Wito kwa Bunge la Katiba: Kura iwe ya Siri kwasababu Hakuna aliyetumwa na Watu Kuwawakilisha!

Wito kwa Bunge la Katiba: Kura iwe ya Siri kwasababu Hakuna aliyetumwa na Watu Kuwawakilisha!

Tuanze na KALENGA,watu wasimame nyuma ya mgombea..CCM wanaturudisha nyuma ya wakati.
 
ccm ni kma kinyonga, kinaendeshwa kulingana na mahitaji ya kimaslai ktk wakati husika, i real hate this party.
 
Huna akili ww, unatakiwa utofautishe kura ya kumchagua mtu kma kiongoz na kura ya kupitisha kifungu flan kwa manufaa y taifa zima na watu wake

Sent from my iPhone using JamiiForums.🔩🔨
 
ccm ni kma kinyonga, kinaendeshwa kulingana na mahitaji ya kimaslai ktk wakati husika, i real hate this party.

Wakati huo huo wanakuwa na hoja ya Msingi sana. Watu wamekaa bungeni kwenye viti Tv zinarusha, wananchi wanataka kuona kinachoendelea,SIRI ya nini?
 
Huna akili ww, unatakiwa utofautishe kura ya kumchagua mtu kma kiongoz na kura ya kupitisha kifungu flan kwa manufaa y taifa zima na watu wake

Sent from my iPhone using JamiiForums.

mkuu humu JF kuna watanzania na CHADEMA, huyo siyo mtanzania ni CHADEMA.
 
Huna akili ww, unatakiwa utofautishe kura ya kumchagua mtu kma kiongoz na kura ya kupitisha kifungu flan kwa manufaa y taifa zima na watu wake

Sent from my iPhone using JamiiForums.🔩🔨

Haya ndio matokeo ya kukaririshwa na akina Zakia Meghji bila kutafakari. Na wewe eti unajiona umetoa BONGE LA POINTI. Shame on your face. Kwani tukapopigia kura za NDIYO AU HAPANA (read referendum) ya rasimu ya katiba mpya tutakuwa tunachagua mtu/kiongozi kwa mawazo yako?! Go back to the drawing board dude! Ulicho argue hapa is alter nonsense! Hang on for a second nimesahau kwamba wewe ni mwana-CCM hivyo you're absolute correct referendum ni ya kuchagua viongozi wa CCM. Poor me!
 
Mkuu ccm wasikuumize kichwa dawa yao ishaiva imebaki kupakuwa tu
 
kura ya wazi haifai kuna wabunge wengine bendera hufata upepo watafata kauli z mabosi wao.
 
Nimefuatilia sana malumbano yanayoendelea kwenye bunge maalum la Katiba kuhusu mambo mbalimbali,kama akidi,jinsi ya upigaji kura na mengine. Kwa leo nijadili kidogo tu kuhusu kura ya WAZI na SIRI.

Kwa namna yoyote ile kura ya WAZi ndio sahihi kutumika kwa sababu wajumbe ni wawakilishi wa watu wengine kwa hiyo hawapigi kura kwa dhamira zao binafsi ila kwa mujibu wa wale wanaowawakilisha. Kama mjumbe ametokana na jimbo la uchaguzi lazima apige kura kulingana na wananchi wake wanavyotaka hata kama yeye binafsi hapendi na lazima watu wake wajue kama mwakilishi wao amewawakilisha vilivyo na akienda kinyume na matakwa ya wananchi wake inabidi wananchi wamwajibishe moja kwa moja na wala sio chama chake.

Kwa wale wanaowakilisha vyama vya siasa ambao ni kama 42 hivi kila mmoja anatakiwa kupiga kura ya wazi kulingana na msimamo wa chama chake na akienda tofauti anastahili kuwajibishwa bila huruma kwani kura si ya kwake binafsi bali ni ya wale waliomtuma,kwa hiyo anawajibika kupigia kura msimamao wa waliomtuma hata kama yeye binafsi hakubaliani nao. Vivyo hivyo wabunge wa viti maalum wanawajibika kwa wanawake waliowapeleka huko na si vyama vyao, utaratibu ni huo huo kwa wale wa makundi maalum wanawajibika kupiga kura kwa matakwa ya waliowawakilisha na si kwa matakwa yao binafsi.

Watu wengi kwa sasa wanaogopa kura ya wazi kwa hofu kwamba watabanwa na misimamo ya vyama vyao,huu ni "uhuni" chama kinatakiwa kuwabana wawakilishi wao rasmi tu, ambao ni kama wawili watatu kwa kila chama wengineo wanabanwa na wale wanaowawakilisha,na kama mwakilishi rasmi wa chama akienda tofauti na msimamo wa chama huyo lazima awajibishwe ila sio mwanachama wa chama fulani anawakilisha wananchi wake hata wasio na vyama alazimike kufuata matakwa au msimamo wa chama chake.

Kwa mawazo hayo kama itapigwa kura ya siri wanachi watajuaje kama matakwa yao na si matakwa binafsi ya mwakilishi wao yamezingatiwa? Hebu tutafakari pamoja kwa nguvu ya hoja...

HAMNA KURA YA SIRI WALA UWAZI NI KUDANGANYANA TU

baada nyerere kuivamia zanzibar january 1964 , aliwakamata mawaziri wote pamoja na waziri mkuu wa zanzibar na kuwafunga jela za tanganyika , kabla ya huo aliouita muungano

jee hapa kuna muungano wa nchi mbili au huu ni uvamizi

tunataka kuifanya haramu kuwa ni halali ??

