Wife kanizidi kipato lakini kila wiki lazima aniombe elfu 20 ya kusukia

Wife kanizidi kipato lakini kila wiki lazima aniombe elfu 20 ya kusukia

Nmekumbuka nlikua demu wangu zamani anaenda kuchukua mshahara , anakuja na tax ananiambia nilipe hela ya tax
Uyo alikuwa hatupendi, ukitakujua mwanamke anakupenda utamuona kwenye matumiz ya pesa kama anazo pesa lazma atakupa na na kama haja kupenda huwez kula hata sent moja yke wanawake wana roho ngumu
 
Mpe pesa ya kusukia mkeo wewe! mbona hiyo ndogo kabisa?
 
Uyo alikuwa hatupendi, ukitakujua mwanamke anakupenda utamuona kwenye matumiz ya pesa kama anazo pesa lazma atakupa na na kama haja kupenda huwez kula hata sent moja yke wanawake wana roho ngumu
Hahahah nakubali, mwanamke akikupenda bana hela yake lazma utaila tu hawezi kuwa mgumu kabisa yani.
 
mkuu simama kama mwanaume kuwa mkali,.... umpangie matumizi ya angalau laki 7 ya huo mshahara wake akishindwa kutimiza majukumu wewe usiweke pesa nyumbani.....

mil 1.9 ni nyingi sana, na hapo ukute kuna house girl ambaye unamlipa wewe mshahara.....tuache unafiki hapa mkeo anaharibu na hii hali ni wewe tu unaweza igeuza.....

Kuingia ndoani na mbinafsi ni kujitafutia kesi na matatizo
Mie kazi yangu huwa ni kushauri tu...Mwanamke mbinafsi hafai jamani, hakawilii kuhesabia mambo aliokufanyia kwa pesa zake siku mkigombana😂😂😂
 
hahaha ni kweli mkuu ila kuacha mil 1.9 afanyie anasa ni uzembe....week hili kwangu angekuwa mama wa nyumbani rasmi.
Mie kazi yangu huwa ni kushauri tu...Mwanamke mbinafsi hafai jamani, hakawilii kuhesabia mambo aliokufanyia kwa pesa zake siku mkigombana[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ndio best yangu....ila ngoja nikufundishe kitu, ukitaka kuoa, oa mwanamke unayempenda sana moyoni mwako!

Masuala ya kazi yake achana nayo kabisa, coz umeoa mwanamke hujaoa kazi,

Ukitaka mwanamke akudharau ulizia hela zake! Hela ya mwanamke hainaga thamani coz ya mashindano ya kununua nguo, les wigi, vipodozi, viatu, pochi, dhahabu n.k...vyote hivyo vinammalizia hela!

Mmoja mmoja ndo anaweza akaamua kujenga/ kufanya maendeleo na ni mpaka ashinde vita ya mashindano ya kuvaa job na wanawake wenzie...

Mwisho kabisa, amini hili

Mwanamke ni kiumbe ambae sio provider kabisa, so ukimuuliza hela zake, asee anakuwa anaona na we ni mwenzie
Hahahah hao wanawake wapumbavu mnawatoaga wapi. Nashukuru nimepata mwanamke aliyekulia kijijini japo kwao hawana njaa kabisa ila amekulia mahala ambapo anajua life ni nini.

Ni mtu ambaye ukimpa mipango yupo tayari ku contribute chochote kitu. Hata kukopa ili mfanikishe yani mpenda maendeleo na wala hayo mambo ya mawigi na kununua nguo kila week hana tamaa nayo.
 
hahaha ni kweli mkuu ila kuacha mil 1.9 afanyie anasa ni uzembe....week hili kwangu angekuwa mama wa nyumbani rasmi.
Mie wangu angekuwa na huo mshahara tungekuwa tushaongeza kiwanja kingine na biashara kubwa tu. Anapenda sana maendeleo sio huo ujinga wa mawigi na nguo. She is willing to give out what she has nikitaka namwambia tu and there are no issues.
 
Yap! Kige
Huyo hakupendi. Mwanamke anayekupenda lazima atakusaidia na kukuhurumia. Huyo Hana huruma nanwewe kuwa makini mkuu .
zo cha mwanamke kupenda anakuwaga na hali ya huruma sana juu yako usiteseke.
 
Kama wajibu wangu YEYE ANAFANYA KAZI ILI IWEJE ?! NDO MAANA NILIAPA NA SIJAOA MWANAMKE MWENYE AJIRA.

Ni mibinafsi, mibishi, kiburi, ujuaji pumbavu kabisa. Mke bora ni MAMA WA NYUMBANI NA KUMUHUDUMIA INALETA RAHA hata akitaka million nitampa sio hii mifeminist kmlammzao
Hahahaha mkuu yalishakukuta nini?
 
Habari wakuu.

Mke wangu ni muajiriwa kwenye moja ya entities hapa tz.kipato chake kwa mwezi ni around 1.9m baada ya makato yote ya serikali.

Mimi kipato changu ni around 500k kwa mwezi na kikweli kama mwanaume najitahidi sana pamoja na kipato changu kidogo kuhudumia familia yangu vizuri

Sasa kilichonifanya kuandika huu uzi ni kisa kilichotokea juzi jumamosi, wife ameninunia sababu ikiwa kwamba aliniomba pesa ya kusukia kama 20k hivi nikamwambia sina, nikamwambia yeye anakosaje hiyo elfu 20 wakati mahitaji yote ya nyumbani natoa mimi. Kanuna mpaka leo.

Nimeambatanisha ushahidi wa salary yake hapa.nishaurini, huyu mwanamke yuko sahihi kuniomba ela ya kusukia wakati kanizidi kipato karibia mara 4?View attachment 1691695
Hao ndivyo walivyo kyanyangwe . Mimi wakwangu nilimfungulia biashara na siingilii hiyo biashara . Kwa kifupi ni ya kwake. Majuzi hapa nimewalipia watoto karo mpaka nikaishiwa akiba ndani. Nikamuomba a ngalau atubebe kwa kugharimia mahitaji ndani kwa mwezi moja nijiweke sawa . Lakini ndani ya siku mbili niliombwa mahitaji ya ndani. Daahh

Kwa kifupi hao ni kama muungano wa Tanganyika na Zanzibar. (Cha kwako ni chetu lakini cha kwangu ni cha kwangu)

Odhis *
 
pesa ya mwanaamkee haina matumizi so tafutapesa mpee mkeo kabla atujaanza mpaaa
 
Yuko sahihi 100% unapo amua kuoa ujue kabisa unaingia kwenye jukumu la kuitunza familia yako familia yenu familia ya mke wako na mkeo umtunze yani iyo ni lazima sasa kama ulioa mwanamke mwenye kipato ukategemea akusaidie umejidanganya mzee we komaa tuu muhudumie mkeo....acha kulalamika si ulimpenda mwenyewe...
 
Back
Top Bottom