Wito kwa Watanzania kumfata Sheikh wetu Ponda Issa Ponda kwa kukiunga mkono chama cha ACT wazalendo

Msimu wa Uchaguzi unapofika kila tabaka lilotajwa ktk katiba kama vile Dini, Kabila, Rangi, Eneo, Jinsi, Walemavu nk wana haki ya kutathmini ni ilani ya chama gani inayolinda maslahi yao.

Kwani kura hupigiwa chama kilichoahidi kutetea maslahi yenu matabaka yote. Na hasa matabaka ya jamii ya walio wengi.

Hata hivyo watu wa kawaida layman hawana uwezo wa kufanya uchambuzi huo ila kwa kupitia viongozi wao wanaowaamini.

Sheikh Ponda historia imeandika ndiye kiongozi pekee anaekubaliwa au mwenye wafuasi wengi wa tabaka la kiislam.

Kajipamvanua kwa mwongo mmoja kuwa ni mtetezi dhidi ya ubaguzi na ukandamizwaji unaofanywa na wahalifu waliojificha ndani ya ofisi za Ummah (serikali) dhidi ya Waislamu na Uislam.

Niwakumbushe nguvu aliyonayo. Ktk kampeni za uchaguzi mwaka 2020 alitoa fupi tu kuwa waislam wamekubaliana kumpigia Kura kiti cha Urais mgombea wa CHADEMA Mh Tundu Lissu. Kauli iliyosababisha mgombea mmoja kuacha kampeni na kwenda kusimamia zoezi la kupanga matokeo mezani.

Huyu ndio Sheikh Ponda ambae muda wa kampeni ukifika atatoa Rasmi mwongozo wa chama gani Chenye maslahi kwa waislam ktk uchaguzi mkuu 2025.

Na atatoa kauli kwa kujivua dhima kwa Mungu kwanini ni haram kumchagua Mwanamke kuwa Rais.

Kwamba sheria ya kiislam inaruhusu mgombea mwanamme wa tabaka lolote, dini yyt sharti awe mwanamme.

Hivyo wito inatolewa kuungana na Sheikh wetu Mkuu Ponda Issa Ponda kwa kukiunga mkono chama cha ACT wazalendo
Sheikh kwani kidini uchaguzi wa hizi serikali zetu ni halali?
 
Nchi nyingi zilizojipambanua hazina dini zilizoendelea na kubagua baadhi ya dini.

Kama si kosa kwa watu wa tabaka fulani kama dini, kabilq kuunga mkono moja ya chama wanachoona kina maslahi kwao. Basi si sahihi kufikiri matakwa yako ndio yanayopaswa kufatwa hata kama hayana tija kwetu.

Unasema tupiganie maslahi ya watz ni yapi, wakati ccm inawatenga waislam ktk teuzi.

Kwanini takwimu zaonyesha hakuna mtz mwenye asili ya asia kwa mfano aliyewahi kupata uteuzi kutoka kwa Rais. Je hawana weledi, kwanini 75% ya wanaoteuliwa ni wakristo tokea uhuru na 25% au chini ya hapo ni waislam. Nafasi za mawaziri, makatibu wakuu. Je waislam hawana weledi.

Maslahi gani utayoyaota ya watz wakati mikoa yenye waislam wengi kama mikoa ya kusini imetengwa na miradi ya maendeleo. Hakuna BBT, Hakuna Reli ya aina yyt, hakuna chuo kikuu, hakuna uwanja wa ndege wa kimataifa, hakuna hospitali ya rufaa, hakuna mkakati wa kupeleka viwanda,

Kwanini sheria ya ugaidi imewahusu wakristo Mbowe na Rwakatare pekee na zaidi ya waislam 300 wamekamatwa.

Ccm imetubagua kupita maelezo.
View: https://youtu.be/obOYhW6LJUI?si=jG5ZLhuj6rSjlicJ

Hivyo ili waislam wajikomboe tutafata katiba si matakwa yenu. Na katiba haikarazi wasukuma kumfata Magufuli, wapemba kumfata Samia, ni kama vile wakristo walivyomuunga mkono Mwandishi wa habari mpaka na badae padre Slaa na kumuacha profess wa uchumi wakati ule Lipumba.

Hivi ni kwanini ndege wote walie akilia bundi uchuro

Hapo kichwani sijui umejaza nini maalim, even your thoughts need a GPS to find each other.
 
