Will a weakened America emerge victorious against communist China?

Bro Boeing imewekeza uchina??
 
Bro Boeing imewekeza uchina??
Ndiyo braza, wamefungua plant yao huko.
 
Hata ukiingia 5star huwez ikuta zaid ya cnn
 
Hudhani kwamba hii ni faida kwa Uchina hasa kwenye kumpunguzia gharama za uzalishaji, upatikanaji wa huduma bora kwa bei rahisi pamoja na kuongeza nguvu yake kijeshi. Au mpaka maisha yawe ya gharama kama Tokyo ndiyo tusema kwamba taifa ni tajiri ???
Juzi usiku nilisoma taarifa moja kuhusu online chains za vyakula. China na watu wake wote inahitaji uzalishaji mkubwa wa chakula ila ni sera ya serikali kuhakikisha wanajitoshelesha kwenye chakula. Serikali ya China iko vizuri sana kwenye kutoa incentives kwa raia.

Kwa vile hili soko ni jipya, giants kama Tencent na Alibaba wanapambana kujitanua uko.

Sasa kilichonishtua ni kusoma kwamba ndani ya miaka hii 10, wages na salaries za mashambani vijijini zimepanda ×3! Kwa rate hii miaka 20 ijayo sijui kama kutakuwa na cheap labour tunayoiona leo. Wamefikia hatua ya kufunga automated bracelets kwenye kila kuku ili kumfatilia. Hapa wanakwepa gharama za wafanyakazi na wanaongeza usahihi wa taarifa. Unakuta shamba la kuku 20,000 kila mmoja amevaa kidani cha electronic.

Gharama za kuzalisha zinapanda taratibu, kitakachoibeba China ni sera za kukaribisha uwekezaji ambazo ni nzuri sana kuliko Marekani yenye makodi makubwa na ukaguzi mwingi. Kwenye miundombinu na nishati wako sawa.

Wasiwasi wangu ni kuona giants wa tech wanawekeza kwenye kulima matunda na kufuga kuku, I think hawajiamini kushindana katika soko la teknolojia pekee. Itakuwa maajabu kuona Intel inaanzisha mradi wa kufuga ng'ombe au Apple inapambana kusaidia walima nganongano, kuna makampuni ya kufanya hizi kazi.
 

Fact check : Umekosea kusema kwamba USD haitishiwi na Gold mind you it is that any fiat currency you know (USD included) it is an artificial Gold
 
You are right my friend, this is indeed a predicament for China: But the good thing is that China can also export her capital to Latin America or the African continent where there's abundant cheap labor, natural resources and a vast market for her finished goods. How do you see this ???

Mkuu T14 Armata you are too calm, observant and versatile: And for this you have my deepest respect !!!
Please keep up this good vibe,......
 
Fact check : Umekosea kusema kwamba USD haitishiwi na Gold mind you it is that any fiat currency you know (USD included) it is an artificial Gold
Mkuu hujadadavua vizuri: Fiat Money ina faida au hasara kwa uchumi wa Marekani ???
 
Kuhusu kuhamisha mtaji hii hatua bado sana kwa sasa.
China ina miundombinu mizuri sana na nishati ya uhakika kuliko nchi nyingine ambazo ni possible candidates. Kama zingekuwepo makampuni ya Marekani yangehama China kwa vile sera za US juu ya China zinasumbua baadhi ya biashara.

China ina watu wengi sana wenye elimu. Human capital yake ni educated na wana nidhamu ya kazi kama ilivyo kwa Japan. Afrika wengi ni wajinga and not suitable for large scale industrial output. Latin America nchi kama Mexico na Brazil bado hazijafikia kuwa mbadala wa China. Vietnam nayo bado, ingekuwa ni jimbo la China ingekuwa ya 13 kiuchumi.

Sasa kwa vile China ni kubwa na ina watu wengi bado. Haiwezi hamisha uzalishaji kwenda kwingine, itakuja uku kutafuta malighafi na uwekezaji wake mwingi ukifatilia ndio huu. Inawekeza kwenye bandari ili isafirishe malighafi zake na kuleta bidhaa zake, inawekeza kwenye uchimbaji. Hizo elimu na afya ni ufadhiri wala sio uwekezaji, hata Norway wanatupatia.

