WHO wathibitisha pombe ni sumu. Sasa nina ujasiri wa kusema: "kunywa pombe bila kulewa ni dhambi."

WHO wathibitisha pombe ni sumu. Sasa nina ujasiri wa kusema: "kunywa pombe bila kulewa ni dhambi."

Biblia haijipingi. Unatakiwa uisome kwa kuzingatia context. Habari ya Paulo kumwambia Timotheo anywe mvinyo nimeishaifafanua. Soma reply.
Bibilia na Quruan zina contradictions nyingi mno, hata ukizingatia context.

Hii ni kwa sababu zilitungwa na watu tu waliokuwa wameshiba ugali.
 
Sasa ww unakataza tusinywe. na sio kusema tunywe kwa tahadhali.
Sijakataza mimi. Aliyekataza ni Mungu aliyetuumba. Ndio sababu nimeweka Maandiko
Unatusimanga sana wakat tunachangia maendeleo ya nchi kwa kulipa kodi...
Kwani maendeleo ya nchi ni lazima yaletwe na pombe? Mbona kuna nchi pombe imepigwa marufuku kabisa lakini wako juu kiuchumi? Saudi Arabia ni moja ya nchi zenye uchumi mkubwa zaidi duniani lakini pombe huko imepigwa marufuku.
Saudi Arabia ina GDP (2024): zaidi ya $1.1 trilioni
Miji kama Riyadh na Jeddah zina maendeleo ya kisasa na miradi ya kiteknolojia kama NEOM bila kutegemea pombe
Unajua wafanya kaz wa hivi viwanda na wamiliki na wauzaji wa pombe wanafamilia pia au wanategemea kaz hii hii ya kuuza bia.

min -me bro. tunasengenywa sana aisee
Ukisema hivyo hata wauza bangi wanaweza kusema wana familia zinazotegemea kula kutokana na mapato ya kuuza bangi na madawa ya kulevya. Hao wanaotegemea pesa za viwanda vya kuuza pombe, wakiwa na nia kweli ya kuacha, Mungu anaweza kuwapa kazi nzuri zaidi za kuwaingizia kipato
 
Ni sawa useme kiwanda cha Sigara kifungwe wakati huo kimeajiri maelfu ya watu na wao waanafanya kazi na kuendesha familia kwa kazi hio hio ya kutengeneza stimulating materials
Mimi sijasema kiwanda kifungwe. Usinilishe maneno. Ukiacha wewe kufanya kazi kwenye kiwanda cha sigara au pombe, Atheists watafurahi, wataenda ku-replace nafasi yako.
Halafu, sio kila kinachoajiri watu ni sawa mbele za Mungu. Hata Madanguro pia huajiri maelfu, biashara ya madawa ya kulevya inawanufaisha wengi, lakini zote ni dhambi. Ni kweli familia zinalishwa, lakini nafsi zinapotea. Maandiko yanasema itamfaidia nini mtu akiupata ulimwengu wote(including pesa) halafu nafsi yake iangamie? (Mathayo 16:26)
 
Hata kuzaliwa na kuishi ni chanzo cha magonjwa na vifo. Kwa kifupi tatizo ni mwili
Duh, chanzo cha magonjwa ni dhambi iliyotendwa na Adam na Hawa. Mungu alipoiumba dunia haikuwa na magonjwa kabisa. Na Yesu alisema anaenda kutuandalia makao. Makao hayo hayatakuwa na magonjwa tena. Lakini ili tuingie kwenye makao hayo mapya ni lazima tuzingatie aliyoyaagiza. Mojawapo ya maagizo yake ni hilo la kujitenga na unywaji wa pombe na ulevi
 
Hatukatai pombe ni mbaya.
Sio pombe tu. kuna sigara. utumiaji sa Sukar na wanga kupita kiasi nk nk.

