Uchaguzi 2020 Wingi wa wagombea CCM ni uthibitisho kazi nzuri ya Rais Magufuli kwa taifa letu. Je, Oktoba ni kuchagua au kuthibitisha tu taratibu?

Uchaguzi 2020 Wingi wa wagombea CCM ni uthibitisho kazi nzuri ya Rais Magufuli kwa taifa letu. Je, Oktoba ni kuchagua au kuthibitisha tu taratibu?

Kuwa na uhakika wa kushinda Oktoba kupitia CCM ndiko kumepelekea wagombea kuwa wengi. Wanaamini kutafanyika fitina Kama za mwaka jana uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo wagombea wote wa CCM walishinda.
 
Bora form moja kuliko huko kwa wapinzani chama Ni Mali binafsi ya mtu Ni Kama vijisaccos tu mwenyekiti Ni wa kudumu ukijaribu kugombea unaweza hata kuuliwa Kama chacha wangwe kufukuzwa Kama kina zito kutishiwa kuuliwa Kama sumaye na wenzake halafu misukule inaambiwa hii ndio demokrasia Ila kiuhalisia Ni Domo krasia
Magufuli alisema atamshangaa IGP kwenda kugombea ili ateuliwe kuwa Waziri. Anaweza akalikatilia mbali jina lake, inategemea siku hiyo atakuwa ameamkaje. Hapa unadhani chama ni mali ya wanachama au ya mtu mmoja? Yani hatma ya watia nia wa CCM ipo mikononi mwake na sio mwa vikao vya chama

Mungu Ibariki Tz - MITz
 
Hilo swali lako hata mimi bado nalitafutia jawabu, ila jawabu nililopata mwanzo liliniambia hao watia nia wanajua as long as watapitishwa na vikao vyao vya ndani, basi automatically watakuwa wabunge tayari, sababu jamaa alishatoa maagizo kwa wakurugenzi wa majiji na halmashauri nchi nzima.
 
Kama lengo ni hilo kuwa watafikiriwa katika nafasi za uteuzi. Naomba nitangaze kuwa kuna watu watapigwa za USO hivi karibuni.
Rushwwa ili kupata vyeo. Hii imekuwepo miaka mingi kabla ya Mwema kuteuliwa kuwa IGP, makamanda kadhaa walipigwa za USO na matapeli wakiokuwa wakijifanya wwanashughulikia mafaili yao kwa ajili ya uteuzi.
 
Wana jamvi wasalaam!

Kumekuwepo na utitiri wa "wana CCM" kutia nia kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huu ujao wa 2020. Tafakuli fikirishi ya hao "wana CCM" JE ni kweli wako serious au wala lao jambo?

Baada ya Uchaguzi wa 2015 kila mtu alishuhudia kilichotokea, baada ya bwana mkubwa kutangazwa kashinda kilichofuatia ni teuzi za watia nia wa wakati huo kuteuliwa haswa haswa kwenye posti za DED na DAS.

Nadhani opportunists wameshasoma mchezo wa uchaguzi uliopita hivyo wameamua kuweka CVs zao kwa bwana mkubwa ili nao wafikiriwe kwenye posti hizo.

Trend hii ya ukada kupewa kipaumbele kwenye teuzi especially watia nia ukiwa unaona mbele itakuwa na matunda yake very soon! Na nadhani dalili ya maua ni suala hili la watia nia, bado kidogo matunda yataanza kudondoka!

Walio serious kugombea huenda wapo ila waliowengi ni wa kusubmit resumes!

Tukae tusubiri
Nafikiri watu hao wanadhani kwamba watashinda tu kwa ubabe wa mwenyekiti.
 
Bora form moja kuliko huko kwa wapinzani chama Ni Mali binafsi ya mtu Ni Kama vijisaccos tu mwenyekiti Ni wa kudumu ukijaribu kugombea unaweza hata kuuliwa Kama chacha wangwe kufukuzwa Kama kina zito kutishiwa kuuliwa Kama sumaye na wenzake halafu misukule inaambiwa hii ndio demokrasia Ila kiuhalisia Ni Domo krasia

Ondoa kule mawazo yako old fashion, bado unaimba nyimbo za kina Wangwe ambazo hata watoto wa marehemu walisha waambia acheni upuuzi!
Uchaguzi wa mwenyekiti hukuuona weye! Unaishi wapi ndugu?
 