Pia kwenye soko. Sisi hapa Afrika tunanunua takataka nyingi kutoka China ambazo hazina thamani kubwa, Latin America nayo sio sana. Exchange baina ya US na China au US na Europe ni kubwa sana. Kuwekeza nchi maskini utakosa advantage ya kuuza kwa soko la ndani, mfano iPhone zinatengenezwa China na pia zina soko kuu uko.

Ikitokea China ikafikia level sawa za mazingira ya kazi ya Ulaya Mashariki bidhaa zake zitapanda bei. Njia rahisi ni kutumia AI na robotics kwenye production kuliko kuwekeza kwingine.

NB: Hapo mwisho mimi mwenyewe nakukubali sana humu ila umebadilisha avatar.
Napata shida kwenda na speed ya thread, sometimes napata interruptions kama sasa nimeitwa kufanya group discussion.
 
Nikufahamishe tu kuwa, hii imekuwa ni tabia ya Wamarekani kwa miaka mingi for some reason! Miaka ya 80 hadi 90, wanahabari na vyombo vya habari kwa ujumla vilikuwa vikiitangaza Japan wakati fulani katika namna ifananayo na hii ambayo vinaitangaza China hivi sasa.

By the way, kinachozungumziwa hapo ni Purchasing Power Parity. Hicho ni kipimo kimoja tu cha uchumi. Si sahihi kukitumia kama kigezo pekee cha nchi kuwa na uchumi mkubwa kuliko nchi nyingine. Unapotumia PPP kama kigezo pekee cha nchi kuwa na uchumi mkubwa kuliko nchi nyingine, unaweza kuulizwa swali: je, Nigeria ina uchumi mkubwa kuliko Sweden sababu tu ina PPP kubwa kuliko Sweden?

Hali ya kimaisha nchini Nigeria inaweza kuwawezesha kufanya manunuzi makubwa ya fungu la bidhaa kuliko Sweden kwa kiasi cha fedha kinachofanana. Let's say, nchini Nigeria, kwa dola 100 unaweza kununua pair 6 za viatu, lakini kwa dola 100 hizohizo ukiwa Sweden, unaweza kujikuta unanunua pair 2 pekee. Maana yake ni kuwa nchini Nigeria, pesa yake ya ndani ina higher purchasing power kuliko pesa ya Sweden nchini Sweden. Lakini, vipi kuhusu ubora wa viatu hivyo na kiwango cha matumizi ya bidhaa hiyo ukilinganisha nchi hizo mbili? Pia, vipi kuhusu ubora wa maisha na vipato vya raia kati ya nchi hizo mbili? Vipi kuhusu mapato yanayoingizwa kwa mwaka kitaifa kati ya nchi hizo mbili?
 
Kwanza kabisa, nimeshangazwa na ombi lako kuhusu andiko la Huntington la miaka ya 50 ambalo limezungumzia "decline of America". Nimeshangazwa kwa sababu sijapata kufahamu sababu juu ya ombi hilo. Je, ni kwa sababu hautaki kukubaliana na hoja yangu kwamba mjadala huu na mingine ya namna hii imekwisha jadiliwa toka miaka ya 50 ama ni kwa sababu nyingine tofauti?

Huntington, kwa maneno yake mwenyewe na katika maandiko na machapisho yake (kama umemfuatilia kwa makini) ameeleza kuhusu chimbuko la huo mjadala wa "decline of America". Kama umemfuatilia kwa makini, amezungumza kwamba alikuwa akiufuatilia huo mjadala tangu miaka ya 50 mwishoni na aliushuhudia huo mjadala ukishamiri katika vipindi tofauti-tofauti ama kwa lugha nyingine "waves". Wave ya kwanza ni kipindi ambacho USSR ilifanikiwa kurusha satellite ya Sputnik 1 mwaka 1957. Mafanikio ya USSR ya Sputnik 1 yaliamsha mjadala kwamba Marekani inaelekea kwenye "decline" na kwamba tayari kuna uwezekano kuwa imekwisha achwa nyuma na USSR katika masuala mbalimbali ambayo yamekuwa yakiiwezesha Marekani kuwa taifa lenye nguvu zaidi duniani. Hiyo ni miaka ya 50 mwishoni.

