DALLAI LAMA
JF-Expert Member
- Jan 31, 2012
- 8,652
- 2,628
Tuanze na KALENGA,watu wasimame nyuma ya mgombea..CCM wanaturudisha nyuma ya wakati.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ccm ni kma kinyonga, kinaendeshwa kulingana na mahitaji ya kimaslai ktk wakati husika, i real hate this party.
Huna akili ww, unatakiwa utofautishe kura ya kumchagua mtu kma kiongoz na kura ya kupitisha kifungu flan kwa manufaa y taifa zima na watu wake
Sent from my iPhone using JamiiForums.
Tuanze na KALENGA,watu wasimame nyuma ya mgombea..CCM wanaturudisha nyuma ya wakati.
Huna akili ww, unatakiwa utofautishe kura ya kumchagua mtu kma kiongoz na kura ya kupitisha kifungu flan kwa manufaa y taifa zima na watu wake
Sent from my iPhone using JamiiForums.🔩🔨
Nimefuatilia sana malumbano yanayoendelea kwenye bunge maalum la Katiba kuhusu mambo mbalimbali,kama akidi,jinsi ya upigaji kura na mengine. Kwa leo nijadili kidogo tu kuhusu kura ya WAZI na SIRI.
Kwa namna yoyote ile kura ya WAZi ndio sahihi kutumika kwa sababu wajumbe ni wawakilishi wa watu wengine kwa hiyo hawapigi kura kwa dhamira zao binafsi ila kwa mujibu wa wale wanaowawakilisha. Kama mjumbe ametokana na jimbo la uchaguzi lazima apige kura kulingana na wananchi wake wanavyotaka hata kama yeye binafsi hapendi na lazima watu wake wajue kama mwakilishi wao amewawakilisha vilivyo na akienda kinyume na matakwa ya wananchi wake inabidi wananchi wamwajibishe moja kwa moja na wala sio chama chake.
Kwa wale wanaowakilisha vyama vya siasa ambao ni kama 42 hivi kila mmoja anatakiwa kupiga kura ya wazi kulingana na msimamo wa chama chake na akienda tofauti anastahili kuwajibishwa bila huruma kwani kura si ya kwake binafsi bali ni ya wale waliomtuma,kwa hiyo anawajibika kupigia kura msimamao wa waliomtuma hata kama yeye binafsi hakubaliani nao. Vivyo hivyo wabunge wa viti maalum wanawajibika kwa wanawake waliowapeleka huko na si vyama vyao, utaratibu ni huo huo kwa wale wa makundi maalum wanawajibika kupiga kura kwa matakwa ya waliowawakilisha na si kwa matakwa yao binafsi.
Watu wengi kwa sasa wanaogopa kura ya wazi kwa hofu kwamba watabanwa na misimamo ya vyama vyao,huu ni "uhuni" chama kinatakiwa kuwabana wawakilishi wao rasmi tu, ambao ni kama wawili watatu kwa kila chama wengineo wanabanwa na wale wanaowawakilisha,na kama mwakilishi rasmi wa chama akienda tofauti na msimamo wa chama huyo lazima awajibishwe ila sio mwanachama wa chama fulani anawakilisha wananchi wake hata wasio na vyama alazimike kufuata matakwa au msimamo wa chama chake.
Kwa mawazo hayo kama itapigwa kura ya siri wanachi watajuaje kama matakwa yao na si matakwa binafsi ya mwakilishi wao yamezingatiwa? Hebu tutafakari pamoja kwa nguvu ya hoja...
Kuhusu vitisho siwezi kulisemea sana maana hao CCM wamekanusha hilo kupitia kwa Nape kwenye gazeti la leo la Mwananchi, swali, je kama kura itakuwa ya siri huoni wajumbe watapiga kura kwa matakwa yao binafsi na si matakwa ya wanaowawakilisha?