Afadhali mawazo yangu ya old fashion kuliko mtu Kama wewe umeshikiwa akili na MBOWE hujui kweli ni lipi unaitikia mapambio ya DJ tu
Mbowe anishikie akili kwa lipi? Mmebaki kukaririshwa nyimbo hizohizo tokea zamani na hambadiliki.
Marehemu Mtikila alikwenda Tarime na gia ya kumtaja Wangwe kauwawa na Mbowe. Kilichompata hakupata kukanyaga tena Mkoa wa Mara hadi anakufa.
Hivi huyo Mbowe nani anamuogopa kama sio nyinyi? Mnajua ni mbadhilifu wa fedha, kamuua Wangwe nk nk. Sasa mnashindwa nini kumshughulikia kisheria?
Huo ndio udhaifu sasa!
 
Ndugu zangu,

Hili wimbi la watia nia kuwa zaidi ya elfu 8, sio jambo la kawaida, inabidi tuliangalie kwa jicho la tatu. Unadhani sababu hasa ni nini????

1. Ukosefu wa ajira?!
Hii inaweza kuchangia kwa vile vijana wengi hawana ajira za kudumu. Inaweza kuangaliwa kwa baadhi ya wagombea ingawa sio wote kwa vile wamekosa kazi za maana serikalini na kuona wakajaribu ubunge.

2. Uminywaji wa Vyama Pinzani?!
Hii ni jambo pia la msingi sana. Binafsi hii ndio sababu kuu. Baada ya awamu hii kuvifinya vyama vingi, basi watu wamerud chama cha CCM na kugombea huko. Kwani ama wanaogopa hofu na maisha yao huko upinzani ama hawana uhakika wa kuishinda CCM wakigombea upinzani.

3. Tamaa kwa Viongoz ama Uwoga wa Kazi za Kuteuliwa na Raisi???
Ndio, hii nayo inawezakana ikawa sababu. Baadhi ya viongoz wamekimbia ofisi na kwenda kugombea ubunge. Nahisi wengi wao wameogopa bila kujua hatma yao ya baadae kutokana na kasi ya Rais na kuamua kugombea ubunge. Hii hasa kwa wateule MA-DC, DED, RC n.k.

4. Hulka ya kuongeza CV ili kuonekana na Raisi ili kuteuliwa mbeleni?!
Hii ipo, kuna baadhi ukiwauliza wanasema wanaongeza CV. Sababu kuu kwao ni kuweza waonekane kwani watia nia wengi 2015 walichaguliwa nafasi za DC, DED, DAS, n.k.

5. Maslahi ya Pesa ya Ubunge?!
Hapa napo kuna sababu ya msingi. Wengi wamepiga mahesabu kwa kuona hela nyingi zinamwagika bungeni. Hapa watu wenye kaz kama RCs au Wakurugenz wa Wizara, wameamua kwenda kugombea!

Mnadhani nini sababu wakuu, tujadiliane kwa hatima za siasa ya nchi yetu.
 
Kuelekea uchaguzi mkuu wa oktoba 2020, wagombea wengi sana wametia nia majimboni, sababu kuu ni hizi,

Kwanza ni Kipato kikubwa, ubunge unalipa sana, ndani ya miaka mitano tu mtu anapata pension zaidi ya million 200 , huku waajiiriwa wa kawaida wanasota wakiwa vijana hadi uzee kustaafu hawapati hiyo pesa, ubunge vilevile una mshahara mkubwa, posho etc, bila kujali elimu ya mtu, uwe STD Four graduate, STD seven, mshahara ni sawa na Prof na Phd holders. Ndio maana viongozi mbalimbali kama RCs,RASs,DCs,DEDs,DASs na waajiiriwa wengne ngazi za chini wameacha ofisi na kwenda kutia nia majimboni

Pili, watanzania wengi wako focused kwenye teuzi. Wengi wameshuhudia baadhi ya watia nia wa chama tawala waliofeli kupenya kwenye kura za maoni 2015,baadhi yao walipata teuzi.

Tatu, Ubunge inaonekana ni kazi nyepesi machoni mwa watu, mbunge akichaguliwa hamna sheria ya kumtengua, imradi awe na chama chake na ahudhuria vikao vya bunge, hata kama atasinzia miaka yote mitano akiwa bungeni na asifanye utekelezaji wowote ndani ya jimbo lake.