Hii kitu haiwezi kuwa milele ,

tanganyika iwaombe radhi wazanzibari na kuwaachia waangalie wenyewe wafanye nini na sio kukaa dodoma na kujipakazia katiba mpya
 
Kuhusu vitisho siwezi kulisemea sana maana hao CCM wamekanusha hilo kupitia kwa Nape kwenye gazeti la leo la Mwananchi, swali, je kama kura itakuwa ya siri huoni wajumbe watapiga kura kwa matakwa yao binafsi na si matakwa ya wanaowawakilisha?

Hiyo mdau si kweli! Kura huwa ni za siri, ni lini wabunge haww walienda kwa Wananchi kuhusu Katiba mpya? Ni tume tu ya mabadiliko ya Katiba ndiyo KISHERIA ilienda kwa Wananchi kukusanya maoni, hayo mengine ni mazingaombwe tu. Na ndiyo maana TLS yaani Chama cha Wanasheria Tanganyika wametoa tamko kuwa kwa kuwa Bunge Maalum la Katiba kama chombo au mjumbe mmoja mmoja hawana mamlaka yoyote ya kubadili Maoni halali ya Wananchi kama yalivyo kwenye RasimuII, kwa kuwa wao hawajakusanya maoni kwa wananchi( Tafuta gazeti la Mwananchi la Alhamisi au Ijumaa ya wiki hii inayoisha leo kama sikosei Ukurasa wa 31 kuna andiko hilo).
 
Hivi wewe elimu yako ni ya darasa la ngapi?, hivi unashindwa kujua kwamba hakuna hata mjumbe mmoja ambaye anawakilisha wananchi?, ni lini umemchagua mtu na kumtuma dodoma kukuandikia katiba?, eti wawakilishi wao', wote walivyo ni yupi anayewajibika kwako au atakayewajibika kwako kwa michango atakayoitoa?, kumbuka vizuri kama uliwahi kumtuma mbunge wako aende kuandika katiba. Kama wewe ni kijana nina wasiwasi na taifa la kesho utakalolijenga.

Hata mi nawashangaa watu wanaosema wawakilishi, ni lini mbunge wa jimbo alikuja kunadi sera zake kuhusu katiba mpya. Kwa mfano, wabunge wa Chama Tawala haikuwa ndani ya Ilani yao, ni busara za Mwenyekiti tu ndo tumepata angalu kuanza mchakato huu, wenzake wengi hawakutaka katiba mpya, sasa huo uwakilishi unatoka wapi? Au uwakilishi wa kupinga, ambao hata ikiwa kura ya Siri si watapinga tu, wanachohofia ni nini?!
 
Anayetaka kupiga kura ya wazi apewe nafasi hiyo na anayetaka ya siri pia. Halafu zijumlishwe.haki kwa kila mjumbe
 
Pasco mwambie huyo Chenge,aache uimla asijifanye uweledi wake wa sheria ndio iwe kisa cha kutaka kuburuza hao wajumbe kwa kura ya wazi,kwanza hana sifa yoyote ya kujidai eti kuwatetea Watanzania,wakati yeye ndie kafanya maisha ya Watanzania kuwa mabaya kwa kutuingiza kwenye mikataba mibovu ikiwemoya Radar,IPTL na mingineo ,ashukuru kazaliwa Tanzania na si China,hata HAYA hana.
 
Wengi wetu hata huku tulipo hakuna umeme wala luninga. Na hata luninga ikiwepo nasikia TBC ni noma sana! Mnadhani tutawaonaje? Wanaosema tumewatuma kwa msimamo wa kura ya wazi ni waongo wanaotaka kupitisha hoja zao kwa hila. Twajua kuwa kura ya kidemokrasia ni ile ya siri!
Tuwaone ili iweje kwenye hayo ni mashindano ya Miss Tanzania au ni ligi ya EPL?maana yoyote ya haki duniani ni kupiga kura kwa debe,mbona raisi /mwenyekiti/wajumbe wa mnec wa CCM wanachaguliwa kwa kura ya siri,mbona huko hawadai tuwaone,tuwaone kwa kipi mno?mambo ya lura za Mlolongo yamepitwa na wakati,kura ni kwa DEBE baaasi.Si CCM inapendwa woga wa nini ,akina Serukamba ,Chenge twendeni kwenye Debe.
 
Hakuna katiba mbili za kupigiwa kura bali kupigiwa kura maoni mbalimbali.huko Marekani kwenyewe kulipokomaa demokrasia bunge hupiga kura za wazi,kila mbunge anafahamika alivyopiga kura kwa miongo mingi kuhusu mambo yao kama umiliki wa silaha,vita, Israel.ndoa, mtoto tumboni mwa mama nk-
 
Hiyo mdau si kweli! Kura huwa ni za siri, ni lini wabunge haww walienda kwa Wananchi kuhusu Katiba mpya? Ni tume tu ya mabadiliko ya Katiba ndiyo KISHERIA ilienda kwa Wananchi kukusanya maoni, hayo mengine ni mazingaombwe tu. Na ndiyo maana TLS yaani Chama cha Wanasheria Tanganyika wametoa tamko kuwa kwa kuwa Bunge Maalum la Katiba kama chombo au mjumbe mmoja mmoja hawana mamlaka yoyote ya kubadili Maoni halali ya Wananchi kama yalivyo kwenye RasimuII, kwa kuwa wao hawajakusanya maoni kwa wananchi( Tafuta ,,gazeti la Mwananchi la Alhamisi au Ijumaa ya wiki hii inayoisha leo kama sikosei Ukurasa wa 31 kuna andiko hilo).
Ndugu fikiria zaidi kidogo.hicho chama cha wanasheria kina agenda zake.rasimu sio maoni yetu bali yale tume iliyoyaandika kutokana na maoni yetu na maoni yao.hivyo ni lazima bunge liondoe maoni ya wanatume kwa uwazi.
 
Agenda gani hizo?
 
Back
Top Bottom