Wimbo wa Isabela Kombo Mungu ni mmoja wazua gumzo

Wimbo wa Isabela Kombo Mungu ni mmoja wazua gumzo

Yani ukristo ni ajabu sana wao wenyewe wanakataana dini haina misingi vikundi kibao kila mtu anasema lake hivi hiyo ni dini kweli
 
Huo wimbo sijausikiliza ila ni wimbo mzuri na nmeupenda sana
Naomba Jina la Wimbo umeimbwa na Msanii J Martin's nakumbuka baadhi ya lyrics kuna line anasema

Who do you dey, my Girl she gon cheat on me (cheating on me)

Jina la Wimbo tafadhari kwa Hisani ya Watu wa JF
 
Nenda Shazam afu Anza kuimba huo wimbo mana lyrics unazijua
 
Hakuna Mungu anaitwa Yesu

Ye mwenyewe anamuomba Mungu

Yesu ni mwana wa Mungu kama wewe ulivyomwana wa Mungu na kuitwa mwana wa Mungu ni sababu ya uumbaji Mungu alipuliza uhai kwa kitu alicholiunda kwa udongo

Yohana 8
52 Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng'amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele.

53 Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani?

56 Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.

57 Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu?

58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.
 
Kwangu Mungu ni dhahiri

Ombi lako limefika na atajidhihirisha kwako Kabla hujaiacha Dunia

Ukumhuke kuleta mrejesho hapa
Kuiacha dunia hata wewe utaiacha na wala mimi sitakuwa wa kwanza wala wa mwisho kuiacha dunia.

Kama kwako Mungu huyo ni dhahiri, thibitisha udhahiri wake kwamba yupo.

Kama wewe huwezi kuthibitisha, Mwambie huyo Mungu wako ambaye ni dhahiri aje hapa ajidhihirishe mwenyewe uwepo wake.
 
Si ndiooooo 😂
Isaya 41
4 Ni nani aliyetenda na kufanya jambo hilo, aviitaye vizazi tangu mwanzo? Mimi, Bwana, wa kwanza na wa mwisho, mimi ndiye.

YESU NI MUNGU

Tito 2
13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;

Mathayo 4
5 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu,

6 akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.

Yohana 14
8 Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.

9 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?

14 Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.

Yohana 5
43 Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo.
 
Kuiacha dunia hata wewe utaiacha na wala mimi sitakuwa wa kwanza wala wa mwisho kuiacha dunia.

Kama kwako Mungu huyo ni dhahiri, thibitisha udhahiri wake kwamba yupo.

Kama wewe huwezi kuthibitisha, Mwambie huyo Mungu wako ambaye ni dhahiri aje hapa ajidhihirishe mwenyewe uwepo wake.

Wewe usiyeamini hata nikithibitisha utaamini unachoamini

Atajidhirisha kwako punde
 
kuna watu wanaquestion tatoo yake kifuani, alishaitolea ufafanuzi kwamba kabla ya kuingia kwenye gospel alikuwa anaimba na kina jaydee duniani, hivyo alishafanya sana hayo mambo ya duniani hadi akawa na matatoo hayo. sasa tatoo ukishaiweka kwani inatoka, kuitoa si hadi uharibu ngozi?
 
Yohana 8
52 Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng'amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele.

53 Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani?

56 Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.

57 Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu?

58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.
Wapi hapo YESU kasema yeye ni Mungu au umeamua tu kujitoa mabetri?
 
Mungu ni MMOJA,

Na YESU KRISTO YESHUA HAMASHIACH ndilo JINA lake.

Amen
 
Kuna nabii ametokea anadai wimbo huu mdada kauimba kwa kutumiwa na shetani bila yeye kujua, labda kwasababu amekuja wakati wa trend shetani anaagiza manabii na mitume wa uongo hao wauza mafuta waufute uungu wa Yesu. what I think about it;

1. Mungu ni mmoja tu, ila amejidhihirisha kwa nafsi tatu.
2. Yesu ni nafsi ya Mungu, hivyo ni Mungu yule yule.
3. Mzee wa ngome ya temboni ambaye namjua ni ajenti, mzee wa kibangu a.k.a Konyagi bapa, manabii mbalimbali wa uongo bongo wameibuka kwa pamoja wanadai Hakuna utatu mtakatifu na kwamba Yesu alikuwa mwanadamu wa kawaida tu, sio Mungu. wakati Biblia inasema hata kabla ya Agano JIpya (kitabu cha Isaya) kwamba Yesu ni Mungu mwenye Nguvu.

4. Wimbo huu ukiusikiliza vizuri, unaweza kuamini kwamba ni mojawapo ya shughuli za adui kuingiza ajenda zake kidogokidogo hadi aufute kabisa Uungu wa Yesu.

5. Kwa msiojua, ukijifanya wewe unamtumikia Mungu hakikisha upo vizuri kiroho, haufungui milango kama uzinzi, ugomvi, na uchafu mwingine. ukifanay hivyo hata kama wewe unajifanya kumtumikia Mungu shetani anaweza kuingia kwako akajifanya malaika wa nuru, akakupa mahubiri ya uongo, akakupa maono ya uongo, akakupa kunena kwa lugha ya uongo, akakupa nyimbo za uongo akakufanay ajenti wake bila wewe kujua kwasababu umeshafungua milango na yupo ndani yako. anaweza hata kufanya miujiza ya ajabu kabisa na watu wakakuona kama ni mtumishi au mwimbaji, kumbe shetani ameingia ndani ya kanisa anapigana kutokea ndani.

Hii ndio imewafanay wahubiri wengi wa Mungu ambao walikuwa wazuri kubadilika, walitumiwa na Mungu, wakateleza na kufungua milango, shetani akaingia akawabadilisha kabisa namna ya utendaji. hao wanaouza mafuta, maji, na keki usifikiri hawajawahi kuokoka. Majority yao wametokea kanisa la TAG, EAGT, FPCT na mengine ya kiroho. walikuwa walokole, ila walifungua mlango shetani akaingia, akabadilisha theologia yao kabisa na wanamtumikia shetani na shetani anawapa pesa.
Kuhusu Mungu kuwa na nafsi 3 huo ni upumbavu na uongo ambao haupo hata kwenye biblia ni upumbavu kamili wa mtu asiye na chembe ya akili.
 
Wapi hapo YESU kasema yeye ni Mungu au umeamua tu kujitoa mabetri?
Nawe acha ubishi, mbona jamaa kakujibu kwa maandiko kuthibitisha hilo. Kwa mfano
Mathayo 4: 6-7
6 akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu BWANA MUNGU WAKO.
 
Kuhusu Mungu kuwa na nafsi 3 huo ni upumbavu na uongo ambao haupo hata kwenye biblia ni upumbavu kamili wa mtu asiye na chembe ya akili.
Rudi upya ukajifunze upya Biblia. Biblia yote imejaa ufunuo wa utatu mtakatifu. Huwezi kupingana na huo ukweli.
 
Back
Top Bottom