Wewe ni muislam, ulishawahi kubambikiwa hayo makosa ya u gaidi? Umesema 2020 sheikh Ponda alitoa muelekeo kuwa waislam mmeiunga mkono CHADEMA, kisha hapa unasema si CHADEMA wala CCM wenye mpango wa kubadilisha hiyo sheria ya u gaidi hauoni kama nyinyi waumini ni bendera fuata upepo?

Kuna wengine hatuamini katika mungu wala dini, sasa viongozi watakaochaguliwa wakiwa na akili kama zako si mnaweza mkaishia kutuua tu ili mpate thawabu kwa allah?
Kwa hiyo ninyi MSI na dini ndio mna haki ya kufata matakwa yenu ndugu.

Hebu rejea maudhui makuu ya andiko langu.

kila watu tabaka ni jukwaa la mabadiliko. Iwe chama, iwe dini.

Lengo ni kumuondoa mkoloni kwa kila jukwaa kutumia matakwa yao ilimradi tu hatuunji katiba.

Kama huundi mkono usinizuie.

Hakuna abaetangaza kuuwa, bali tunapigania kujitoa ktk lakucha ya wale wanaobagua, walevi, watekaji, wasagaji waliojificha ndani ya ccm
 
Ndugu kwa hiyo unapendekeza nini.

Kwamba kwa vile sheria ya ugaidi pamoja na kuwabagua waislam iendelee kuwepo kwa kuwa waislam ni watu wa amani.

Na sheria za tume ya uchaguzi zibaki kama zilivyo ili kulinda amani. Kwani ni nani anaetaka kuvuruga amani kati ya aliyekabidhiwa silaha. Na yule anaetaka kuiondoa serikali ya kibaguzi kwa kutumia kura.
Sijapendekeza lolote kati ya uliyoorodhesha. Langu ni kuelewesha tu kuwa dini unayoishadidia, uislamu au ukristu, ni matokeo hasi ya utumwa na ukoloni. Ni ajali ya kihistoria na kijiografia. Wala wewe kuwa muislamu au mkristu halikuwa chaguo lako bali umejikuta tu umezaliwa na wazazi waliojikuta ni waislamu/wakristo kwa sababu nilizozitaja. Hivyo tutulize vichwa tutafute namna ya kujikomboa kutoka utumwa huu wa kifikra, tujitambue kama waafrika/watanzania na si kwa lebo ya uislamu/ukristo waliotuwekea wazungu na waarabu. Kamwe waarabu au wazungu hawatatuona kuwa ni wenzao kwa kujivika imani zao. Ukitaka kuthibitisha hili jaribu kubisha hodi kwa nyumba ya mwarabu siku ya Idd au Maulid uwaeleze kuwa wawe ni muislam mwenzao
 
Msimu wa Uchaguzi unapofika kila tabaka lilotajwa ktk katiba kama vile Dini, Kabila, Rangi, Eneo, Jinsi, Walemavu nk wana haki ya kutathmini ni ilani ya chama gani inayolinda maslahi yao.

Kwani kura hupigiwa chama kilichoahidi kutetea maslahi yenu matabaka yote. Na hasa matabaka ya jamii ya walio wengi ndio hushinda.

Hata hivyo watu wa kawaida layman hawana uwezo wa kufanya uchambuzi huo ila kwa kupitia viongozi wao wanaowaamini.

Sheikh Ponda historia imeandika ndiye kiongozi pekee anaekubaliwa au mwenye wafuasi wengi wa tabaka la kiislam.

Kajipamvanua kwa mwongo mmoja kuwa ni mtetezi dhidi ya ubaguzi na ukandamizwaji unaofanywa na wahalifu waliojificha ndani ya ofisi za Ummah (serikali) dhidi ya Waislamu na Uislam.

Niwakumbushe nguvu aliyonayo. Ktk kampeni za uchaguzi mwaka 2020 alitoa fupi tu kuwa waislam wamekubaliana kumpigia Kura kiti cha Urais mgombea wa CHADEMA Mh Tundu Lissu. Kauli iliyosababisha mgombea mmoja kuacha kampeni na kwenda kusimamia zoezi la kupanga matokeo mezani.

Huyu ndio Sheikh Ponda ambae muda wa kampeni ukifika atatoa Rasmi mwongozo wa chama gani Chenye maslahi kwa waislam ktk uchaguzi mkuu 2025.