Kipindi kingine maarufu kilicho shamirisha mjadala huo ni miaka ya 70 mwishoni. Mafanikio ya kiuchumi ya Japan yalipelekea kuamsha mjadala wa namna hiyohiyo nchini Marekani kwamba uchumi wa Marekani inakabiliwa na tishio la ukuaji na Japan inakaribia kuizidi Marekani na huenda imekwisha izidi katika masuala mbalimbali muhimu ya kiuchumi. Pia, ukisoma machapisho ya karne hii ama ya hivi karibuni kuhusiana na hoja hii ya "decline of America", wasomi mbalimbali wanadai kuwa Marekani ipo katika "wave ya 5 ya declinism", na wanafuatisha trend ileile ya kina Huntington ya kuanzia miaka ya 50 mwishoni kuanzia USSR na Sputnik 1, kuelekea Vietnam war, kisha Japan, Ulaya na mpaka hivi sasa, China.

Tuendelee na mjadala!

Umetoa hoja kwamba tuachane na makisio na tuzitumie data zilizopo. Kwanza kabisa, hizo data unazozisema ndizo ambazo zimekuwa zikitumika kufanya makadirio au makisio mbalimbali ya kiuchumi ambayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara. Wataalamu wa masuala ya kiuchumi hutoa makadirio ya ukuaji wa uchumi kwa kuhusisha taarifa mbalimbali zilizopo za kiuchumi kutoka katika mashirika mbalimbali hususani haya tunayoyafahamu sana. Kuna taarifa kuhusu mapato ya nchi na uzalishaji katika kipindi cha muda maalumu, mapato ya raia kutokana na mapato ya nchi zao (per capita income), taarifa za ukuaji wa kiuchumi (GDP growth), na masuala mengineyo.

Hebu sasa tuangazie hizo data za kiuchumi. Nitauzungumzia uchumi wa Marekani kwa data za kiuchumi za hivi sasa ili ku-justify hoja yangu ya awali kuwa China bado haijaizidi Marekani kiuchumi. Fuatana nami!

1) Nominal GDP. Pato la taifa kwa mwaka. Mashirika mbalimbali duniani hasa yale tunayoyafahamu kama vile IMF, World Bank pamoja na UN yanatuambia kwamba, Marekani ni nchi yenye uchumi mkubwa zaidi duniani kwa kipimo cha nominal GDP ikifuatiwa na China. Kuna haja ya kuziweka takwimu hapa?

2) Net wealth ama national net worth. Thamani ya mali zote za nchi ukitoa madeni (assets minus liabilities), ikiwemo thamani ya mali zinazomilikiwa na raia wote kwa ujumla. Marekani ni kinara katika hili pia kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kiuchumi.

3) GDP per capita. Pato la raia kutokana na pato la taifa zima kwa mwaka. Marekani inafanya vizuri zaidi hapa ukiilinganisha na China. Kulingana na data za hivi karibuni za kina IMF, WB na wenzake, Marekani imeorodheshwa katika nafasi kumi za juu ikishindana na nchi za Scandinavia, Luxembourg, Qatar n.k.

4) GDP per capita (PPP). Pato la raia katika kipimo cha Purchasing Power Parity kutokana na thamani ya bidhaa zote na huduma zinazozalishwa kwa mwaka. Pia, Marekani inafanya vizuri zaidi kuliko China kulingana na data zilizopo za hivi karibuni.

Sambamba na masuala hayo, kuna vipimo vingine ambavyo hutumiwa na wataalamu wa masuala ya uchumi kuonesha uwezo wa kiuchumi wa nchi kwa kuzingatia masuala mbalimbali muhimu. Kuna vipimo vya uchumi kama vile: Ease of Doing Business Index, Indices of Economic Freedom, Global Competitiveness Index n.k.

Ease of Doing Business Index. Hutumika kuonesha, pia kulinganisha nchi zenye urahisi katika kufanya shughuli za kiuchumi ama kibiashara. Hapa kuna masuala ya masharti rafiki ama rahisi ya kibiashara, ulinzi madhubuti na usalama wa mali, hakimiliki ama property rights hususani intellectual property n.k. Kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni, Marekani inatajwa miongoni mwa nchi zenye urahisi zaidi duniani katika kufanya biashara ikishindana na nchi kama vile Korea Kusini, Denmark, Singapore n.k.

