kufa? Mbinguni au motoni? Kifo sio mwisho wa maisha.
 
Hoja yako ya kisayansi kuhusu nyama nyekundu ni sahihi kwa muktadha wa afya, lakini sio sahihi kwa muktadha wa dhambi
Kwanini nyamq nyekundu isiwe dhambi sababu nayo inaharibu hekalu la Mungu
Pombe iko kwenye kundi tofauti kabisa: WHO imeiweka kama Group 1 carcinogen, yaani inahusishwa moja kwa moja na saratani kwa binadamu
Sausage and other processed meat zipo group 1 pia nazo zinaharibu hekalu la Mungu kama pombe inavyofanya.

Wito wangu nakuomba usibague unapo address hivi vitu waambie pia, Ugali, Wali na Ngano ndio chanzo kikuu cha Kisukari na Magonjwa mengine yasiyo ambukiza, hayo yote yanaharibu hilo unaloita hekalu la Mungu.

Anyway Tutaongea sana lakini suluhusho letu ni Kristo, Je Yesu alisema nini kuhusu vyakula na Vinywaji kuleta dhambi... Pitia hapa ndugu Setfree

Mk 7:18-19 SUV
[18] Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi; [19] kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote.

Sasa hebu utuambie kati ya wewe plus aya zote ulizoweka VS maneno ya moja kwa moja ya Yesu ni yupu tumfuate? Tukufuate Setfree au tumsikie Kristo?
 
Huna akili bana, unatumia A.I kudhani watu wataacha beer? Unakichaa kikubwa. Haohao WHO, wamebadilisha defintion ya watu wa upinde kutoka gender identity disorder na kuwa kitu normal una akili timamu wewe? Kwanza unafahamu juu ya guidelines? Alafu unafahamu alcoho haijawekwa kama ni causative agent? Acha ujuaji. You are an acting pseudo-smart.
Your response, unfortunately, leans heavily on ad hominem attacks rather than objective reasoning. Labeling someone 'kichaa' or 'pseudo-smart' does not qualify as a rebuttal, it only underscores a lack of substantive engagement with the argument.

The classification of alcohol as a Group 1 carcinogen by the WHO is a matter of established science, not personal conviction.

If you take issue with this position, the intellectually honest path is to critique the data or the methodology, not the person presenting it. Resorting to emotional rhetoric and mockery, contributes nothing to meaningful discourse.

You may dismiss it as AI, but critical thinking and fact-based reasoning predate any algorithm.
 
Ukichanganya ya Mungu na ya Kaizari umepotea dada. Ya Mungu mpe Mungu na ya Kaizari mpe Kaizari. Sasa WHO na Biblia unaviunganishaje?

Ukiendelea hivyo kuna siku utaleta bandiko linalohusu LGBTQ uunganishe na mistari ya Biblia alafu uanze kusifia.
 
Kama ulikuwa huna habari, kisayansi, pombe ni sumu. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa Ethanol, kiambato kikuu katika pombe, ni dutu ya sumu kwa mwili wa binadamu. Shirika la Afya Duniani (WHO) through International Agency for Research on Cancer (IARC) linaiainisha pombe (ethanol in alcoholic beverages) kama Group 1 carcinogen, sawa na tumbaku, asbestos, na virusi kama HPV.

Pombe inaharibu ini, ubongo, moyo, na hata mfumo wa kinga. Hakuna kiwango salama cha pombe kilichothibitika kuwa hakileti madhara.
WHO, 2023: “There is no safe amount of alcohol that does not affect health"

Sasa tukija kwenye Maandiko, katika kitabu cha 1 Wakorintho 6:19-20 tunaambiwa hivi: “...hamjui ya kuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu… Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu.”

Andiko hilo linatufundisha kwamba mwili wa Mkristo ni Hekalu la Mungu. Hekalu hili hatutakiwi kuliharibu. Ukiliwekea sumu unaliharibu. Unaliua. Mungu hapendi tuliharibu hekalu hili, yaani miili yetu. Angalia anavyosema katika kitabu cha 1 Kor 3:17
"...mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi."

