Wiki sasa sina amani

Hapo ndio tunapima upendo wa kweli sasa kama ulimpenda kwa shida na raha ishi nae tu, ila kama utamuacha basi hukumpenda kweli
 
Huyu tayar amechanganyikiwa, brother Ili ujue Kama umepata maambukizi ni lazima ufanye vipimo.

Kuwa poa haimaanishi hujaambukizwa, kuwa mpole.

Pia una uhakika gani Kama alikuwa anatumia dawa vizuri wakati unasema ulimfumania siku moja Kwa Siri?
Relax
 
yaani viral load ni kiasi cha virusi kwenye damu

kama muathirika akitumia ARVs vizuri basi kile kiasi kinapungua na uwezo wa kumuambukiza mtu unakuwa mdogo

hii ni kwa uelewa wangu DR Mambo Jambo anajua kiundani
Ni kweli kabisa!

Cha kwanza, kabla ya Vyote anatakiwa Kuvunja ukimya kwa Upole amuulize mwenzake kwa ukimya sana Bila kuonyesha Hasira, Kukwazwa wala kuwa Disappointed, Na kuonyesha kwamba Hajali hali yake Kama ni muathirika au Lah na kumuambia amuambie Ukweli, naumuapie kabisa kama kwa vyovyote atakavyokuwa hali yake ataendelea kumpenda na hatamuacha...

Nina Uhakika kwa 100% lazima atamuambia Ukweli...

Pili, Kwa wagonjwa wanaotumia dawa kila muda fulani huwa wanachukuliwa Damu kwa ajili ya kipimo cha RNA PCR kwa ajili ya Kuangalia HVL (HIV viral Load) yaani wingi wa Virusi ndani ya Damu..
Kama itatokea Akawa na Idadi ndogo sana ya Virusi kwenye Damu,Mara Nyingi HVL ikisoma TND (Target Not Detected)..

Uwezo wa mtu huyo kumuambukiza Mwingine huwa Ni mdogo sana yaani ni chini ya 1%
Kwahyo kama anatumia Dawa Vizuri na Amepima HVL majibu ni TND asiwe na hofu kabisa
 
Huyo aliyekuficha kwa makusudi na hali anajua afya yake nenda kamshitaki.
Lakini Mwenyezi Mungu ametufunza tuache zinaa ndugu zangu.
 
Mkuu unayemshauri sidhani hata miaka 30 kafikisha na Yeye alikuwa anavimba humu anamiliki Lishangazi aasa sijui ilikuwa ni kweli au anatuchangamsha tu?
Mkuu mbona kama unanisagia kunguni sasa
 
Haya mbona yalisha pita mkuu.ujana maji ya moto elewa
 
Acha tuu
 
Acha kuwadanganya watu humu yaani uzi mzima usiulize dalili za ukimwi zinaanza kuonekana baada ya muda gani maana ndio kitu cha kwanza mtu akipitia hali huanza kuuliza mara kwa mara.
Daaah niulize dalili... !!
Nilichouliza ni muhimu kuliko hizo dalili mkuu.

Nauliza kupata uhakika tu before that nimesoma nyuzi nyingi za UKIMWI..

Mkuu katika nchi yetu huu ugonjwa tunaanza kufundishwa toka primary level

Primary darasa la 4 , la 5 na la 7
Secondary form 1, form 2 na 4
Advance kama umesoma bios hii utagusa tu kwenye virus pale.

Hata kama hutosoma bios pia utaikuta kwenye GS kama sub topic..

Ukija chuo pia unasoma kwenye development study....

Bado unataka niulize kuhusu dalili....?
 
Hapo ndio tunapima upendo wa kweli sasa kama ulimpenda kwa shida na raha ishi nae tu, ila kama utamuacha basi hukumpenda kweli
Kuna kitu ujaelewa...!!?

Kama mtu anakuficha kitu huo ni upendo...
Au unazungumzia upendo gani
 
Breki za katuni msala kaka. Dah
 
Mkuu, suala muhimu hapa ni kupima tu. Kuna watu imewahi kuwatokea hali kama hii pia na kwa bahati nzuri wakakutwa sawa. So bila kupima hutojua pa kuanzia. Jikaze upime au mkomalie akueleze vizuri kuhusu hivyo vidonge na hata ikibidi mtishe kuwa unaviulizia matumizi yake kwa wafamasia au madaktari.

Japo mwishoni hata akikueleza ukweli na wewe ukaujua ni wazi kupima hakukwepeki. Kapime na umuache mkuu.
 
Daaah mkuu jibu kama hili nimesubiri sana kwa mda mrefu...

Je unazani hapa kuna haja ya kupima ?
Je niendelee nae au ..?
We pima kujiridhisha sababu hata mngetoka wote kwenda nae pima, majibu yangekuwa negative wote ijapokuwa yeye positive

Sababu anatumia dawa tayari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…