Wiki sasa sina amani

Wiki sasa sina amani

Hapo ndio tunapima upendo wa kweli sasa kama ulimpenda kwa shida na raha ishi nae tu, ila kama utamuacha basi hukumpenda kweli
 
Huyu tayar amechanganyikiwa, brother Ili ujue Kama umepata maambukizi ni lazima ufanye vipimo.

Kuwa poa haimaanishi hujaambukizwa, kuwa mpole.

Pia una uhakika gani Kama alikuwa anatumia dawa vizuri wakati unasema ulimfumania siku moja Kwa Siri?
Relax
 
yaani viral load ni kiasi cha virusi kwenye damu

kama muathirika akitumia ARVs vizuri basi kile kiasi kinapungua na uwezo wa kumuambukiza mtu unakuwa mdogo

hii ni kwa uelewa wangu DR Mambo Jambo anajua kiundani
Ni kweli kabisa!

Cha kwanza, kabla ya Vyote anatakiwa Kuvunja ukimya kwa Upole amuulize mwenzake kwa ukimya sana Bila kuonyesha Hasira, Kukwazwa wala kuwa Disappointed, Na kuonyesha kwamba Hajali hali yake Kama ni muathirika au Lah na kumuambia amuambie Ukweli, naumuapie kabisa kama kwa vyovyote atakavyokuwa hali yake ataendelea kumpenda na hatamuacha...

Nina Uhakika kwa 100% lazima atamuambia Ukweli...

Pili, Kwa wagonjwa wanaotumia dawa kila muda fulani huwa wanachukuliwa Damu kwa ajili ya kipimo cha RNA PCR kwa ajili ya Kuangalia HVL (HIV viral Load) yaani wingi wa Virusi ndani ya Damu..
Kama itatokea Akawa na Idadi ndogo sana ya Virusi kwenye Damu,Mara Nyingi HVL ikisoma TND (Target Not Detected)..

Uwezo wa mtu huyo kumuambukiza Mwingine huwa Ni mdogo sana yaani ni chini ya 1%
Kwahyo kama anatumia Dawa Vizuri na Amepima HVL majibu ni TND asiwe na hofu kabisa
 
Habari za muda huu ndugu zangu,

Wakuu nina week sasa nimekuwa na hali ya unyonge tangu nikutane na kopo la vidonge kwenye droo la huyu mwenzangu.

Hali ambayo imenistua zaidi hivi vidonge nina asilimia mia ni vya HIV.

Kuna siku nilimfuma anakunywa kwa siri nikauliza akasema ni dawa za vidonda vya tumbo..

Wakuu nina wasi wasi sana maana hata ishu ya kupima yeye ndio alifosi mimi nikapime nimletee majibu.

Baada ya kusema hivo nikajiwekea asilimia mia kua yeye yupo salama..

Ila mpaka sasa nimekua na wasi wasi mno.

Nataka kujua yafuatayo wakuu wenye experience hivi mtu anayetumia dawa vizuri kabisa ni kweli hawezi kuambukiza au ni story za vijiweni...?

Na ile ya kusema kuna watu hawapati virusi ni kweli au ? maana mpaka sasa naona nipo poa kabisa...

Wakuu ni week sasa hata hamu ya kula chakula cha usiku sina mpaka ananistukia sasa...

Najuta.... Kitu kinachoitwa kupima kwa sasa HAPANA
Huyo aliyekuficha kwa makusudi na hali anajua afya yake nenda kamshitaki.
Lakini Mwenyezi Mungu ametufunza tuache zinaa ndugu zangu.
 
Mkuu unayemshauri sidhani hata miaka 30 kafikisha na Yeye alikuwa anavimba humu anamiliki Lishangazi aasa sijui ilikuwa ni kweli au anatuchangamsha tu?
Mkuu mbona kama unanisagia kunguni sasa
 
Shida ilianzia hapa Sasa ni muda wa kula matunda uliyoyapanda😂
"
Wewe shangazi kwa pigo zako. Kila mtu atakung'ang'ania.

Sio kwa kuchukua moyo wangu na kuuteka hivi.

Uliponiroga karoga tena maana nainjoi umefanya mpaka nisahau kilichonileta hapa jijini dasalam.

Nakuachaje kwa mfano. Kwa hizi starehe.... 😋😋😋😋😋"
Haya mbona yalisha pita mkuu.ujana maji ya moto elewa
 
Ndoa bwana. Unaishi na mtu ila moyoni una siri nyingi kiasi unajiona haupo salama, inafika mahali unaanza kuishi kwa matumaini na kujifariji kwamba ipo siku utakuja kuishi bila ya huyo... Nyie ndoa ikikosa kibali machoni pa Mungu ni mateso mazito hujapata ona zaidi utayaona ukiwa tyr umeyavagaa

Nyie nyie nyie
Acha tuu
 
Acha kuwadanganya watu humu yaani uzi mzima usiulize dalili za ukimwi zinaanza kuonekana baada ya muda gani maana ndio kitu cha kwanza mtu akipitia hali huanza kuuliza mara kwa mara.
Daaah niulize dalili... !!
Nilichouliza ni muhimu kuliko hizo dalili mkuu.

Nauliza kupata uhakika tu before that nimesoma nyuzi nyingi za UKIMWI..

Mkuu katika nchi yetu huu ugonjwa tunaanza kufundishwa toka primary level

Primary darasa la 4 , la 5 na la 7
Secondary form 1, form 2 na 4
Advance kama umesoma bios hii utagusa tu kwenye virus pale.

Hata kama hutosoma bios pia utaikuta kwenye GS kama sub topic..

Ukija chuo pia unasoma kwenye development study....

Bado unataka niulize kuhusu dalili....?
 
Hapo ndio tunapima upendo wa kweli sasa kama ulimpenda kwa shida na raha ishi nae tu, ila kama utamuacha basi hukumpenda kweli
Kuna kitu ujaelewa...!!?

Kama mtu anakuficha kitu huo ni upendo...
Au unazungumzia upendo gani
 
Umenikumbusha Kuna dada mmoja muuza uji mtaani nilikua namzimia kinoma sasa mi siyo mpenzi wa uji lakini nikaanza tabia ya kunywa uji kila siku siku moja nimempa hela nimesimama nae karibu akafungua pochi yake ili anipe chenji eeh bana wee si nikaona kikopo cha ARV
Nilipiga zile breki za katuni
Breki za katuni msala kaka. Dah
 
Mkuu, suala muhimu hapa ni kupima tu. Kuna watu imewahi kuwatokea hali kama hii pia na kwa bahati nzuri wakakutwa sawa. So bila kupima hutojua pa kuanzia. Jikaze upime au mkomalie akueleze vizuri kuhusu hivyo vidonge na hata ikibidi mtishe kuwa unaviulizia matumizi yake kwa wafamasia au madaktari.

Japo mwishoni hata akikueleza ukweli na wewe ukaujua ni wazi kupima hakukwepeki. Kapime na umuache mkuu.
 
Daaah mkuu jibu kama hili nimesubiri sana kwa mda mrefu...

Je unazani hapa kuna haja ya kupima ?
Je niendelee nae au ..?
We pima kujiridhisha sababu hata mngetoka wote kwenda nae pima, majibu yangekuwa negative wote ijapokuwa yeye positive

Sababu anatumia dawa tayari
 
Back
Top Bottom