Ila pia wapo wanaokunywa pombe na wamefikisha miaka 90. babu yangu amefariki akiwa na miaka 105.
Kila weekend lazima umkute bar bad alipofika miaka 80 ndio kaacha na alikuwa analetewa bia had kitandani.

Kila kitu ukitumia kistaarabu madhara yanapungua.

Narudia tena. kila kitu ukitumia kistaarabu madhara yanapungua au yanakuwa hayapo.
Unafikiri kwa unywaji wake huo, sasa hivi babu yako yuko wapi. Mbinguni au motoni?
 
Katika uislamu pombe ni haramu kabisa kunywa,kuuza,kusafirisha,kutengeneza,kuwauzia wengine,kupangisha nyumba yako,iuzwe pombe.Kwa hiyo Mtume Muhammad, aligundua ubaya wa Pombe,miaka
Karibia 1500 iliyopita,kabla hata wanasayansi wa sasa kugundua.
Safi kabisa.
Dini nyingi zinaonya kuhusu pombe, na hilo linaonesha kwamba uharibifu wa pombe uko wazi hata kwa macho ya kawaida. Biblia ilishatoa onyo hilo hata kabla ya karne ya 6 BK. Kwa mfano, zaidi ya miaka 3,000 iliyopita, Mfalme Sulemani aliandika:
Mit 20:1
"Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima."
 
Hata soda ni sumu so kila mtu achague sumu yake ajifie taratibu. Waiter Lete safari ya baridiiiiiiiii
Aisee, unashauri kila mtu achague sumu yake? Hapana, mie nimemchagua Yesu wangu — nipate uzima!

Haya, safiri salama, lakini nakutahadharisha: hiyo "Safari ya baridiii" inakupeleka kwenye "shimo lenye motooooo."
1 Kor 6:9-11

"Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi."
 
Aisee, unashauri kila mtu achague sumu yake? Hapana, mie nimemchagua Yesu wangu — nipate uzima!

Haya, safiri salama, lakini nakutahadharisha: hiyo "Safari ya baridiii" inakupeleka kwenye "shimo lenye motooooo."
1 Kor 6:9-11

"Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi."
Ndo ukufe na yesu wako, watakao kufa kwa sumu ya pombe na soda na wao watakuwa wamefanya uchaguzi wao. By the way kifo ni kifo tu who cares.
 
Hivi wanaouguza figo na ini ni walevi tu?
Ni kweli sio wote wanaouguza ini au figo ni walevi. Lakini pombe bado ni sababu kubwa ya magonjwa hayo, na mara nyingi huongeza hatari hata kwa asiye na tatizo. Biblia haitukatazi pombe kwa sababu ni chanzo pekee cha maradhi, bali kwa sababu ‘ina ufisadi’ (Waefeso 5:18), inaharibu maamuzi ya mtu, na kumtoa kwenye utakatifu wa kweli. Kwa hiyo, hoja sio magonjwa tu, ni kutunza hekalu la Mungu (1 Wakorintho 6:19–20). Right?
 
Mijagamaster kama kawa,mi seafoods,totoz kwa kwenda mbele,we usinywe na cha ajabu ukatangulia kufa kabla yangu.
Sawa. Uchaguzi ni wako, mkuu. Mimi nikifa kabla yako naenda kupumzika. Kama wewe kwa pombez hizo unafikiri utawakuta totoz jehanam, songa mbele, utaukumbuka uzi huu.
Babu yangu kafa mwaka juzi na miaka 123 na alikuwa mnywaji tena wa vitu vikali balaa
Duh, miaka 123 tu umeona mingi?
Urefu wa maisha sio kipimo cha haki au kibali mbele za Mungu. Methusela, ni mtu aliyeishi muda mrefu sana katika Biblia (miaka 969, soma Mwanzo 5:27), lakini Biblia haimtaji kama mwenye haki wala mfano wa kuiga.

