Yohana 1
1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
5 Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.
6 Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana.
7 Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye.
8 Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru.
9 Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu.
10 Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua.
11 Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.
12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Yohana 1
17 Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.
18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.
From hiyo Yohana 1: 14 means yesu ni neno aliye umba vyote.
Tuongeze mengine Kidgo.
Yohana 8:58
[58]Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.
Jesus said unto them, Verily, verily, I say unto you, Before Abraham was, I am.
Yohana 10:30
[30]Mimi na Baba tu umoja.
I and my Father are one.
Matendo ya Mitume 20:28
[28]Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.
Take heed therefore unto yourselves, and to all the flock, over the which the Holy Ghost hath made you overseers, to feed the church of God, which he hath purchased with his own blood.
[ Kanisa MUNGU alilo linunua kwa Damu yake mwenyewe, Means someone alimwaga damu, wew jibu wajua ]
Tito 2:13
[13]tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;
Looking for that blessed hope, and the glorious appearing of the great God and our Saviour Jesus Christ;
Mathayo 2:11
[11]Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane.
And when they were come into the house, they saw the young child with Mary his mother, and fell down, and worshipped him: and when they had opened their treasures, they presented unto him gifts; gold, and frankincense, and myrrh.
[ Kuna settings nyingi sanaa, watu wa rohon, wachaw,mama jusi wanaofaham mambo ya rohon walikuw wakisujudia mbele ya Yesu]
Ufunuo wa Yohana 22:13-16
[13]Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
I am Alpha and Omega, the beginning and the end, the first and the last.
[14]Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.
Blessed are they that do his commandments, that they may have right to the tree of life, and may enter in through the gates into the city.
[15]Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.
For without are dogs, and sorcerers, and whoremongers, and murderers, and idolaters, and whosoever loveth and maketh a lie.
[16]Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi.
I Jesus have sent mine angel to testify unto you these things in the churches. I am the root and the offspring of David, and the bright and morning star.