Pia, kuna kipimo kingine kinachofahamika kama Global Competitiveness Index.
Watafiti wa masuala ya kiuchumi huangalia uwezo wa nchi kuweza kuufanya uchumi wake uwe na ustawi kwa jinsi ambavyo nchi hiyo inavyoweza kuzitumia ama inavyozitumia rasilimali ilizonazo.

Hapa kuna masuala kadhaa muhimu sana katika ukuaji na ustawi wa uchumi ambayo huangaliwa ama huzingatiwa:
a) Institutions ama taasisi za umma na zile za binafsi ambazo ni well-functioning.
b) Elimu bora (primary & higher education).
c) Afya bora.
d) Miundombinu mahususi.
e) Market size. Ukubwa wa soko la nje na lile la ndani.
f) Innovation. Uwezo katika uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia.
g) Matumizi ya teknolojia zilizopo na mbinu za kisasa katika uzalishaji. Na kadhalika!

Marekani inafanya vizuri katika hili pia kuliko China. Kwenye ripoti kadhaa za GCI hasa za miaka ya hivi karibuni za World Economic Forum, Marekani imekuwa ikitajwa katika nafasi bora na za juu (ya kwanza ama ya pili) ikishindana na nchi za Scandinavia pia na nchi kama vile Singapore.

Marekani inafanya vizuri kuliko China katika studies nyinginezo muhimu kama vile Global Innovation Index (capacity for, and success in innovation) pia hata katika HDI yaani Human Development Index. Katika HDI kuna masuala kadha wa kadha ambayo huzingatiwa ikiwemo life expectancy ya watu, literacy rate n.k.

Kuna hoja umeiwasilisha kuhusiana na Purchasing Power Parity kwamba ni kipimo "kinachoaminika zaidi kuliko GDP", hapa nafikiri unamaanisha nominal GDP. Nafikiri hoja yako hapa haiko sawa!

Iko hivi,
Kila kipimo cha uchumi kinachotumika na mashirika makubwa kama vile IMF, World Bank na UN kina mipaka yake ya matumizi ama limitations. Wataalamu wa masuala ya uchumi kwa ujumla wanaposema kuwa kipimo fulani ni bora kuliko kingine, ni katika kuzingatia baadhi ya masuala pekee. Kuhusu PPP, ni kipimo kizuri hasa pale unapolinganisha bei ya bidhaa kati ya nchi moja na nyingine kulingana na masoko ya nchi hizo lakini kina mapungufu yake mengi ambayo kwayo hakiwezi kusimama kama kipimo pekee sahihi cha uchumi. Hivi sasa kuna mjadala mkubwa sana kuhusiana na hicho kipimo na baadhi ya vipimo vingine hali ambayo itapelekea wataalamu kuja na vipimio vipya hapo baadaye.

Wataalamu wa masuala ya uchumi wanaeleza kuwa, comparisons kwa kutumia kipimo cha Purchasing Power Parity are more useful than those using nominal GDP. Lakini, Purchasing Power Parity is limited when measuring financial flows kati ya mataifa mbalimbali. Pia huleta shida katika kulinganisha ubora wa bidhaa zinazofanana kati ya mataifa mbalimbali (kuna mfano nimeutoa katika post yangu iliyopita wakati nikijibu hoja ya mchangiaji fulani). Purchasing Power Parity pia inahitaji makisio zaidi ama estimations katika mahesabu yake kuliko nominal GDP. Yote hayo ni kwa mujibu wa IMF. Kwa logic ya kawaida tu, kipimo kinachohitaji makisio zaidi kuliko kipimo kingine sidhani kama kinaweza kusimama pekee kama kipimo bora zaidi ama cha kuaminiwa zaidi kuliko vipimo vingine vyote na katika masuala yote muhimu.