Na atatoa kauli kwa kujivua dhima kwa Mungu kwanini ni haram kumchagua Mwanamke kuwa Rais.

Kwamba sheria ya kiislam inaruhusu mgombea mwanamme wa tabaka lolote, dini yyt sharti awe mwanamme.

Hivyo wito inatolewa kuungana na Sheikh wetu Mkuu Ponda Issa Ponda kwa kukiunga mkono chama cha ACT wazalendo
Takbiiiiiiirrrrrr!!!
 
Nimekuelewa kuwa Ujamaa, Ubepari, Usekyula ni dhana si za kwetu tumeletewa na wazungu.

Kwa maana turudi kwenye ujumla ili turejee kwenye asili yetu.

My friend. Kuna maneno yamezoeleka kutamkwa kwa jamii. Ikiwemo neno Udini, dini tumeletewa. Na kuna maneno hatujazoea kuyatamka. Na yakiletwa huwa ni kama nuru. Akili haipokei kwa haraka. Kama vile ukipigwa nuru ukiwa ktk giza.

Neno Dini kwa tz ni kama jinai. Lkn ukisoma katiba hiki nilichosema si kosa ya jinai wala madai. Kwani dini ni imani, mama vile Ujamaa ni imani.

Na hakuna mtu aweza kuishi bila imani. Swali la msingi je tuna imani ambayo ni universal? Kama taifa. Kama hakuna kwanini sasa matakwa yako kulazimisha kuwa ndio mwongozo wa nchi.

Kwa muda mrefu tumekuwa ccm wanatumazimisha imani ya Ujamaa iwe ndio imani ya nchi.

Lkn moja ya matakwa ya imani hii ya Ujamaa (marxi) inasema ili tupate maendeleo tunapaswa kukubali kuwa Mungu hayopo. Na kwamba dini ni uratibu. Je imani hii ni universal.

Sasa mimi sitaki kwenda huko. Bali matakwa yangu au yetu ni kutaka kukiondoa chama cha Mapinduzi kwa kutumia watu ambao hawaamini, si mlevi, si mzinzi atuelekeze njia ya kuiondoa ccm. Kwanini iwe UCHURO.
 
What the heal is this.

Hao wote ni wafuasi wa imani ya Ujamaa.

Sisi ni wafuasi wa Imani ya Unyenyekevu (Uislam)

Hii comment imeonyesha jinsi ulivyo na akili ndogo
Ujamaa unauhusiano gani na uislamu au ubepari sababu kinyume cha ujamaa ni ubepari

Ukiangalia ukarimu wa dini ya kislamu unaendana na ujamaa kuliko ubepari
Iweje leo ujamaa uwe mbaya kwa uislamu

Tanzania viongozi ni mabilionea unasema ni wajamaa
 
Kwa hiyo chadema kutoteuwa wajumbe wa kamati kuu waislam ni ubaguzi? Achilia mbali wale waliochaguliwa kwa kuwa ni wazanzibar

..sio kweli.

..Mwenyekiti wa Taifa Bawacha ni Muislamu.

..pia kuna Mjumbe wa Kamati Kuu wa kuteuliwa na Mwenyekiti ni Muislamu.

..Chadema hakuna Udini pale, ni suala la mhusika kuwa tayari kukabiliana na mateso ya vyombo vya dola, mahakama, na msajili.

..Hata Shekhe Ponda alipowataka Waislamu wamchague Lissu mwaka 2020 alijua chama hicho hakibagui.
 
Hii comment imeonyesha jinsi ulivyo na akili ndogo
Ujamaa unauhusiano gani na uislamu au ubepari sababu kinyume cha ujamaa ni ubepari

Ukiangalia ukarimu wa dini ya kislamu unaendana na ujamaa kuliko ubepari
Iweje leo ujamaa uwe mbaya kwa uislamu

Tanzania viongozi ni mabilionea unasema ni wajamaa
Pata somo kidogo.

Imani na itikadi ya Ujamaa inaendelea kutawala. Lkn uchumi wa kijamaa ndio umekufa, umeshindwa.

Ndio maana waona serikali inaongozwa kiimla.

Sasa ni kweli Ujamaa na Uislam unafanana sana.

Tofauti iliopo ni ktk itikadi. Wakati Ujamaa unaamini hakuna Mungu, hivyo kila kitu tunamalizana tukiwa hai. Uislam unaamini Uwepo wa Mungu.