Ukweli ni kwamba, Mungu huwapa watu rehema kwa sababu anawapenda hata wasiotii. Lakini mwisho wa maisha, ‘kila mmoja atasimama mbele ya kiti cha hukumu’ (Warumi 14:10). Kwa hiyo, tusijifunze kutoka kwenye urefu wa miaka ya huyo babuu, bali kutoka kwenye Neno la Mungu lisilokosea. Okay?
Hiyo sayansi yenu peleka kule,mbona imeshindwa tu kuzuia uzee achana na kuipata dawa ya ukimwi,fumbaf
Pole sana unataka usizeeke? Hilo haliwezekani. Mungu aliishasema kila mtu lazima afe. Na uzee ni ishara ya kuondoka duniani.
 
Mambo yapo wazi acha kurukaruka vifungu. Yohana alikula nzige na asali tu wakasema anapepo. Yesu anakula na kunywa wakasema mlafi na mlevi( maana alikuwa anatumia hicho kinywaji kinacho levya na kula misosi mbalimbali) na kushinda na makahaba na watoza ushuri( walioonekana wadhambi) ndio maana hakukanusha hayo. Mantiki yake ni kukemea unafiki. Wanataka awe kama Yohana ambaye nayeye walimshutumu anapepo.

Ukweli ni kwamba Yesu alikula, alikunywa mvinyo, alishinda na makahaba(M. Magdalene) na watoza ushuri (Akina zakayo). Na si kwamba walimsingizia ni fundisho mpya anatoa.

Usitumie pombe Kwa discipline yako binafsi ni nzuri. Ila si dhambi katu. Hiyo ni swala la self discipline tu.
Duh, kweli kama alivyosema Smart911 wanadamu siku hizi ni wabishi sana.

Ni kweli Yesu alikula na kunywa, na ni kweli alishinda na watoza ushuru na wanawake waliodhaniwa kuwa wenye dhambi. Lakini Yesu hakufanya hivyo ili afanane nao, bali awalete kwenye toba.

Mathayo 9:13
‘Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu.’

Yesu hakuwahi kulewa, wala kuhalalisha ulevi. Kuitwa ‘mlevi’ haimaanishi alikuwa mlevi. Hiyo ilikuwa ni kashfa ya wanafiki, kama walivyosema Yohana ana pepo (Mathayo 11:18-19). Yohana hakuwa na pepo. Tangu lini mtu mwenye pepo akabatiza watu?

Yesu hakuwa mlafi, hakuwa mlevi, hakuwa mchafu, bali mwenye rehema.
 
Duh, kweli kama alivyosema Smart911 wanadamu siku hizi ni wabishi sana.

Ni kweli Yesu alikula na kunywa, na ni kweli alishinda na watoza ushuru na wanawake waliodhaniwa kuwa wenye dhambi. Lakini Yesu hakufanya hivyo ili afanane nao, bali awalete kwenye toba.

Mathayo 9:13
‘Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu.’

Yesu hakuwahi kulewa, wala kuhalalisha ulevi. Kuitwa ‘mlevi’ haimaanishi alikuwa mlevi. Hiyo ilikuwa ni kashfa ya wanafiki, kama walivyosema Yohana ana pepo (Mathayo 11:18-19). Yohana hakuwa na pepo. Tangu lini mtu mwenye pepo akabatiza watu?

Yesu hakuwa mlafi, hakuwa mlevi, hakuwa mchafu, bali mwenye rehema.
Yesu hakuwa mlafi, hakuwa mlevi Wala hakutenda dhambi. Ila Yesu alikula, alikunywa mvinyo, alishinda na wenye dhambi.

Ulafi ni dhambi ila chakula si dhambi, Ulevi ni dhambi ila pombe si dhambi, Uzinzi ni dhambi ila mwanamke au mwanamke si dhambi. Elewa hii mantiki!!
 