Asante!
 
kwanza mimi ntaweka na refence kabisa, cha kwanza unatakiwa ujue China ndio nchi yenye uchumi mkubwa kwa sasa kwa mujibu wa IMF (IMF Admits China Has Overtaken The US As The World’s Largest Economy; But Why Is The Media Silent? )
kumvimbia marekani usifikiri ni ishu ya kitoto ni lazima uwe nae sawa au umemzidi

si kweli kwamba china haina conglomerates kubwa duniani, sema sio maarufu kama za west na nyingine ni kubwa kuliko hata za west, Alibaba, Huwawei hizo ni kampuni ndogondogo China, katika makampuni 10 makubwa zaidi duniani , matano yametoka china manne us na moja saudi arabia, kampuni la kwanza na la pili kwa ukubwa duniani yote yametoka china (https://www.forbes.com/global2000/#142b81a9335d )

soko la hisa halimaanishi kwamba uchumi wako ndio mkubwa kuliko mwingine, na wala soko la hisa sio kigezo cha uchumi wa nchi ndio maana China hilo jambo sio ishu sana, Makampuni mengi ya china wanaorodheshwa marekani lakini mwisho wa siku faida kubwa inaenda kwenye makampuni ya china na sio marekani! ndio maana kuna baadhi ya makampuni trump aliyatoa sokola hisa marekani

Suala ya yuan kutokutumika kimataifa huu ni mfumo ambao china wanautaka wenyewe na yuan hawataki ipande thamani kuliko dola kwasababu ya kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja! ukiwa na dola mia ni rahisi kuwekeza China kuliko marekani! dola 100 kwa marekani ni hela ya maji ya kunywa tu lakini ukiwa china hiyo hela unaweza fanyia mengi sana! Ndio maana mpaka kesho china hawezi pandisha thamani ya yuan ili kuvutia watu na marekani hua analalamika sana kila siku juu ya hili lakini hawez fanya lolote,mpaka kampuni kama telsa na apple kuwekeza china ndo ujiulize

China ni mtengeneza silaha mzuri tu, ila sio muuzaji silaha kila nchi na strategy yake, china, india na urusi ndo nchi pekee zina hypersonic missiles mpaka sasa hata hao marekani na israeli hawana ! china ina jeshi kubwa kuliko nchi yoyote duniani (29 Largest Armies In The World) , China ndo nchi yenye jeshi la majini kubwa kuliko nchi yoyote
(China Has The World’s Largest Navy. And It’s Getting Better, Pentagon Warns )

china ndo nchi inaoongoza kwa matumizi ya artificial intelligence duniani (China Leads in Practical AI | Enterprise IT News) na kampuni zinazojihusisha na AI ni nyingi China kuliko marekani

Kwa mara ya kwanza china imeipita marekani kwa mauzo ya filamu duniani (In 2020, China Surpassed America In Box Office Revenue ) china haiitaji hollywood tena bali hollywood ndo inahitaji china kwa sasa

kwenye cyber security china wapo vizuri sanaaa, waliwaibia NSA pentagon silaha ya kufanyia hacking (Chinese spies stole NSA hacking tools, report finds) na wakaitumia kuwa hack wao wenyewe kwa miaka kadhaa bila kushtukiwa, kwenye cyber securty China na Urusi wapo vizuri sana kuliko unavyofikiri

suala la vita , experience na vifaa kwenye vita vina advantage ndogo sana, marekani alipigwa na kataifa kadogo sana ( vietnam)lenye silaha duni sana na bila experience yoyote mpaka akakimbia akarudi kwako! vita ni teknik bana sio silaha wala experience! unaweza pigana vita miaka 20 mfululizo lakini ukaja kupigwa na mtu ambae hakuwahi kunyanyua hata jiwe maishani mwake! hakuna siku marekani atamvamia na kumpiga mchina, america hana uwezo huo hata china hawezi piga marekani! hizi nchi kamwe haziwez kuingia vitani kwasababu hakutakua na mshindi kati yao
 
Hivi technology Kama ya cocacola ina nafasi gani Kwenye uchumi kwa Karne ya 21
 
Acha kuokoteza habari kwenye source za kipropaganda,,,unajua licence ya kuuza Azam cola anaitoa wapi?
sitaki kujua hilo, jaman kweli kutengeneza soft drinks mpaka leo ni ishu???kwa hyo unataka kusema kapewa na kokakola???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…