Unaweza ongeza sababu za mafuriko ya watia nia majimboni!
 
Wanabodi,

Tunapoelekea kwenye hatua ya kwanza ya uchaguzi kwa uchukuaji wa fomu za kugombea kwenye vyama vya siasa, kumejitokeza, uwingi wa mkubwa, wa wagombea kupitia CCM.

Huu ni uthibitisho wa kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na Rais, Dr. John Pombe Joseph Magufuli na awamu yake ya 5, na inayoendelea kufanywa kwa taifa letu la Tanzania, ikiwemo kupambana na rushwa, kuongeza uwajibikaji, kupaisha maendeleo ya nchi kwa maendeleo makubwa ya kuonekanika katika baadhi ya sekta, ikiwemo kulifufua shirika la ndege la Tanzania, ATCL, kujenga SGR, Stigler, barabara za juu kwa juu, elimu bure, kujenga Tanzania ya viwanda, kuiingiza nchi yetu kuwa ni nchi ya uchumi wa kati na mengine mengi makubwa mazuri, kulikopelekea Watanzania wengi wakiwemo wapinzani kumkubali JPM na kuikubali CCM, hivyo kuunga mkono juhudi kwa kumpenda JPM, kumkubali, na kuipenda CCM na kuifanya kukubalika sana, hivyo kwenye uchaguzi wa mwaka huu, kujikuta watu wengi kujitokeza kwa mamia kugombea jimbo moja mfano jimbo la Kawe, ili tuu kumuunga mkono rais Magufuli na kujitokeza kumsaidia.

Swali ni jee uchaguzi wa October ni uchaguzi wa kuchagua kwa kushindanisha vyama au kushindanisha wagombea, au ni tunakwenda tuu kwenye uchaguzi kuithibitisha tuu ushindi wa kishindo wa CCM, ambayo tayari imeishashinda uchaguzi Mkuu huu mioyoni mwa watu, na uchaguzi ni kwa ajili tuu ya kukamilisha taratatibu za uchaguzi, au kutakuwa na ushindani wa kweli wa kisiasa au CCM tuu huku ikisindikizwa na vyama vingine?.

Angalizo:
Wakati hata mimi nikiendelea kujishauri na kujiuliza, ndani ya siku mbili hizi, kama na mimi nijitose au laa, naomba kuwapa angalizo dogo, kuwa sio kila anayejitokeza kuchukua fomu kugombea ubunge au udiwani kupitia CCM, yuko very serious kugombea ili kupata ubunge au udiwani!, kuna baadhi wanagombea kwa sababu nyingine kabisa kadhaa wa kadha na wala sio kuutaka ubunge, udiwani au uwakilishi wa wananchi. Hivyo naombeni sana, mkisikia na mimi nimejitosa, msishangae!.

Kwa vile hili la kazi nzuri ya Rais Magufuli niliisha lizungumza humu tangu ile 2015, mara tuu baada ya uchaguzi, nikizungumzia uchaguzi Mkuu huu wa 2020, na sasa hii ndio 2020 yenyewe na uchaguzi wenyewe ndio huu, kuna haja ya kujikumbusha tu ile 2015 nilisema nini kuhusu Magufuli na uchaguzi wa 2020, na sasa hii 2020 ndio hii, nini kinatokea...

Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Na October yenyewe ndio hiyo inakuja, iko just around the corner, jee sasa tunakwenda kwenye uchaguzi kuchagua au ni kwenda tuu kuithibitisha kazi nzuri ya JPM na CCM tuu ili aendelee?.

