Wimbi la vijana wengi kutembelea gari za kike

Wimbi la vijana wengi kutembelea gari za kike

Ndugu zangu

Inakuwaje mwanaume mzima anaendesha ka baby Walker?

Yaani jibaba nene linatumia kigari cha mkewe? Huoni aibu? Si bora hata upande daladala?

Hata Bashite alisema wazi vi gari vya IST ni vigari vya kuhongwa wewe mwanaume huoni aibu?

Hii tabia walikuwa nayo wanaume wa Kinondoni, ila sasa wameambukiza na wa mikoani..

Aibu sana
Kuna namna nyingi sana za kuonesha ujinga. Nadhani hii ni mojawapo
 
Bonge la mtu,kitambi kule na suti kuubwa,anachomoza kwenye IST...
Exposure yako ndogo sana mkuu, kama wewe ni jinsia ya kiume basi ni tatizo. Ungelikuwa umeitembea hii dunia japo kidogo usingeandika ulichoandika. Wewe na mtoa mada bado hamjakua kama rafiki yenu Makonda.
 
Wazee hapa always mnajigamba sana kwamba kila mwanaume ana gari kumbe gari zenyewe ni IST?

Poleni sana japo nimewashambulia sanaaa
Wewe ushamba unakusumbua. Mataifa yote yaliyoendelea asiliamia kubwa ndiyo magari yao.
 
Hajamtibua yeyote zaidi ya kuonyesha UJUHA wake hadharani. Kaambiwa aweke list ya manufacturers wa magari inayoonyesha magari ya kile/kiume anang’aa macho! Baadhi ya Watanzania ni Wapumbavu wa kutupa kwa kupenda kujifanya wanajua mambo ambayo kumbe hawajui lolote lile.
Jaamaa katibua watu na wamekubali kutibuliwa
 
Watanzania kuna mahala tumerogwa,ndio maana wanasiasa ni rahisi sana kututeka na kututawala vile watakavyo,ksbb ni mijitu haijielewi ni kitu gani inataka. Huyu nae aliefungue tred ukute nae,ana digree au diproma kwa utumbo huu. Ni Tanzania tu utaona kuna watu wamechambua magari kijinsia. Halafu ukute hata toroli huna,huku unajifanya una hela za V8,mbweha we. Kwa bashite kweli ndio umeona unaweza kupata maneno?
 
Uliza kwanza kwa nini vijana wengi hawana hata bajaji badala ya kuanza kuongea ushamba wako
 
Japo sikatai kuwa mimi ni masikini sana, lakini kwa kweli kuna vigari ni vya kike.

Kigari kiko kama toroli lililoezekwa bati! Hapana aisee....

Kama una pesa nunua gari yenye nguvu....... Kama hauna pia sio mbaya kuwa na IST. Maisha ni kuchagua.

Lakini penye ukweli pasemwe tu!

Tugari tudogo dogo twa kichina kama IST ni twa kike!
 
Watanzania kuna mahala tumerogwa,ndio maana wanasiasa ni rahisi sana kututeka na kututawala vile watakavyo,ksbb ni mijitu haijielewi ni kitu gani inataka. Huyu nae aliefungue tred ukute nae,ana digree au diproma kwa utumbo huu. Ni Tanzania tu utaona kuna watu wamechambua magari kijinsia. Halafu ukute hata toroli huna,huku unajifanya una hela za V8,mbweha we. Kwa bashite kweli ndio umeona unaweza kupata maneno?
Usifoke sana bro... kuwa na IST sio dhambi.
 
Kuna shoga angu alikuwa anagombana na mfanyakazi mwenzie kazini ( huyo mwenzie Ana gari)
Katika kubwatuzana yule shoga angu akaropoka " unaringia hicho kigari.....wakati hilo ni kaburi tu..mnajifanya matajiri mnanunua makaburi"
Wakati yeye anapanda daladala Kila siku.
Nilivyosoma hii thread nimemkumbuka shoga yangu..
Maneno ya mkosaji!!!
🤣
Nimecheka kwa sauti.
Yeye atuambie anaendesha gari gani, au ndio wale "bora kupanda daladala kuliko kuendesha baby walker"
 
Exposure yako ndogo sana mkuu, kama wewe ni jinsia ya kiume basi ni tatizo. Ungelikuwa umeitembea hii dunia japo kidogo usingeandika ulichoandika. Wewe na mtoa mada bado hamjakua kama rafiki yenu Makonda.
Usinielewe vibaya mkuu,mimi sijapondea kuwa ni vigari vya kike,nimesemea tu jinsi mtu wa aina hiyo akiwa anatoka kwenye hiyo aina ya gari huwa hapendezi kiukweli,lakini kama nguvu yake ndio ilipoishia anunue tu,cha muhimu na yeye anaenda akiwa amekaa...
 
Kuna watu wanaendesha ist lakini Wana miliki majumba ya milioni 500 na kuendelea
 
Mkuu tuwapuuze hawa vijana maana hawajui hali ya maisha kitaa ilivyo ngumu🤣🤣🤣
🤣 🤣 🤣 hakika mkuu. Kutokana na hali ya kiuchumi kubadilika, raia wengi kwa sasa wanakimbilia kununua na kutumia magari ambayo ni fuel economic (yenye injini ndogo). Kwa maana hii, magari kama IST, Passo, Vitz, Suzuki Swift, Premio, Corona, Carina TI na Pajero Mini yanakuwa dili sana. Kwa nini uhangaike na injini kubwa kama ndogo zipo> Sawa hawa wanaoishi kwa wazazi wao ndio wanaoponda hizi gazi na kuita za kike. Ni pumbavu wa hali ya juu sana. Unless kama kaandika ni JOKES
 
Back
Top Bottom