ndugu yangu, kwani hapo tunaongelea miaka ipi? usije kuwa unajadili miaka ya 1800 na 1900. tunaongelea kabla ya hapo. hatuwezi kusema waliondoka wote kabisa, ila ukweli ukienda Iran kwa mfano, wale waliohamishwaga miaka ileee ya kina Jeremia, shedrack meshack na abednego, kizazi kile, kipo hadi leo na kuna myahudi mmoja hadi alikuwa waziri huko iran miaka ya nyuma. hadi leo iran kuna wayahudi takriban 8000, zamani walikuwa maelfu ila walikimbia wote miaka ya 1900.
ukienda Iraq nako hivyo hivyo. walichukuliwa mateka sana enzi za kina Nebukadreza. jamii za kiyahudi zote hata ukienda israel wanajuana, ni sawa na sisi sote ni watanzania ila tunajuana huyu mtanzania wa Lindi, huyo wa bukoba n.k, na pale israel wanaongea lugha nyingi tu za kuzaliwa nazo. mojawapo ya jamii kubwa sana ya wayahudi walikimbilia na kusettle Yemen, hao wanaitwa wayahudi wa kiyemen, wapo wengi sana walikimbilia uyunani/ugiriki, wapo wengi sana walikimbilia uturuki na huko tangu enzi hizo ndiko alikozaliwa Paulo, paulo alikuwa mtu wa tarso huko uturuki. hata wakati wa Yesu alipopaa mitume walikuwa wakienda nchi kwa nchi wakihubiri kwenye masinagogi ya wayahudi, walishasettle huko.
ukienda israel leo kuna wayahudi, pamoja na kwamba wanaongea kiebrania, ila wanaongea kirusi, kiarabu, kiukraine, kiingereza, kijerumani, kipolishi, kifaransa n.k. mpaka mwaka wa 1900 idadi ya waarabu pale holy land ilikuwa kubwa mno kuizdi wayahudi ambao walisharudi kuungana na wachache sana ambao hawakupelekwa ukimbizini. huko kote walitawanyika walitawanyika kama wakimbizi waliokuwa wanakimbia persecution kutokana na dini yao. ila kufikia 1948 wayahudi walishafikia 600,000 na wakawazidi waarabu idadi.
hao wanaoitwa wapalestina, ni wahamiaji wa kiarabu waliovamia ardhi ya wayahudi baada ya kukimbilia ukimbizini. wengi ni wamisri, wajordan, lebadon, syria n.k. na hata sura zao zinajulikana hata kiongozi wa mmoja aliongea hapa juzi kwamba wapalestina ni wahamiaji toka mataifa hayo.
wanashindwa kufuta historia kwasababu hadi leo pale israel kuna kaburi la Daudi, Absalom , kisima cha yakobo na ushaidi mwingi unaoonyesha eneo lile ilikuwa falme ya wayahudi lakini baada ya kwenda ukimbizini waarabu wakavamia, wakapaita kwao.