Kama tulivyoona kauli hiyo ya WHO, kunywa pombe, hata kidogo tu, ni kuweka sumu mwilini(katika hekalu la Mungu). Na ethanol(ethyl alcohol) iliyomo katika pombe, tumeona kuwa ni sawa na sumu ya tumbaku na asbestos!

Kama unadai pombe unayokunywa haikuletei madhara yoyote katika mwili, bado unapingana na Mungu, kwa sababu ametukataza hata kuwa miongoni mwao wanywao.
"Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo" (Mithali 23:20-21)

Ili ujue kwamba Mungu anachukizwa na pombe, angalia hapa anavyotukataza hata kumpa jirani kileo. Yaani wewe hunywi lakini ukimpa jirani yako pombe tayari ni dhambi
"Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo."(Habakuki 2:15)

Tumekatazwa pia hata kuitamani pombe.
Methali 23:31
"Usiitamani divai hata kwa wekundu wake, hata kama inametameta katika bilauri, na kushuka taratibu unapoinywa."

Kwa ushahidi huo wa kisayansi na wa ki-Maandiko, bado tu unadhani kunywa pombe "kidogo" bila kulewa sio dhambi? NIPE UTETEZI WAKO.
================
Ndugu zangu, mambo yanayofanyika duniani sasa: vita, kuongezeka kwa maasi, upendo wa wengi kupoa, kuongezeka kwa maarifa... ni dalili za wazi kuwa Yesu amekaribia kuja kulinyakua Kanisa. Tutafute utakatifu kwa bidii(Ebr 12:14) vinginevyo Yesu akija tutaachwa katika dhiki kuu.

Itakuwa kilio na kusaga meno ukiachwa Yesu atakapokuja. Maisha yako yote umekuwa ukienda kanisani, lakini siku ya kuja kwa Yesu uachwe kwa sababu ya kunywa pombe tu?? Jamani, mbinguni kuna raha tele. Tutakula na kunywa vinono huko. Tuwe na subira!
Kwani pombe ilikufanya nini lakini, emu tuache bana
 
Ndugu yangu Servus
Soma Maandiko kwa ufahamu. Yesu hakunywa pombe. Watu waliompinga ndio waliomsingizia. Maandiko hayasemi alikuwa mlevi. Walimuita ‘mlafi na mlevi’ kwa kumkejeli tu. Angekuwa anakunywa, asingesema walevi hawataurithi ufalme wa Mungu (1 Wakorintho 6:9-

Kwa namna ulivyoanza vizuri, sikutarajia kama pengine ungeamua kuikana biblia na kuingiza usanii. Unachosema ni kwamba fungu hili linasema uongo, na msingi wa kauli yako umeutoa andiko gani?

Pengine Kuna haja ya wewe kujipa muda wa kujifunza ili kile unachokihubiri kiwe na base ya maandiko badala ya kujikita kwenye hisia na tafsiri zako binafsi.
 
Ndugu yangu Servus
Soma Maandiko kwa ufahamu. Yesu hakunywa pombe. Watu waliompinga ndio waliomsingizia. Maandiko hayasemi alikuwa mlevi. Walimuita ‘mlafi na mlevi’ kwa kumkejeli tu. Angekuwa anakunywa, asingesema walevi hawataurithi ufalme wa Mungu (1 Wakorintho 6:9-10)
Divai ni juice?
 
Aisee kama warembo ndio kilevi chako basi ujue hiyo ni sumu kali kuliko pombe! Sura za warembo zinaweza kukuletea magonjwa hatari kama gonorrhea, chlamydia, syphilis, UKIMWI, na hata hepatitis B!

Mbaya zaidi ukiondoka duniani utatupwa motoni. Chagua leo: kilevi chako kiwe Neno la Mungu(Biblia). Isome kila siku uyajue mapenzi ya Mungu
Wewe ni mrembo ?
 
Usiweke mistari nusunusu kuogopesha watu andika mstari mzima hiyo Habakuki 2:15 Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!
Dhambi hapo si unaoona ni kumlewesha mtu na kutazama uchi?ukilewa mwenyewe ukarudi zako kwa mke wako bila kupitia kwa makahaba kuna shida gani?
 
