William Miller: Kama Yesu hakujua Hisabati au kutafsiri mambo bora angalikaa Kimya. Mbona siku ya mwisho wa dunia inakokotoleka kirahisi?

Kulingana na namba saba,
Unamaana tafsiri ya Miller ni ya akili zake na hakuongozwa na Roho mtakatifu ambae wasabato wa sasa wanaamini alikuwa anamuongoza yy na Ellen,namba 1 na 2,kwa hyo baada ya wao kudanganya ndo wakaanzisha usabato na mkawafuata,
Kwa hiyo ninyi ni wafuasi wa waongo maarufu wawili kuwahi kutokea?
 
Kukosea kutafsiri unabii siyo dhambi...hata wayahudi hawakuulewa unabii wa ujio wa Yesu, walikuwa wanamsubiri masihi mwingine. Hata wanafunzi wa Yesu walikuwa wanajua kuwa Yesu anakuja kusimika ufalme wake duniani, na ndiyo maana alivyowaambia anaenda zake mbinguni hawakumuelewa.

Pointi ni kwamba, huo unabii ulikuwa unalenga tukio fulani, lakini si kama yeye alivyoelewa, swali ni kwamba nyie mnaombeza Miller mnatoa tafasri gani ya huo unabii?
 
Kwa Wasabato, dhambi wanayoichukia sana kuliko zote ni '' kufanya ibada siku ambayo siyo Jumamosi''! Kusema uongo si kitu kwao!
 
Ilishaandikwa "Hakuna ajuaye siku wala saa ya kurudi kwa mwana wa Adam" ikimaanisha kurudi kwa Yesu Kristo ni siri ya Mungu mwenyewe, kwahiyo huyo Miller na wapuuzi wenzie waondolee huko upuuzi wao

Mkuu:

Tusipuuze hiyo formula ya Miller.Inawezekana labda kuna jambo la maana kizazi cha leo na vijavyo vinaweza kujifunza .

Yawezekana labda wataalamu wa Hisabati wakikaza macho na akili kunaweza siku za mbele kutokea kugundua fomula sahihi.Ninasema hivyo kwa sababu wafuasi wa Miller, Ellen White na wenzie, walisema Miller alikosea padogo tu katika kufikiri kwamba siku ile ya 22 Oktoba Yesu angaliwasili kabisa duniani kumbe Yesu aliamua kupumzika katika "chumba" fulani kinaitwa "patakatifu pa patakatifu.Na yuko hapo hadi leo akikagua daftari wa wafuasi wa Usabato.Hirum Edson, mwanzilishi mmoja wapo wa usabato alimuona Yesu akiingia hapo "chumbani" na hata wafuasi wake kama Ellen White ambaye alibahatika kupewa maono 2000 alimuona Yesu sehemu hiyo na ndiyo maana aliandika machapisho lukuki juu ya namna hukumu ya kipelelezi inavyoendeshwa sehemu hiyo na Yesu.

Na ndio maana sasa tunawaalilka wanahisabati wasiuweke pembeni huo mchakato wa Miller wa kutumia fomula ili kufahamu lini Yesu anaingia hapa maskani. Inawezekana siku moja dunia ikaja kuokota kitu cha maana sana huko mbeleni.

Na katika kufanya hivyo ni vizuri tukashirikiana na wasabato kwa sababu hawa jamaa walibahatika kumuona Yesu akiingia humo chumbani na wanamuona kila mara akiendelea na kazi yake ya kupitia daftari la wateule wa kisabato.
 
1. Tueleze hilo tukio ni lipi ambalo unabii ulikuwa unalenga?

2. Hivi unaelewa maana ya unabii?

3. Kwa maelezo yako anayeweza kukosa kuelewa unabii ni mpokea Unabii au mtoa unabii?

4. Unapowatolea mfano Wayahudi, je, wayahudi ndio waliokuwa wametoa unabii au wao walikuwa wapokea unabii?

5. Unapotolea mfano wa wanafunzi wa Yesu kutoelewa kupaa kwake Mbinguni unamaanisha wanafunzi ndio waliotoa huo unabii au wao walikuwa wapokeaji wa unabii husika tu?