Paskali
Anko Maghu,amefanya makubwa,Nidhamu utumishi wa umma,Wizi wa Tanzanite umezibitiwa kabisa.
Ila amearibu Diplomasia ya nje,Demokrasia imeshuka sana,watu ni waoga hata kuongea mtaani,
Bado kuna matumizi mabaya ya fedha tena ndani ya ofisi ya Raisi.msafara wake ni kufuru tupu.
Bunge limekua kituko,
Mwisho inabidi apunguze kuongelea ishu binafsi za watu,kama kuoa,kuolewa,mishahara ya watu,apunguze vulgar language,zenye matusi ndani yake,asipende kuhukumu hadharani,kusema huyu anatembea na wake za watu,zipo idara chini yake,zakufanya hayo.
Korosho,Mtwara ameburunda kabisa,Sekta binafsi imedorola sana tangu aingie,ni muda muhafaka kuiacha ishamiri,
Asipende sana kuabudiwa,TZ sio yake,wala anaowateua,na kuwapa nafasi,sio yeye anayewalipa mishahara,ni kodi za Wananchi,asitumie Teuzi,na kutumbua,kama fimbo ya kuwshikisha adabu asiowqpenda,.
Mwisho aache ubaguzi wa kikabila,na kikanda,
Kwa kauli alizowahi kutoa Gwajima,hakustahili kukalibishwa Ikulu,Madudu yote aliyofanya Makonda,hakutumbuliwa,Lakini Anne kilango kosa moja tu,alitumbuliwa fasta!
Inabidi ajue,TZ inawatu wengi wenye uwezo wa kufanya kazi ya uraisi kwa ubora Mara 100,zaidi yake,yeye sio Yesu wa TZ,
 
Brother pm unajikomba mpka unapitiliza bro,lizika na ulichikipata kwenye tathnia yako uteuzi upo na kufa kupo lakin ukifa kwa kusema ukweli naamini Mungu atakupokea,unaswma Magu ameirudisha nchi wakati wa Nyerere,kweli!! Aisee hv wakati wa Nyerere watu walipotezwa km kina ben wazwaz?wabunge walipigwa risasi km Lissu/Mbowe,je wanajeshi waliteuliwa kijinga kwenye teuz za hovyo,je Nyerere hakuongeza mishahara?Mr Mayara jaribu kuwa mkweli hatq sekunde basi,kika kipindi startv wewe ni kujikomba tu! Haya bwana subiri utwuzi lakin kumbuka kwa uongo na upotoshaji unaousema na kuufanya utalipwa ujira sawasawa na matendo yako.nakusalim.
 
Wanabodi,

Tunapoelekea kwenye hatua ya kwanza ya uchaguzi kwa uchukuaji wa fomu za kugombea kwenye vyama vya siasa, kumejitokeza, uwingi wa mkubwa, wa wagombea kupitia CCM.

Huu ni uthibitisho wa kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na Rais, Dr. John Pombe Joseph Magufuli na awamu yake ya 5, na inayoendelea kufanywa kwa taifa letu la Tanzania, ikiwemo kupambana na rushwa, kuongeza uwajibikaji, kupaisha maendeleo ya nchi kwa maendeleo makubwa ya kuonekanika katika baadhi ya sekta, ikiwemo kulifufua shirika la ndege la Tanzania, ATCL, kujenga SGR, Stigler, barabara za juu kwa juu, elimu bure, kujenga Tanzania ya viwanda, kuiingiza nchi yetu kuwa ni nchi ya uchumi wa kati na mengine mengi makubwa mazuri, kulikopelekea Watanzania wengi wakiwemo wapinzani kumkubali JPM na kuikubali CCM, hivyo kuunga mkono juhudi kwa kumpenda JPM, kumkubali, na kuipenda CCM na kuifanya kukubalika sana, hivyo kwenye uchaguzi wa mwaka huu, kujikuta watu wengi kujitokeza kwa mamia kugombea jimbo moja mfano jimbo la Kawe, ili tuu kumuunga mkono rais Magufuli na kujitokeza kumsaidia.

Swali ni jee uchaguzi wa October ni uchaguzi wa kuchagua kwa kushindanisha vyama au kushindanisha wagombea, au ni tunakwenda tuu kwenye uchaguzi kuithibitisha tuu ushindi wa kishindo wa CCM, ambayo tayari imeishashinda uchaguzi Mkuu huu mioyoni mwa watu, na uchaguzi ni kwa ajili tuu ya kukamilisha taratatibu za uchaguzi, au kutakuwa na ushindani wa kweli wa kisiasa au CCM tuu huku ikisindikizwa na vyama vingine?.

Angalizo:
Wakati hata mimi nikiendelea kujishauri na kujiuliza, ndani ya siku mbili hizi, kama na mimi nijitose au laa, naomba kuwapa angalizo dogo, kuwa sio kila anayejitokeza kuchukua fomu kugombea ubunge au udiwani kupitia CCM, yuko very serious kugombea ili kupata ubunge au udiwani!, kuna baadhi wanagombea kwa sababu nyingine kabisa kadhaa wa kadha na wala sio kuutaka ubunge, udiwani au uwakilishi wa wananchi. Hivyo naombeni sana, mkisikia na mimi nimejitosa, msishangae!.