Hivyo hata serikali tutakayoioendekeza chini ya ACT ni Taifa Moja, Imani zote, Chini ya Mungu
 
..sio kweli.

..Mwenyekiti wa Taifa Bawacha ni Muislamu.

..pia kuna Mjumbe wa Kamati Kuu wa kuteuliwa na Mwenyekiti ni Muislamu.

..Chadema hakuna Udini pale, ni suala la mhusika kuwa tayari kukabiliana na mateso ya vyombo vya dola, mahakama, na msajili.

..Hata Shekhe Ponda alipowataka Waislamu wamchague Lissu mwaka 2020 alijua chama hicho hakibagui.
Mwenyekiti bawacha coincides ni Muislam. Lkn walichaguliwa kwasababu ni Mzanzibar
 
Katiba bora ni ile ambayo imekusanya matakwa ya kila tabaka. Na mfano wa katiba bora ni ya Afrika kusini ambayo hata vyama vya kitamaduni (dini) vinaruhusiwa. UNIVERSAL LAWS. Je tz tunafata Universal law au Matakwa ya nani. Ni makwata ya katiba, makatwa ya katiba yanayotokana na matabaka yote?

Ilani bora ya chama ni ile iliyokusanya maslahi ya matabaka mengi na hasa matabaka makubwa (population).

Msimu wa Uchaguzi unapofika kila tabaka lilotajwa ktk katiba kama vile Dini, Kabila, Rangi, Eneo, Jinsi, Walemavu nk wana haki ya kutathmini ni ilani ya chama gani inayolinda maslahi yao.

Kwani kura hupigiwa chama kilichoahidi kutetea maslahi yenu matabaka yote. Na hasa matabaka ya jamii ya walio wengi ndio hushinda.

Hata hivyo watu wa kawaida layman hawana uwezo wa kufanya uchambuzi huo ila kwa kupitia viongozi wao wanaowaamini.

Sheikh Ponda historia imeandika ndiye kiongozi pekee anaekubaliwa au mwenye wafuasi wengi wa tabaka la kiislam.

Kajipamvanua kwa mwongo mmoja kuwa ni mtetezi dhidi ya ubaguzi na ukandamizwaji unaofanywa na wahalifu waliojificha ndani ya ofisi za Ummah (serikali) dhidi ya Waislamu na Uislam.

Niwakumbushe nguvu aliyonayo. Ktk kampeni za uchaguzi mwaka 2020 alitoa fupi tu kuwa waislam wamekubaliana kumpigia Kura kiti cha Urais mgombea wa CHADEMA Mh Tundu Lissu. Kauli iliyosababisha mgombea mmoja kuacha kampeni na kwenda kusimamia zoezi la kupanga matokeo mezani.

Huyu ndio Sheikh Ponda ambae muda wa kampeni ukifika atatoa Rasmi mwongozo wa chama gani Chenye maslahi kwa waislam ktk uchaguzi mkuu 2025.

Na atatoa kauli kwa kujivua dhima kwa Mungu kwanini ni haram kumchagua Mwanamke kuwa Rais.

Kwamba sheria ya kiislam inaruhusu mgombea mwanamme wa tabaka lolote, dini yyt sharti awe mwanamme.

Hivyo wito inatolewa kuungana na Sheikh wetu Mkuu Ponda Issa Ponda kwa kukiunga mkono chama cha ACT wazalendo
Na inshallah aanguke mweleka wa mende tena kwa pua. Aaamin.
 
Mwenyekiti bawacha coincides ni Muislam. Lkn walichaguliwa kwasababu ni Mzanzibar

..hapana.

..yule Mama Muislamu kawashinda vigogo haswa wa Chadema akiwemo Susan Kiwanga, na mgombea aliyetangaza wazi kuwa anamuunga mkono Tundu Lissu.

..Chadema hakuna udini, unachohitaji ni utayari wa kuvumilia mateso na dhuluma toka jeshi la Polisi, Usalama, Msajili, na Mahakama.

..Na Lissu ndiye mgombea Uraisi pekee aliyewatetea Mashekhe wa Answar Sunna, Uamsho, pamoja na Wazanzibari waliouwawa toka zama za Sheikh Abeid Karume.
 
Nimekuelewa. Kwahiyo yule dada yetu walichaguliwa kwa kura. Hoja yangu ni nafasi za teuzi za kamati kuu.
 
Back
Top Bottom