Kama ulikuwa huna habari, kisayansi, pombe ni sumu. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa Ethanol, kiambato kikuu katika pombe, ni dutu ya sumu kwa mwili wa binadamu. Shirika la Afya Duniani (WHO) through International Agency for Research on Cancer (IARC) linaiainisha pombe (ethanol in alcoholic beverages) kama Group 1 carcinogen, sawa na tumbaku, asbestos, na virusi kama HPV.

Pombe inaharibu ini, ubongo, moyo, na hata mfumo wa kinga. Hakuna kiwango salama cha pombe kilichothibitika kuwa hakileti madhara.
WHO, 2023: “There is no safe amount of alcohol that does not affect health"

Sasa tukija kwenye Maandiko, katika kitabu cha 1 Wakorintho 6:19-20 tunaambiwa hivi: “...hamjui ya kuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu… Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu.”

Andiko hilo linatufundisha kwamba mwili wa Mkristo ni Hekalu la Mungu. Hekalu hili hatutakiwi kuliharibu. Ukiliwekea sumu unaliharibu. Unaliua. Mungu hapendi tuliharibu hekalu hili, yaani miili yetu. Angalia anavyosema katika kitabu cha 1 Kor 3:17
"...mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi."

Kama tulivyoona kauli hiyo ya WHO, kunywa pombe, hata kidogo tu, ni kuweka sumu mwilini(katika hekalu la Mungu). Na ethanol(ethyl alcohol) iliyomo katika pombe, tumeona kuwa ni sawa na sumu ya tumbaku na asbestos!

Kama unadai pombe unayokunywa haikuletei madhara yoyote katika mwili, bado unapingana na Mungu, kwa sababu ametukataza hata kuwa miongoni mwao wanywao.
"Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo" (Mithali 23:20-21)

Ili ujue kwamba Mungu anachukizwa na pombe, angalia hapa anavyotukataza hata kumpa jirani kileo. Yaani wewe hunywi lakini ukimpa jirani yako pombe tayari ni dhambi
"Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo."(Habakuki 2:15)

Tumekatazwa pia hata kuitamani pombe.
Methali 23:31
"Usiitamani divai hata kwa wekundu wake, hata kama inametameta katika bilauri, na kushuka taratibu unapoinywa."

Kwa ushahidi huo wa kisayansi na wa ki-Maandiko, bado tu unadhani kunywa pombe "kidogo" bila kulewa sio dhambi? NIPE UTETEZI WAKO.
================
Ndugu zangu, mambo yanayofanyika duniani sasa: vita, kuongezeka kwa maasi, upendo wa wengi kupoa, kuongezeka kwa maarifa... ni dalili za wazi kuwa Yesu amekaribia kuja kulinyakua Kanisa. Tutafute utakatifu kwa bidii(Ebr 12:14) vinginevyo Yesu akija tutaachwa katika dhiki kuu.

Itakuwa kilio na kusaga meno ukiachwa Yesu atakapokuja. Maisha yako yote umekuwa ukienda kanisani, lakini siku ya kuja kwa Yesu uachwe kwa sababu ya kunywa pombe tu?? Jamani, mbinguni kuna raha tele. Tutakula na kunywa vinono huko. Tuwe na subira!
Acha pombe ufe kwa msongo wa mawazo!!
 
Ukichanganya ya Mungu na ya Kaizari umepotea dada. Ya Mungu mpe Mungu na ya Kaizari mpe Kaizari. Sasa WHO na Biblia unaviunganishaje?

Ukiendelea hivyo kuna siku utaleta bandiko linalohusu LGBTQ uunganishe na mistari ya Biblia alafu uanze kusifia.
Asante flank kwa maoni yako.
Kuwataja WHO haimaanishi kuchanganya ya Mungu na ya Kaisari, bali ni kuonyesha kuwa hata taasisi za kidunia zinathibitisha kile ambacho Biblia iliishasema zamani:
'Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.’ (Methali 20:1).
Usiutazame mvinyo iwapo ni mwekundu; uitiapo bilauri rangi yake, ushukapo taratibu; Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira.(Mithali 23:31-32)

Ukweli wa Mungu hausimami juu ya WHO, bali WHO ikisema kweli, tunaitumia kama shahidi wa pili, kama ilivyoandikwa:
‘Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa.’ (2 Wakor 13:1)

Umenipata?
 
Back
Top Bottom