Kwa vile hili la kazi nzuri ya Rais Magufuli niliisha lizungumza humu tangu ile 2015, mara tuu baada ya uchaguzi, nikizungumzia uchaguzi Mkuu huu wa 2020, na sasa hii ndio 2020 yenyewe na uchaguzi wenyewe ndio huu, kuna haja ya kujikumbusha tu ile 2015 nilisema nini kuhusu Magufuli na uchaguzi wa 2020, na sasa hii 2020 ndio hii, nini kinatokea...

Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Na October yenyewe ndio hiyo inakuja, iko just around the corner, jee sasa tunakwenda kwenye uchaguzi kuchagua au ni kwenda tuu kuithibitisha kazi nzuri ya JPM na CCM tuu ili aendelee?.

Paskali
Acha njaa shwain wewe
 
Paskal hiyo uliyosema wewe ni A, B yake ni kuwa kazi ya ubunge siku hizi imekuwa rahisi mno na haina maana tena kwa great thinkers mbali ya kujua kuandika na kusoma sifa kubwa kwa awamu hii ya tano ni kumsifu mtukufu na kumpongeza bungeni. Watu wengi wamejipima na kujiona sifa hii wanayo ndio maana wamechukua form. mmewaumiza sana waliona mawazo tofauti na ya Magu sasa mmeona mtakuwa peke yenu lakini hii sio kweli wananchi wataona.

Kama magu katekeleza ilani aliyoahidi mwenyewe sifa za nini, Magu anavisasi ndio maana wenye mawazo tofauti na yake wamekaa kimya sababu wanajua atawafanya nini mbeleni. Viongozi waandamizi wamekimbia vyeo vyao sababu Jiwe ahaminiki na kutumbua ni nje nje sasa kuliko kufanya kazi usio na uhakika wa kesho yake bora wakimbilie bungeni.

Mmezuia pensheni za wafanyakazi wasilipwe mafao yao kwa mkupuo lakini wabunge wakimaliza wao wanalipwa sasa nyie mliokuwa sekta binafsi pia mnakimbilia ubunge kupata uhakika wa maisha. Uchaguzi uliopita Jiwe alikuwa na tabia ya kuteua wote walioshindwa kura za maoni sasa Paskali ulitegemea watu wasijae kweli au ndio umetia pamba masikioni na kusingizia nyimbo zenu za siku zote kuwa flyover, ndege, etal ndio wananchi wanafurahia. Kama kweli kwanini mlimiminia watu risasi, wengine mliwatia katika viroba na kuwatosa majini. Vyombo vyote vya habari mmewafunga midomo mlifikiri wangapi wataenda Chadema ambao wanataka kesi mahakamani kwa miaka mitano.

Kazi aliyofanya JPM na CCM imetiwa doa na roho mbaya yake, kutokupenda ushindani wa kisiasa, visasi vya hovyo, kuamua peke yake kama kweli kafanya kazi nzuri mwambie aweke manunuzi ya serikali kwa miaka yake mitano hadharani na uliza PPRA lini walimkagua. Watu wanajitoa tena muhanga kupambana na CCM kudai katiba mpya, haki sawa kwa watu wote. Acacia walikuwa wanalipa kodi Bilioni moja kwa miezi mitatu jana wamelipa milioni 185 kwa miezi sita Nyang'hwale hizi taarifa wewe na wenzako hamuwezi na wala hamtaki kuzichambua ebu tafuta economic loss hapa kwa Nyang'hwale tu miaka 4 nyuma ndio mtajua nyie mnaosifia hamtumii akili zenu mnamseti mzee wa watu baada ya kujua uzaifu wake wa kupenda sifa. Haya machache ngoja atoke madarakani ndio mtapata akili.
 
Kama alivyosema askofu Bagonza, mpinzani anapojaza fomu kugombea nafasi toka chama cha upinzani vilevile anaandika wosia. Siasa za Tanzania awamu hii imekuwa uadui, kutekana na kubambikiwa kesi ukiwa mpinzani.
Utitiri CCM ni kujipendekeza kulinda maslahi. Wengi wanajua hawatoboi kura za maoni ila wanataka tu waonekane kuwa wao ni CCM ili wasisumbuliwe.
Hii iko wazi.
 
Back
Top Bottom