6.Je,historia inaonyesha kwamba manabii mbalimbali walipewa unabii au ufunuo fulani na Mungu.Je,unapojitetea kwamba hutokea unabii usiende sawa unaweza kutupatia mifano isiyoacha shaka ya manabii ambao waliwahi kutoa unabii na ukashindwa kwenda sawa sawa?

7.Ellen White aliwaachia wasabato unabii kibao ikiwemo wa Kanisa Katoliki kupitia Papa kuja kuwatesa wasabato, je kwa kutumia utetezi wako wa kwamba hutokea unabii uka-deviate from the reality,unaupa ufunuo au unabii huo wa Ellen White asilimia ngapi kutimia?
 
Mkuu:

Hii yote inatokana na uelewa mdogo wa maandiko matakatifu.Yesu alikuja kufafanua zile Amri kumi kwamba zote ni UPENDO.Kwamba ni upendo kwa Mungu na kwa binadamu wenzetu na mazingira yanayotuzunguka.Kwa hiyo, ukikosa kipengele kimoja unakuwa umekosa upendo wote na Mungu atakuhukumu kwa kukosa upendo na wala si kwa sababu ulikuwa hukosi sabato Jumamosi pamoja na kuongopa na kupotosha watu wake!

Hawa jamaa wanawapotosha sana wafuasi wao kwa kuwajengea chuki dhidi ya wanadamu wenzao wasiokutana nao huko Kanisani kwao Jumamosi.Wanawajengea matumaini makubwa kwamba kwa vile ni wasabato tayari wanayo tiketi ya kuingia Mbinguni na kwamba majina yao yalishaandikwa tayari na ndio maana Yesu alishaanza kushuka kutoka Mbinguni na yuko mahali fulani kwa kazi moja tu ya kupitia majina hayo.Unaweza kuona Ellen White kwa uelewa finyu wa maandiko aliwahi kuwaambia wasabato wenzie wauze mali zao ili wachangie kazi za utume ikiwa ni maandalizi ya kumpokea Yesu mwaka 1885 baada ya ile 1844 kubuma.Utashangaa wakati alikuwa akiwaeleza wenzie juu ya kuuza mali ili wachangie utume katika kujiandaa kumpokea Yesu mwaka 1885 yeye hakuuza hata kijiko chake!
 
Maswali yote la 1-7, hayana mantiki, kwa sababu unabii tunaoungelea ni unabii wa Daniel, siyo wa Miller. Miller hakutoa unabii, bali alitafasri vibaya unabii, kwahiyo Miller hakuwa nabii bali alikuwa mhubiri. Kwahiyo unabii wa Daniel 8:14, hukufail, bali umeshatimia, kama vile mama White alivyoonyeshwa katika maono yake.

Kuhusu kutimia kwa unabii unaohusu mateso kwa kanisa la Mungu, huo lazima utatimia, maana si unabii wa Mama White bali ni unabii wa Mungu mwenyewe, inaweza isiwe katika wakati wangu mimi na wewe lakini lazima utimie maana neno la Mungu haliendi bure.
 
1. Tueleze hilo tukio ni lipi ambalo unabii ulikuwa unalenga?

2. Hivi unaelewa maana ya unabii?

3. Kwa maelezo yako anayeweza kukosa kuelewa unabii ni mpokea Unabii au mtoa unabii?

4. Unapowatolea mfano Wayahudi, je, wayahudi ndio waliokuwa wametoa unabii au wao walikuwa wapokea unabii?

5. Unapotolea mfano wa wanafunzi wa Yesu kutoelewa kupaa kwake Mbinguni unamaanisha wanafunzi ndio waliotoa huo unabii au wao walikuwa wapokeaji wa unabii husika tu?

6.Je,historia inaonyesha kwamba manabii mbalimbali walipewa unabii au ufunuo fulani na Mungu.Je,unapojitetea kwamba hutokea unabii usiende sawa unaweza kutupatia mifano isiyoacha shaka ya manabii ambao waliwahi kutoa unabii na ukashindwa kwenda sawa sawa?

7.Ellen White aliwaachia wasabato unabii kibao ikiwemo wa Kanisa Katoliki kupitia Papa kuja kuwatesa wasabato, je kwa kutumia utetezi wako wa kwamba hutokea unabii uka-deviate from the reality,unaupa ufunuo au unabii huo wa Ellen White asilimia ngapi kutimia?
 