Hivi wewe elimu yako ni ya darasa la ngapi?, hivi unashindwa kujua kwamba hakuna hata mjumbe mmoja ambaye anawakilisha wananchi?, ni lini umemchagua mtu na kumtuma dodoma kukuandikia katiba?, eti wawakilishi wao', wote walivyo ni yupi anayewajibika kwako au atakayewajibika kwako kwa michango atakayoitoa?, kumbuka vizuri kama uliwahi kumtuma mbunge wako aende kuandika katiba. Kama wewe ni kijana nina wasiwasi na taifa la kesho utakalolijenga.
Watapiga kura ya siri!.
Pasco
Tuwaone ili iweje kwenye hayo ni mashindano ya Miss Tanzania au ni ligi ya EPL?maana yoyote ya haki duniani ni kupiga kura kwa debe,mbona raisi /mwenyekiti/wajumbe wa mnec wa CCM wanachaguliwa kwa kura ya siri,mbona huko hawadai tuwaone,tuwaone kwa kipi mno?mambo ya lura za Mlolongo yamepitwa na wakati,kura ni kwa DEBE baaasi.Si CCM inapendwa woga wa nini ,akina Serukamba ,Chenge twendeni kwenye Debe.Wengi wetu hata huku tulipo hakuna umeme wala luninga. Na hata luninga ikiwepo nasikia TBC ni noma sana! Mnadhani tutawaonaje? Wanaosema tumewatuma kwa msimamo wa kura ya wazi ni waongo wanaotaka kupitisha hoja zao kwa hila. Twajua kuwa kura ya kidemokrasia ni ile ya siri!
Hakuna katiba mbili za kupigiwa kura bali kupigiwa kura maoni mbalimbali.huko Marekani kwenyewe kulipokomaa demokrasia bunge hupiga kura za wazi,kila mbunge anafahamika alivyopiga kura kwa miongo mingi kuhusu mambo yao kama umiliki wa silaha,vita, Israel.ndoa, mtoto tumboni mwa mama nk-Tuwaone ili iweje kwenye hayo ni mashindano ya Miss Tanzania au ni ligi ya EPL?maana yoyote ya haki duniani ni kupiga kura kwa debe,mbona raisi /mwenyekiti/wajumbe wa mnec wa CCM wanachaguliwa kwa kura ya siri,mbona huko hawadai tuwaone,tuwaone kwa kipi mno?mambo ya lura za Mlolongo yamepitwa na wakati,kura ni kwa DEBE baaasi.Si CCM inapendwa woga wa nini ,akina Serukamba ,Chenge twendeni kwenye Debe.
Ndugu fikiria zaidi kidogo.hicho chama cha wanasheria kina agenda zake.rasimu sio maoni yetu bali yale tume iliyoyaandika kutokana na maoni yetu na maoni yao.hivyo ni lazima bunge liondoe maoni ya wanatume kwa uwazi.Hiyo mdau si kweli! Kura huwa ni za siri, ni lini wabunge haww walienda kwa Wananchi kuhusu Katiba mpya? Ni tume tu ya mabadiliko ya Katiba ndiyo KISHERIA ilienda kwa Wananchi kukusanya maoni, hayo mengine ni mazingaombwe tu. Na ndiyo maana TLS yaani Chama cha Wanasheria Tanganyika wametoa tamko kuwa kwa kuwa Bunge Maalum la Katiba kama chombo au mjumbe mmoja mmoja hawana mamlaka yoyote ya kubadili Maoni halali ya Wananchi kama yalivyo kwenye RasimuII, kwa kuwa wao hawajakusanya maoni kwa wananchi( Tafuta ,,gazeti la Mwananchi la Alhamisi au Ijumaa ya wiki hii inayoisha leo kama sikosei Ukurasa wa 31 kuna andiko hilo).

Ndugu fikiria zaidi kidogo.hicho chama cha wanasheria kina agenda zake.rasimu sio maoni yetu bali yale tume iliyoyaandika kutokana na maoni yetu na maoni yao.hivyo ni lazima bunge liondoe maoni ya wanatume kwa uwazi.