Wimbo wa Isabela Kombo Mungu ni mmoja wazua gumzo

Yani ukristo ni ajabu sana wao wenyewe wanakataana dini haina misingi vikundi kibao kila mtu anasema lake hivi hiyo ni dini kweli
 
Huo wimbo sijausikiliza ila ni wimbo mzuri na nmeupenda sana
Naomba Jina la Wimbo umeimbwa na Msanii J Martin's nakumbuka baadhi ya lyrics kuna line anasema

Who do you dey, my Girl she gon cheat on me (cheating on me)

Jina la Wimbo tafadhari kwa Hisani ya Watu wa JF
 
Naomba Jina la Wimbo umeimbwa na Msanii J Martin's nakumbuka baadhi ya lyrics kuna line anasema

Who do you dey, my Girl she gon cheat on me (cheating on me)

Jina la Wimbo tafadhari kwa Hisani ya Watu wa JF
Nenda Shazam afu Anza kuimba huo wimbo mana lyrics unazijua
 
Hakuna Mungu anaitwa Yesu

Ye mwenyewe anamuomba Mungu

Yesu ni mwana wa Mungu kama wewe ulivyomwana wa Mungu na kuitwa mwana wa Mungu ni sababu ya uumbaji Mungu alipuliza uhai kwa kitu alicholiunda kwa udongo


Yohana 8
52 Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng'amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele.

53 Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani?

56 Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.

57 Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu?

58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.
 
Kwangu Mungu ni dhahiri

Ombi lako limefika na atajidhihirisha kwako Kabla hujaiacha Dunia

Ukumhuke kuleta mrejesho hapa
Kuiacha dunia hata wewe utaiacha na wala mimi sitakuwa wa kwanza wala wa mwisho kuiacha dunia.

Kama kwako Mungu huyo ni dhahiri, thibitisha udhahiri wake kwamba yupo.

Kama wewe huwezi kuthibitisha, Mwambie huyo Mungu wako ambaye ni dhahiri aje hapa ajidhihirishe mwenyewe uwepo wake.
 
Si ndiooooo 😂
Isaya 41
4 Ni nani aliyetenda na kufanya jambo hilo, aviitaye vizazi tangu mwanzo? Mimi, Bwana, wa kwanza na wa mwisho, mimi ndiye.


YESU NI MUNGU

Tito 2
13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;

Mathayo 4
5 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu,

6 akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.

Yohana 14
8 Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.

9 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?

14 Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.

Yohana 5
43 Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo.
 

Wewe usiyeamini hata nikithibitisha utaamini unachoamini

Atajidhirisha kwako punde
 
kuna watu wanaquestion tatoo yake kifuani, alishaitolea ufafanuzi kwamba kabla ya kuingia kwenye gospel alikuwa anaimba na kina jaydee duniani, hivyo alishafanya sana hayo mambo ya duniani hadi akawa na matatoo hayo. sasa tatoo ukishaiweka kwani inatoka, kuitoa si hadi uharibu ngozi?
 
Wapi hapo YESU kasema yeye ni Mungu au umeamua tu kujitoa mabetri?
 
Mungu ni MMOJA,

Na YESU KRISTO YESHUA HAMASHIACH ndilo JINA lake.

Amen
 
Kuhusu Mungu kuwa na nafsi 3 huo ni upumbavu na uongo ambao haupo hata kwenye biblia ni upumbavu kamili wa mtu asiye na chembe ya akili.
 
Wapi hapo YESU kasema yeye ni Mungu au umeamua tu kujitoa mabetri?
Nawe acha ubishi, mbona jamaa kakujibu kwa maandiko kuthibitisha hilo. Kwa mfano
Mathayo 4: 6-7
6 akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu BWANA MUNGU WAKO.
 
Kuhusu Mungu kuwa na nafsi 3 huo ni upumbavu na uongo ambao haupo hata kwenye biblia ni upumbavu kamili wa mtu asiye na chembe ya akili.
Rudi upya ukajifunze upya Biblia. Biblia yote imejaa ufunuo wa utatu mtakatifu. Huwezi kupingana na huo ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…