Kama ulikuwa huna habari, kisayansi, pombe ni sumu. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa Ethanol, kiambato kikuu katika pombe, ni dutu ya sumu kwa mwili wa binadamu. Shirika la Afya Duniani (WHO) through International Agency for Research on Cancer (IARC) linaiainisha pombe (ethanol in alcoholic beverages) kama Group 1 carcinogen, sawa na tumbaku, asbestos, na virusi kama HPV.
Pombe inaharibu ini, ubongo, moyo, na hata mfumo wa kinga. Hakuna kiwango salama cha pombe kilichothibitika kuwa hakileti madhara.
WHO, 2023: “There is no safe amount of alcohol that does not affect health"
Sasa tukija kwenye Maandiko, katika kitabu cha 1 Wakorintho 6:19-20 tunaambiwa hivi: “...hamjui ya kuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu… Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu.”
Andiko hilo linatufundisha kwamba mwili wa Mkristo ni Hekalu la Mungu. Hekalu hili hatutakiwi kuliharibu. Ukiliwekea sumu unaliharibu. Unaliua. Mungu hapendi tuliharibu hekalu hili, yaani miili yetu. Angalia anavyosema katika kitabu cha 1 Kor 3:17
"...mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi."
Kama tulivyoona kauli hiyo ya WHO, kunywa pombe, hata kidogo tu, ni kuweka sumu mwilini(katika hekalu la Mungu). Na ethanol(ethyl alcohol) iliyomo katika pombe, tumeona kuwa ni sawa na sumu ya tumbaku na asbestos!
Kama unadai pombe unayokunywa haikuletei madhara yoyote katika mwili, bado unapingana na Mungu, kwa sababu ametukataza hata kuwa miongoni mwao wanywao.
"Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo" (Mithali 23:20-21)
Ili ujue kwamba Mungu anachukizwa na pombe, angalia hapa anavyotukataza hata kumpa jirani kileo. Yaani wewe hunywi lakini ukimpa jirani yako pombe tayari ni dhambi
"Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo."(Habakuki 2:15)
Tumekatazwa pia hata kuitamani pombe.
Methali 23:31
"Usiitamani divai hata kwa wekundu wake, hata kama inametameta katika bilauri, na kushuka taratibu unapoinywa."
Kwa ushahidi huo wa kisayansi na wa ki-Maandiko, bado tu unadhani kunywa pombe "kidogo" bila kulewa sio dhambi? NIPE UTETEZI WAKO.
================
Ndugu zangu, mambo yanayofanyika duniani sasa: vita, kuongezeka kwa maasi, upendo wa wengi kupoa, kuongezeka kwa maarifa... ni dalili za wazi kuwa Yesu amekaribia kuja kulinyakua Kanisa. Tutafute utakatifu kwa bidii(Ebr 12:14) vinginevyo Yesu akija tutaachwa katika dhiki kuu.
Itakuwa kilio na kusaga meno ukiachwa Yesu atakapokuja. Maisha yako yote umekuwa ukienda kanisani, lakini siku ya kuja kwa Yesu uachwe kwa sababu ya kunywa pombe tu?? Jamani, mbinguni kuna raha tele. Tutakula na kunywa vinono huko. Tuwe na subira!