Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ilijitegemea, ikarudhishwa huku kwa mapenzi ya watawala wetu humuKwa maswali yako hayo mazuri, na wewe ungeazisha thread yako inayojitegemea!
Unachokisema kinatoka moyoni au unafurahisha kijiwe?Watia nia nafasi ya ubunge ni wengi kuliko wapiga kura.
Wakuu yaani kila ninayemfahamu anaona anaweza kuwa mbunge kupitia CCM.
Niko na mdogo wangu hapa ananiambia hata yeye anaona kama anaweza kuwa mbunge wa CCM mwaka huu akiamua wakati hajui hata Polepole ni nani au katibu mkuu wa CCM ni nani.
Maana kila mtu anaona anaweza.
NINI MAONI YAKO.
1: Je, Ubunge umerahisishwa sana wakati huu?
2: Je, CCM Imekuwa safi kiasi kwamba hakuna hata wasio na pesa nao wanaweza kupita kuwa wabunge?
3: Je, Ubunge Watu wanatamani kufanya kazi na Raisi ajaye ikiwa mwenyekinti wa CCM atashinda?
Nini maoni yako
Wanaandaliwa wawakilishi wa rais.Siasa za Magufuli ni sawa na kocha anayefundisha mfumo wa kupack basi. Mchezo wa aina hiyo unaboa sana. Ndio maana kwa sasa siasa zetu ni so boaring. Katika mazingira haya ndio hapo unapoona kundi la kubwa la upande mmoja, maana ushindani halisi haupo. Sidhani kuwa ccm ni imara au inakubalika sana, bali siasa zenye ushenzi, uhayawani na ukatili wa wazi, umefanya chaguzi zetu kuondoa ushindani halisi, na kuleta ushindani wa kujipendekeza kwa rais. Matokeo yake, kila anayeona anajuana na rais kwa namna yake, anajitokeza kutaka kuchaguliwa kugombea uwakilishi.
Wanaandaliwa wawakilishi wa rais.
Sisi wananchi hatuna mwakilishi hata tukipiga kura.
Watia nia wote wanalilia matumbo yao hawaipendi CCM bali nafsi zao binafsiWanaounga mkuno juhudi za Mh. Rais ni wale walioamua kufanya kazi (hasa za uzalishaji) kwa bidii, weledi na uaminifu kwa ajili ya maendeleo ya taifa. Watia nia wote ni watafuta umaarufu na wachumia tumbo tu.
Nafasi za uongozi kama Ubunge, Udiwani
Wengi wanajua ukiwa CCM ukawa na madaraka ni njia bora ya kufanya chochote pasipo kusumbuliwa na yeyoteWingi wa watia nia ni uthibitisho kua tamaa ya madaraka imeongezeka sana.
Rais ajaye anakazi kubwa sana! Itabidi tumsamehe kipindi cha miaka ile mitano ya kwanza hata asipofanya maendeleo yoyote! Ana kazi ya kurejesha mifumo kama ilivyo kwenye kanuni za uongozi wa nchi! Watanzania tumeamua kumwachia mtu mmoja ndiye aamue mwelekeo wetu kama taifa na katika hili wala hatujiulizi je mtu huyo tunayemwamini ana akili timamu? Watz ipo siku tutatumia akili ya taahira!!Bwana yule kaharibu sana mifumo ya hii nchi na kajigeuza Mungu mtu,na matokeo yake sasa kila mtu anamlamba miguu maana maamuzi yote ni yake baada ya kuvuraga demokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa kuanzia kwenye chama chake na nchi nzima kwa ujumla