Huu wimbo hua unanikumbusha mama yangu aise, alikua akitwanga mpunga anakua anauimba sana. Nikimmiss hua nauimba huu.Nyimbo zangu pendwa za zamani na za sasa
11. Mke Mwema - FPTC Kasulu vijana choir
Mwana mpotevu imenikumbusha enzi za utoto mbali sanaMuungano kwaya + Natembea mimi ni Marehemu
St.James/Tumaini kwaya Arusha /Shangilieni - Habari ya Mwana mpotevu, Nuhu, Nakulilia Jehova
Kijitonyama Upendo group
Huu wimbo hauchujiHakuna Mungu kama wewe ikipigwa Club au Bar walevi wote lazima waserebuke...
Ile ni hatari nimesave na video kabisaHakuna Mungu kama wewe ikipigwa Club au Bar walevi wote lazima waserebuke...
Huu ndo ule kwetu pazuuuriiiiZablon Singers --Mkono wa Bwana
Huu wimbo unapendwa mpaka na waislamu na sometimes inapigwa mpaka kwenye kumbi za starehe
Sio kasikilize youtube ndio utajua vizuriHuu ndo ule kwetu pazuuuriiii
3 na 4, Umenikumbusha mbali.Lakini hapo KKKT Kijitonyama umewakazia hebu rejea hizi
1)eyawe simbanga
2)simba wa Yuda
3)msalaba wa yesu
4)hakuna mwanaume kama yesu
5)ndani ya safina
Kama unapenda kusikiliza vyombo vya mziki hebu sikiliza hizo kitu ni habari nyingine kabisa
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Namba mbili.Nyimbo zangu pendwa za zamani na za sasa
1. Simba wa yuda - unanikumbushaga siku ya send off yangu miaka hiyo, ukumbi ulirindima
2. Sauti ikatoka - kkkt mabibo
3. Albamu nzima ya mwenye mamlaka - Ulyankulu
4. Ee Mungu Nitakushukuru - Rose Mudando
5. Huyo ni Yesu - Ambassador Kigali
6. Nenda na uzima wako - AIC chang'ombe
7. Ombi langu - Magena youth
8. Haiwezekani na Nyanyua bendera - Kkkt Keko vijana
9. Mkono wa Bwana - Zabron singers
10. Alfajiri ya Kupendeza - Nairobi University
11. Mke Mwema - FPTC Kasulu vijana choir
Kuwa serious jombaa[emoji134][emoji134][emoji134]Nabii Tito - Ni wema wako Yesu
Kwa hili nitakuita baba samahani Kama ni mwanamkeShaloom wakuu,
Tasnia ya muziki wa injili kwa vikundi vya kwaya hapa Tanzania ni tasnia kongwe na iliyotawala zaidi kwenye chati za nyimbo za dini ya Kikristo mpaka ilipofikia miaka ya 2000's ambapo walianza kuibuka waimbaji wa kujitegemea wa nyimbo za injili na kwa wingi wao imepelekea umaarufu wa vikundi na nyimbo za kwaya kushuka kwa miaka ya karibuni.
Binafsi ni mpenzi mkubwa wa nyimbo za kwaya toka miaka hiyo mpaka sasa na leo niliamka nikiwaza ni nyimbo gani ya injili ya kwaya ambayo tunaweza kusema ndio nyimbo bora zaidi kupata kutengenezwa/kuimbwa hapa Tanzania toka mziki huu uanzishwe.
Naomba mnisaidie kuchagua namba moja kwenye list ya nyimbo za kwaya ninazoona ziliwahi kutikisa sana tasnia ya nyimbo za injili na wewe pia unaweza kuongezea chaguo lako kama unaona haipo kwenye orodha hiyo;
1. Tabata Menonite - Kunyata nyata
2. AIC Makongoro- Utumwa wa waisrael & Kekundu
3. Mtoni Evangelical- Lulu
4. Bethel Gospel - Yupo Mungu
5. Barabara ya 13- Samson na Delila
6. Mapigano Ulyankuru- Katika viumbe vyote & Goliati & Fahari ya vijana
7. Nkinga choir - Sauli wanitesa
8. KKKT Mabibo - Nijaposema kwa lugha & Sauti ikatoka.
9. AIC Chang'ombe - Gusa
10. Zablon Singers - Mkono wa Bwana
11. Jerusalem choir - Kesho ni yako
12. Kijitonyama uinjilisti - Hakuna Mungu kama wewe & Simba wa Yuda
13. Pastor Alex & Mary Atieno - Sodoma na Gomorrah
14. Eternal life gospel - Sio sisi
15. Mtakatifu Kizito Makuburi - Mimina & Yesu ni mwema
16. Mt. Theresia Matogoro - I love you
17. Kapotive star- Nimeonja pendo lako
18. Arusha town - Kila mtu na mzigo wake
19. Tafes (Ardhi)- Maserafi
20. Essence of worship- Mimi siwezi
21. The reapers - Ninaye rafiki
22. Muungano choir- Natembea mimi ni marehemu.
23. Mt Kizito- Watoto wa nyumba zote
Karibuni.