Tetesi: Wiki ijayo nchi kutikisika, mtu mkubwa sana kukihama Chama cha Mapinduzi

Tetesi: Wiki ijayo nchi kutikisika, mtu mkubwa sana kukihama Chama cha Mapinduzi

Habari zilizotufikia hivi punde

Kuna kiongozi moja aliyewai kushika nyazifa za juu kabisa kwenye chama na nchi anakihama chama cha mapinduzi CCM kwa kutoridhika na uongozi na nchi inavyokwenda kwa sasa kwa habari zaidi nitaendelea kuzileta hapa

Mwanahabari Huru
Mwambie Wanaccm tunamtakia kila la heri[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
Jana nilimuona A Town na MH.LEMA nikajiuliza na nikamuliza Mh lema vipi huyu kiongozi wa ccm anatafuta nini lema kanikonyeza na kusema kamanda kaja kujisajili.



Swissme
Nobody ever leaves the KGB..Hii kauli nimeikumbuka kwenye zile muvi zetu za wahenga.
Poor maandazi!
 
Mh, atakua Dr. Shika ndo anahama....
Si bure, hapa kuna namna
 
Wakija kwenu mnashangilia kweli kweli, wakianza kurudi walikotoka mnalalamika kuwa kuna mpango wa kuuwa upinzani. Siasa za bongo ukiwa mtazamaji ni burudani tosha.
Kweli kiongozi ngoja tubakie jukwaani tushuhudie mtanange live bila chenga.
 
Watu mmekuwa akina mfalme njozi, kazi kutoa tabiri za watu kuhama vyama, tunangojea kutimia kwa hizo tabiri zenu za kwamba Nyani yule anakaribia kumega embe bichi na kulitupa chini wakati kikweli nyani hali embe bichi
 
Habari zilizotufikia hivi punde

Kuna kiongozi moja aliyewai kushika nyazifa za juu kabisa kwenye chama na nchi anakihama chama cha mapinduzi CCM kwa kutoridhika na uongozi na nchi inavyokwenda kwa sasa kwa habari zaidi nitaendelea kuzileta hapa

Mwanahabari Huru
Poa, huyu hajanunuliwa kweli??
Sioni mkongwe wa sisiemu zaidi ya kikwete, mkapa, kinana kuhama sisiemu na kuleta mtikisiko, wa kuhama na kuleta mtikisiko ni vijana kina Nchemba, Makamba, Kigwa, etc!! Wengine wakihama hawatakuwa na impact yoyote.
 
Mmeanza kununua?kwi kwi kwi...!!

CCM hamna mtu mkubwa wote ni sawa mbele ya Jicho la chama.

By the way hakuna muadilifu anayeweza kuhama CCM bali fisadi tu...
Hivi kale kawimbo unakakumbuka mkuu?tuna imaniiiiiiii na ..................?
 
Nchi kutikisika[emoji23][emoji23][emoji23]
Wanasiasa mnapenda kiki sana. Nchi haitatikisika kwa kiki za watu na tutaendelea na kazi zetu kama kawaida na mwenye njaa atabaki na njaa endeleeni kuhamahama vyama kila mtu apate sehemu atakayokula vizuri.
Tusio wanasiasa tunawatakia kila la heri na kazi njema
"Siasa ni Ajira"
 
Kama sio Membe au Mwandosya sijui...

Membe siyo rahisi kwenda chadema kuna sababu nyingi tu ambazo ziko wazi, inatumika nguvu kubwa tu kumchonganisha na rais.

Mwandosya naye naweza kusema siyo kweli kama alishindwa kuhama kipindi kile anazindua kitabu chake ushawishi ulikuwa ni mkubwa sana kwake, na walijaribu sana lakini aligoma kabisa kuhama.

CHADEMA kuondokewa na hawa vijana wake hasa yule mwenyekiti wa Bavicha taifa imewapa wakati mgumu sana hivyo wanatumia nguvu nyingi sana kujitanabaisha kwa jamii kwamba bado wanamvuto.

Tangu chama kiuzwe kwa yule mzee watu wake wamekuwa kama mtu asiye mjuvi wa kuogelea.
 
Back
Top Bottom