Kwa Wasabato, dhambi wanayoichukia sana kuliko zote ni '' kufanya ibada siku ambayo siyo Jumamosi''! Kusema uongo si kitu kwao!

Mkuu:

Hii yote inatokana na uelewa mdogo wa maandiko matakatifu.Yesu alikuja kufafanua zile Amri kumi kwamba zote ni UPENDO.Kwamba ni upendo kwa Mungu na kwa binadamu wenzetu na mazingira yanayotuzunguka.Kwa hiyo, ukikosa kipengele kimoja unakuwa umekosa upendo wote na Mungu atakuhukumu kwa kukosa upendo na wala si kwa sababu ulikuwa hukosi sabato Jumamosi pamoja na kuongopa na kupotosha watu wake!

Hawa jamaa wanawapotosha sana wafuasi wao kwa kuwajengea chuki dhidi ya wanadamu wenzao wasiokutana nao huko Kanisani kwao Jumamosi.Wanawajengea matumaini makubwa kwamba kwa vile ni wasabato tayari wanayo tiketi ya kuingia Mbinguni na kwamba majina yao yalishaandikwa tayari na ndio maana Yesu alishaanza kushuka kutoka Mbinguni na yuko mahali fulani kwa kazi moja tu ya kupitia majina hayo.Unaweza kuona Ellen White kwa uelewa finyu wa maandiko aliwahi kuwaambia wasabato wenzie wauze mali zao ili wachangie kazi za utume ikiwa ni maandalizi ya kumpokea Yesu mwaka 1885 baada ya ile 1844 kubuma.Utashangaa wakati alikuwa akiwaeleza wenzie juu ya kuuza mali ili wachangie utume katika kujiandaa kumpokea Yesu mwaka 1885 yeye hakuuza hata kijiko chake!
 
zamani nilikuwa nkisikia mwisho wa dunia nawaza watu wote twafaaa....kumbe sio....KILA NAFSI itaonja mauti kwa miaka, miezi, wiki, siku na mida tofauti!

WACHAGGA walishaambiwaga mwisho wa duniaa....hahaaaa...WAZEE wakachinja mbuzi wakanywa supu na mashoraaa, wengine wapo hai adi leo
 
Hivi bado kuna mkirisito mwenye akili anaamini kusali jumosi au jumapili ndo kigezo cha kwenda mbinguni??
 
Hujui unalolisema...Namwomba Mungu akusamehe tu!
 
Hujui unalolisema...Namwomba Mungu akusamehe tu!

1.Ni jambo jema kuniombea msamaha kwa Mungu.

2.Lakini toka lini wasabato mnaaamini katika fundisho la mtu mmoja kumuombea mwenzie msamaha kwa Mungu na kweli Mungu akapokea msamaha kama huo? Ni kwa nini usionyeshe tu dhambi yangu halafu mimi nijiombee msamaha mwenyewe maana bado niko hai sijafa.Kama Mungu anaweza kupokea ombi lako kwa dhambi zangu wakati mimi mwenyewe bado niko hai ni kwa nini basi akatae maombi ya msamaha wa dhambi kwa ajili ya waliokwisha kufa?
 
Hivi bado kuna mkirisito mwenye akili anaamini kusali jumosi au jumapili ndo kigezo cha kwenda mbinguni??

Waulize wenye sabato yao kwa maana wanasema Agizo hilo halina mjadala.Na ndio maana katika nyimbo zao mara zote wanaimba Mungu aje awachukue haraka na nyingine wanaimba kwa madaha kuonyesha jinsi watakavyokuwa wakipokelewa na Mungu siku hiyo.Hii yote ni kuonyesha kwamba tayari wanayo ASSURANCE la sivyo wangaliimba nyimbo za kuomba HURUMA ya Mungu.
 
Upo vizuri mkuu! Heshima kwako.
 
Mkuu! Hivi ni kweli kanisa la wasabato lipo kwenye muungano wa makanisa?
 
Unasema William Miller hakutoa unabii? Umeshindwa kuangalia hata maana ya neno Unabii katika Kamusi? Unaka tuamini kwamba William Miller kusema Yesu angalirudi tarehe 22 Oktoba 1844 siyo Unabii bali mahubiri tu,siyo? Kusema kwamba jambo fulani linalohusiana na imani litatokea namna hii au tarehe fulani au sehemu fulani siyo unabii bali ni mahubiri tu,siyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…