Kwa kiasi fulani naweza kukubali kwamba yaliyopita si ndwele.
Lakini pia kinga na kinga ndipo moto uwakapo, na tena mtondoo haufi maji kama vile jungu kuu lisivyokosa ukoko.
Kwa hiyo kueleweshana ni ada.
Bila kujua yaliyopita, hata hayo yajayo kuganga itakuwa vigumu, watoto ambao hawajasoma Herodotus na Homer watafikiri watu weusi siku zote walikuwa wanyonge kwa weupe tu. Wakati Herodotus kaandika habari za majeshi ya Cambyses yalivyokula kichapo kikali mpaka ku retreat kutoka kwa healthy "Ethiopian" (the ancient name for black Africans) soldiers. Herodotus kaandika kwamba Ethiopians walikuwa warefu, wazuri na wanaishi maisha marefu kuliko sehemu yoyote.
Hakuna kujenga uelewa mzuri unaotazama mbele kwa kuzingatia usawa wa binadamu kama hatujaeleweshana kwamba hii hali ya unyonge tuliyonayo sasa imeanza relatively late na haikuwa hivi siku zote.
Vijana wakijua kwamba kuna wakati mtu mweusi alikuwa ni mtu mwingine tu dunia hii, si mtu wa chini kwa mwingine, labda wataweza kujua kwamba tunaweza kurudi hapo tena.
Kwa hiyo, kwa mtazamo huo, yaliyopita yanaweza kuwa na umuhimu hata kama tunajua kwamba hatuwezi kuishi kwenye past glory.