Ulianza na Sayansi vizuri, ila ukaharibu ulipoaanza kutaja vifungu vya Kitabu na kuhusianisha na Mungu. Mm nimesoma mpk apo WHO 2023 There is no safe amount.......
Chagua kama ni sayansi au ni Mungu, tupe product moja.
Umenikera sana kiukweli kubadilisha mada feom science to God scripture
Samahani sana MoroGent kama mada imekukera. Lengo langu sio kuwakera watu bali kuwasaidia wasiende motoni. Ukweli ni huu: Sayansi na Biblia havipingani. Vyote vimekiri kwamba pombe ni sumu. WHO (2023) ilisema wazi: ‘There is no safe amount of alcohol use.’ Na Biblia ilitoa kauli kama hiyo miaka zaidi ya 3,000 iliyopita:

‘Usiutazame mvinyo… mwisho wake huuma kama nyoka’ (Methali 23:31–32).

Maandiko yanasema tena kwamba kwa vinywa vya mashahidi wawili kila neno litathibitika (2 Wakorintho 13:1)

Sasa kama sayansi inasema ‘ni hatari’ na Mungu anasema ‘ni ufisadi,’ sioni kosa kuchanganya sayansi na Maandiko, maana vyote vimepaza sauti moja: “Usinywe.”

Comment yako umeimalizia na Ki-english! Permit me, as well, with all due circumspection and intellectual candor, to pose a question whose necessity arises not from hostility but from theological curiosity and spiritual concern. Do you, in any sincere or confessional sense, identify yourself as a follower of Jesus Christ, one who stands within the historic and sacred communion of the Christian faith?

I ask this not as a matter of rhetorical maneuvering but in response to a discernible resistance, perhaps even a philosophical detachment, toward the authority and sanctity of the Holy Scriptures. Your tone, whether intentionally or not, conveys a subtle yet unmistakable aversion to the very texts upon which the entire edifice of Christian truth is constructed and sustained.

It is among the most foundational tenets of Christian orthodoxy that the Scriptures are not relics of antiquity nor cultural expressions of primitive religion. Rather, they are the living and active voice of the Eternal God. These writings are divinely inspired, profitable for teaching, rebuke, correction, and the training of the soul in righteousness. If Christ Himself affirmed them without hesitation and the apostles regarded them as the bedrock of all godly instruction, then by what logic can one who professes allegiance to Christ treat them with indifference or even disdain?

With the utmost reverence, I submit this for your reflection. Can anyone truly claim to follow Christ while rejecting the authority of the very Word He embodied and fulfilled? Such a posture does not merely present a theological contradiction; it reveals a deeper issue of estrangement from the voice of God. Perhaps the matter at hand is not intellectual discomfort, but a heart still unreconciled to the authority of divine revelation. Thank you.
 
Usibague... Waambie pia sausage na processed meat zingine nazo ni Group 1 carcinogens.

Nyama nyekundu(Beef, Pork, lamb n.k) hizi pia ni Group 2A carcinogens.

Kwahiyo kama unakula nyama ya Ng'ombe unaharibu hekalu la Mungu ndugu Setfree

Kiufupi hekalu la Mungu siyo Hilo tumbo, mkono Wala Tako lako unaloliona hapo. Sababu mwisho wake vyote vinakufa na kuzikwa au vinaweza kukatwa.

Hekalu Gani la Mungu linakufa na kuzikwa. Hekalu la Mungu halifi Wala haliwezi kukatika kipande😂
 
Namshukuru Mungu aliyenitoa huko miaka 28 iliyopita.
Kama ni hivyo WHO ingeagiza viwanda vinavyotengeneza bia duniani kuweka tangazo la ONYO kwenye chupa kama ilivyofanya kwenye Sigara(kama sikosei)!
Ili mtu akinywa,anywe kwa "his own risk"!
Kama watu hawaogopi ukimwi,sidhani kwa walevi hili litaingia akilini mwao.
 
Kinondoni pale makaburi ya walokole yapo mengi sana ,kifo ni kifo
 
Back
Top Bottom