KERO Wiki tatu bila maji: Wananchi wa Unyinga, Mamise na Unyakumi tunataka ufafanuzi kutoka SUWASA

KERO Wiki tatu bila maji: Wananchi wa Unyinga, Mamise na Unyakumi tunataka ufafanuzi kutoka SUWASA

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tunapenda kufichua kero kubwa inayowakabili wananchi wa maeneo ya Unyinga, Mamise na Unyakumi na maeneo mengine mjini Singida kutokana na ukosefu wa huduma ya maji takribani wiki tatu sasa

Kwa kipindi cha hivi karibuni, maeneo haya yamekuwa yakikumbwa na ukosefu wa maji kwa siku nyingi mfululizo. Jambo linalosikitisha zaidi ni kwamba mamlaka husika ya maji (SUWASA) haijatoa taarifa rasmi kueleza chanzo cha tatizo, muda wa kurejea kwa huduma, wala hatua zinazochukuliwa kutatua changamoto hiyo.

Wananchi wanapowasiliana na SUWASA kwa njia ya simu huambiwa kuwa kuna mgao wa maji, lakini hakuna maelezo ya kina kuhusu sababu za mgao huo, lini utaisha, au ratiba rasmi ya upatikanaji wa maji. Mara nyingi wananchi hupewa taarifa kuwa maji yatapatikana baada ya siku tatu, lakini hata baada ya wiki nzima kupita huduma hiyo hairejei

Kutokana na hali hii, wananchi wanalazimika kutumia gharama kubwa kununua maji au kutafuta maji kutoka maeneo ya mbali, jambo ambalo linaathiri maisha ya kila siku, usafi wa mazingira na shughuli za kiuchumi.

Tunaomba SUWASA na mamlaka husika kutoa maelezo ya wazi kwa wananchi kuhusu:
  • Chanzo halisi cha tatizo la maji katika maeneo haya.
  • Sababu za mgao unaodaiwa kuwepo.
  • Ratiba rasmi ya upatikanaji wa maji.
  • Muda wa uhakika wa kurejesha huduma ya maji katika hali ya kawaida.
Wananchi wa Unyinga, Mamise na Unyakumi na maeneo mengine wanastahili kupata taarifa sahihi na huduma bora ya maji kama haki yao ya msingi.
 
Si walisema wamechimba kisima kingine huko mwankoko chenye maji mengi kuliko cha mwanzo na kina uwezo mkubwa wa kuhudumia eneo kubwa la mji, sasa imekuaje maji yaadimike hivyo?
 
Back
Top Bottom