Lady Mwali
Senior Member
- Nov 15, 2018
- 147
- 333
Wanapendwa,
Watoto wadogo kuanzia umri wa miaka 6 mpaka 12 asilimia kubwa wasichana kwa nyakati tofauti wamekuwa wakitoa shuhuda za kujishughulisha na uchawi katika kanisa maarufu lilipo Dar es Salaam.
Katika shuhuda hizo watoto hao hukiri kujihusisha katika vitendo vya kichawi vya kuua watu na kula nyama zao na kunywa damu zao.
Mchunguji umuhoji mtoto husika ameeingia vipi katika chama cha kichawi,wengi wanakiri bibi zao wamewapa uchawi, miongoni mwao hukiri kutaka kuwaua wazazi wao kwa uchawi.
Mtoto anahojiwa amekuja na nani na kumtaja mtu aliyekuja naye, mara nyingi mama na kuitwa kuja madhahabuni.
Mzazi huambiwa maisha yake yalikuwa hatarini kwa kuuawa na mwanae kishirikina.
Watoto hao huto shuhuda hizo muda wa usiku kuanzia saa tano mbele ya waumini wengi huku wakionesha kujiamini.
Mchungaji anawatoa katika chama cha kichawi na kuwa watoto wema.
Shuhuda iliyokuwa kubwa ni ile ya binti wa umri wa miaka 16 anayesoma kidato cha pili shule ya Kibasila kukiri kuua watu kwa kuwaaambukiza HIV kishirikina.
Amekiri kuua wanaume 600 kwa kuwaaambukiza HIV kishirikina.
Wasiwasi wangu ni vipi usalama wa hawa watoto baada ya kukiri kuua watu wengi kishirikina wakirudi mitaani? Maana kumekuwa na mauaji ya washirikina katika sehemu mbalimbali nchini.
Ikumbukwe shuhuda hizi zanarushwa kwenye tv na kuonwa na watu wengi ndani na nje ya nchi.
Sheria za mtoto zinasemaje kumlinda mtoto katika hali hii?